Population ya Dubai ni milioni 3.5M na Tanzania ni milioni 63, ina maana hakuna kabisa watu wa ku-design Bandari?

Population ya Dubai ni milioni 3.5M na Tanzania ni milioni 63, ina maana hakuna kabisa watu wa ku-design Bandari?

20230609_000710.jpg
 
Jamani Hela tunazo,wasomi tunao .Tatizo ni nini?Na karne hii tuna uwezo kabisa wa kuangalia hizo Bandari kama Shangai,Singapore zimefanya nini hadi kuwa na ufanisi?Wachina ,wasingapore wazungu wa Roterdam na Antwerp wamevanya fanya nini?Kulikuwa na Haja ya kumleta huyu katili Sheikh wa Dubai kuwekeza kwetu?Wale ni pesa tu.

Kwanza tujiulize,watalipa kodi ama?Wenye mkataba uwekeni basi hapa tuone.


Tanzania hakuna wasomi wa kusimamia mambo kama hayo na inchi ikapata faida

Tanzania kuna wasomi wa kukwambia ujui kuongea kingereza, au umevaa tai ya njano na Leo ni ijumaa

Wasomi wetu ni wa makaratasi zaidi, ukiwapa site hakuna kitu


Ile bandari pale wenye viti wa bod ni wasomi ila ndio hao hao kila siku vikao ni Singapore
 
Kuwa wengi sio tija. Hata Serengeti utakuta nyumbu zaidi ya 5000 wanakimbizwa na Simba mmoja ambaye hajabalehe. Katika watu 63m kuna wafuatao;
1. Wenye ugonjwa wa kuchanganya L & R kwenye sentensi.
2. Mashabiki wa Yanga.
3. Wakazi wa Geita na Njombe.
4. Wasukuma
5. Wafuasi wa chama cha Mbowe.
6. Wafuasi wa Mwamposa na Kuhani Musa.
7. Mashabiki wa muziki wa Singeli
8. Wahadzabe
9. Machalii wa R
10. Wateja wa Kimboka, Sewa, Corner Bar, Kitambaa cheupe, nk.
12. Video vixens
13. Mpwayungu Village.

Ukitoa hayo makundi hapo juu unakuta wanaobaki wenye akili ni wachache sana kama laki 8 tu.
Wewe na hao waliokupa like wote ni mb waaa,, huezi kutukana kabila za watu na kujiona bora zaid...kunguni mmoja ww
 
....inawezekana huko juu wapi ambao wamesha dadavua shida tuliyonayo.

...Hakuna sayansi yeyote ile kubwa ya kufanya Design ya Bandari. Bandari zote zilizokwepo duniani zinatumia dizaini hiyo hiyo iiliyotumiwa in entiquities.

....Nauliza ni kwanini tukope, kutengeneza miundombinu? Kuna sababu gani ya kufanya hivyo? nauliza kwasababu hoja zinazoibuliwa ya kwanini "Wawekezaji" au umuhimu wa uwepo wa Private Public relationship ni Kuongeza Ufanisi; Kwamba kwa sababu wana hela basi sio rahisi kwao kujiibia, kwamba wanafanya kwa werevu na weledi mkubwa sana kuhakikisha kunapatikana faida tu!

Nauliza tena, Kwanini badala yaa kukopa na kufanyia ukarabati(mfano ukarabati wa mkongo wa umeme wa matrilioni)(tetesi inafuatia kuuzwa) tusiwaachie waje wajenge hizo miuondombinu wenyewe, au waanzishe kampuni au mashirika au viwanda wenyewe.....yaani kwanini Serikali ifanye uwekezaji(investment) kwa kitu iliyofanyia upembuzi yakinifu halafu ikaja kushindwa kutekeleza maazimio na azma ya miradi yao, shida ipo wapi?
Kwanini wasibakie kuwa ni arbiters kwanini wasibakie kuwa ni Insurers?

Isitoshe hakuna mengi mapya ambayo wawekezaji huwa wanaongeza zaidi ya Mtaji/fedha na maarifa tu, kwani wafanyakazi wanabakia ni wale wale tu! Na mara nyingi huwapunguza(naamini fika watafukuzwa wengi tu bandarini) Majengo na miundombinu ya eneo yanabakia ni yale yale? Na Madeni yanabakia pale pale tu! Yaani yale mamikopo tuliyachukua kuendeleza Bandari yanabakia pale pake! Maikopo tunayochukua kurakabisha sijui umeme yatabakia pale pale....halafu anakuja mtu kuchukua faida yake kwanza kabla hajaweza kukulipa hata ka ushuru kidogo!

