....inawezekana huko juu wapi ambao wamesha dadavua shida tuliyonayo.
...Hakuna sayansi yeyote ile kubwa ya kufanya Design ya Bandari. Bandari zote zilizokwepo duniani zinatumia dizaini hiyo hiyo iiliyotumiwa in entiquities.
....Nauliza ni kwanini tukope, kutengeneza miundombinu? Kuna sababu gani ya kufanya hivyo? nauliza kwasababu hoja zinazoibuliwa ya kwanini "Wawekezaji" au umuhimu wa uwepo wa Private Public relationship ni Kuongeza Ufanisi; Kwamba kwa sababu wana hela basi sio rahisi kwao kujiibia, kwamba wanafanya kwa werevu na weledi mkubwa sana kuhakikisha kunapatikana faida tu!
Nauliza tena, Kwanini badala yaa kukopa na kufanyia ukarabati(mfano ukarabati wa mkongo wa umeme wa matrilioni)(tetesi inafuatia kuuzwa) tusiwaachie waje wajenge hizo miuondombinu wenyewe, au waanzishe kampuni au mashirika au viwanda wenyewe.....yaani kwanini Serikali ifanye uwekezaji(investment) kwa kitu iliyofanyia upembuzi yakinifu halafu ikaja kushindwa kutekeleza maazimio na azma ya miradi yao, shida ipo wapi?
Kwanini wasibakie kuwa ni arbiters kwanini wasibakie kuwa ni Insurers?
Isitoshe hakuna mengi mapya ambayo wawekezaji huwa wanaongeza zaidi ya Mtaji/fedha na maarifa tu, kwani wafanyakazi wanabakia ni wale wale tu! Na mara nyingi huwapunguza(naamini fika watafukuzwa wengi tu bandarini) Majengo na miundombinu ya eneo yanabakia ni yale yale? Na Madeni yanabakia pale pale tu! Yaani yale mamikopo tuliyachukua kuendeleza Bandari yanabakia pale pake! Maikopo tunayochukua kurakabisha sijui umeme yatabakia pale pale....halafu anakuja mtu kuchukua faida yake kwanza kabla hajaweza kukulipa hata ka ushuru kidogo!
....ngoja ninywe uji nilale
Mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Wenzetu Watanganyika washalitumbua jipu, sasa ni zamu yetu Wazanzibari kuukamua usaha mpaka tuufikie moyo wake na kuliponya moja kwa moja jeraha.
Ingefaa tuwaulize wenzetu, kama wao wameumia mno kwa kuona uhuru na rasilimali zao zimeingia hatarini kwa mkataba mmoja TU wa bandari, wanadhani wametuumiza kwa kiasi gani sisi wenzao kwa miaka 60 yote hii tangu walipoupora uhuru na mamlaka yetu YOTE na kutudumaza kiustawi kwa kutufungia njia kuu za kiuchumi.
Wanaumia kuona Mzanzibari anakuwa rais wa Tanzania hata kama ni kisheria na kikatiba, wakati wao wamejipa mamlaka ya kimabavu, kwa miaka yote hii ya kutupangia nani atuongoze Wazanzibari na kwa mipaka gani ya mamlaka!
Tuwathibitishie kwamba iwe iwavyo, sasa tumeshabaini bila chembe ya shaka, kwa yaliyotoka kwenye ndimi zao, kwamba wana chuki kubwa dhidi ya Uarabu na Uislamu na kwamba chuki hizo ndizo zilizochangia pia kutubana tusifurukute ndani ya 'muungano'; na ndio maana kina Lukuvi na Sitta hawakuulizwa chochote na yeyote waliponena waliyoyanena dhidi ya Uarabu na Uislamu, kwa sababu waliwasilisha na kuwakilisha mtazamo rasmi wa Tanganyika kuhusiana na Wazanzibari katika muungano.
Na kwa hapa tulipofika tukubaliane kwamba, kama ni kuuendeleza muungano, basi hakuna mbadala mwingine wa mahusiano yetu ya kisiasa na Watanganyika isipokuwa kufuta kwanza jina Tanzania na kurudi kwenye
Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuamua ama kuwa na muungano wa mkataba au wa serikali tatu. Ghairi ya hivyo ni kila nchi kurudi kwenye asili yake ya taifa na nchi kamili