....ngoja ninywe uji nilale
Mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu


Wenzetu Watanganyika washalitumbua jipu, sasa ni zamu yetu Wazanzibari kuukamua usaha mpaka tuufikie moyo wake na kuliponya moja kwa moja jeraha.
Ingefaa tuwaulize wenzetu, kama wao wameumia mno kwa kuona uhuru na rasilimali zao zimeingia hatarini kwa mkataba mmoja TU wa bandari, wanadhani wametuumiza kwa kiasi gani sisi wenzao kwa miaka 60 yote hii tangu walipoupora uhuru na mamlaka yetu YOTE na kutudumaza kiustawi kwa kutufungia njia kuu za kiuchumi.

Wanaumia kuona Mzanzibari anakuwa rais wa Tanzania hata kama ni kisheria na kikatiba, wakati wao wamejipa mamlaka ya kimabavu, kwa miaka yote hii ya kutupangia nani atuongoze Wazanzibari na kwa mipaka gani ya mamlaka!

Tuwathibitishie kwamba iwe iwavyo, sasa tumeshabaini bila chembe ya shaka, kwa yaliyotoka kwenye ndimi zao, kwamba wana chuki kubwa dhidi ya Uarabu na Uislamu na kwamba chuki hizo ndizo zilizochangia pia kutubana tusifurukute ndani ya 'muungano'; na ndio maana kina Lukuvi na Sitta hawakuulizwa chochote na yeyote waliponena waliyoyanena dhidi ya Uarabu na Uislamu, kwa sababu waliwasilisha na kuwakilisha mtazamo rasmi wa Tanganyika kuhusiana na Wazanzibari katika muungano.

Na kwa hapa tulipofika tukubaliane kwamba, kama ni kuuendeleza muungano, basi hakuna mbadala mwingine wa mahusiano yetu ya kisiasa na Watanganyika isipokuwa kufuta kwanza jina Tanzania na kurudi kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuamua ama kuwa na muungano wa mkataba au wa serikali tatu. Ghairi ya hivyo ni kila nchi kurudi kwenye asili yake ya taifa na nchi kamili
 
Kabisa mkuu Yani sisi ni kama ma ng'ombe yanayo swagwa wala hayajui yanapo pelekwa.
Pana muda nikiwaangalia hao Wanyama kama Simba au Tembo wana akili kuliko Watanzania haiwezekani tunawekewa kiwango kikubwa cha Tozo huku Mali zetu wakipewa Wajinga tuu wa Nje harafu tupo kimya na kubaki kujisifia ma degree ya uongo tuu inaumiza sana...
 
Jamani Hela tunazo,wasomi tunao .Tatizo ni nini?Na karne hii tuna uwezo kabisa wa kuangalia hizo Bandari kama Shangai,Singapore zimefanya nini hadi kuwa na ufanisi?Wachina ,wasingapore wazungu wa Roterdam na Antwerp wamevanya fanya nini?Kulikuwa na Haja ya kumleta huyu katili Sheikh wa Dubai kuwekeza kwetu?Wale ni pesa tu.

Kwanza tujiulize,watalipa kodi ama?Wenye mkataba uwekeni basi hapa tuone.
Tatizo sugu liko hapa👇👇👇


Unateua Machawa, wanaokutukuza, watoto wa vigogo na waliokusaidia kwenye kampeni.

Mambo yanaenda mrama.

Bado hujui kwanini hatupigi hatua Kama nchi??!!

Unaona suluhisho ili kupata matokeo ni kubinafsisha kila kitu, right?

Hivi, ni kweli hatujui ni kwanini hatuendi mbele??!!
 
nimecheka sana hapa nilipo aisee mpaka nimepaliwa na kahawa.

3.5mil population vs 63mil.
ratio hapo ni kama 18:1 yaani mwarabu mmoja wa dubai ni sawa na watanzania 18.

Tunaweza kusema mabogus 63mil hawana akili kabisa ya kuendesha bandari miaka yote toka uhuru mpaka wasaidiwe.
 
Robert Heriel once said

Akili ni muhimu kuliko kuwa na resources nying ambazo huna akili ya kuzitumia"
 
Narudia kila siku kusema, Watanzania ni watu wasiojua nini wanataka, kije wakati gani na kiwafanyie nini. Na bado
 
Kuwa wengi sio tija. Hata Serengeti utakuta nyumbu zaidi ya 5000 wanakimbizwa na Simba mmoja ambaye hajabalehe. Katika watu 63m kuna wafuatao;
1. Wenye ugonjwa wa kuchanganya L & R kwenye sentensi.
2. Mashabiki wa Yanga.
3. Wakazi wa Geita na Njombe.
4. Wasukuma
5. Wafuasi wa chama cha Mbowe.
6. Wafuasi wa Mwamposa na Kuhani Musa.
7. Mashabiki wa muziki wa Singeli
8. Wahadzabe
9. Machalii wa R
10. Wateja wa Kimboka, Sewa, Corner Bar, Kitambaa cheupe, nk.
12. Video vixens
13. Mpwayungu Village.

Ukitoa hayo makundi hapo juu unakuta wanaobaki wenye akili ni wachache sana kama laki 8 tu.
Mbona umewaacha wapiga nyeto
 
Back
Top Bottom