Posho wanazojilipa Wakurugenzi na Mameneja huwa ni wizi mtupu! Bila kuzifuta posho hatutoboi

Posho wanazojilipa Wakurugenzi na Mameneja huwa ni wizi mtupu! Bila kuzifuta posho hatutoboi

Wewe huna tofauti na popo anaekojoa kabinulia matako juuu akizani anaikomoa mbingu, kumbe ananuka mkojo mwenyewe
Mkojo utanuka wewe, kwa sababu huna uwezo wa kuzuia posho......utaishia kubwabwaja tu.
 
Acha tu mzee. Mi ninachofanya kuwakomoa nadownload series ata GB 20-50 kwa siku. Eti nadhani nawatia hasara.

Weekend kama hivi, naishia kuangalia tu movie za Kikorea.
Na wewe ni fisadi tu wa Mali za umma (mtandao)
 
Mkojo utanuka wewe, kwa sababu huna uwezo wa kuzuia posho......utaishia kubwabwaja tu.
Wee subiri cabinet inakuja na maamuzi magumu! Unafikili naropoka tu kama wewe! Kaa kwa kutulia utasikia tu
 
Mtoa mada sio bure utakuwa ulitimuliwa vyeti feki. Una hasira kama mbogo aliyejeruiwa
 
Tunaonanana kwenye daladala ni manyani sio. Waafrika tuna safari ndefu sana. Upumbavu umetujaa. Ndio maana unakutana na lijitu limevimba tumbo linakutisha ati wanijua mimi ni nani?. Nawe unaliuliza ukifa hauozi?. Nyani kabisa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Wee subiri cabinet inakuja na maamuzi magumu! Unafikili naropoka tu kama wewe! Kaa kwa kutulia utasikia tu
Kwamba posho ziondolewe, hizo safari na vikao utazilipia wewe, huna akili aisee....na inavyoonekana huna unalolijua.
 
Posho katika taasisi za umma kwa kiasi kikubwa ni uwizi wa kodi!
nadhani posho zifutwe hata bungeni maana wanalipwa mishahara...naamin hata waziri anayelalamika watu kujilipa posho ,, i bet na yeye alichukua posho kwa ajili ya siku ile aloenda kwenye ofisi hiyo ,,, inshort posho ni halali sema tu hatujaletewa hesabu ya wanachochukua viongozi ..tutaomba wajiuzulu wote............🙄🙄🙄🙄
 
Kwamba posho ziondolewe, hizo safari na vikao utazilipia wewe, huna akili aisee....na inavyoonekana huna unalolijua.
Magari ya safari yapo, mafuta wanawekewa, dereva analipwa, hiyo Moja.

Pili posho nyingi wanalipana kwa vikao vya pale paleofisini wala hata hawasafiri kama hujui tulia!
 
Mizizi wa haya yote chanzo chake ni bungeni kule tulikotuma wawakilishi wetu, mshahara 3.8m posho 8m kwa mwezi, akihudhuria kikao cha bunge kwa siku anakula 360k ambao ni mshahara wa mtumishi mwingne kwa mwezi, anapewa mafuta ya gari lita 1000 kwa mwezi na mkopo wa gari 90m, bima ya afya daraja la kwanza ambayo utatibiwa popote duniani na pensheni ya 250m ndani ya miaka 5.
Afu wakiwa bungeni wanajadili nguvu za kiume mamaye haya mambo yanatia hasira.
 
Daah
 
HAKUNA NIDHAMU YA FEDHA HATA KITOGO

Labda walifanyia kazi nje ya kituo cha kazi wakalipana per diem huwezi jua.
 
watu hawana kazi nyie mnalipana Mamilion ya pesa za posho kweli nchi hii inamwitaji dikteta hata zaidi ya dikteta kuitawala. Mama asipoangalia watamchezea sana na wemeanza mapema sana. Mama samia usipoziba ufa utajenga ukuta.
Ati walikuwa utawala mmoja! Inaelekea rais hakuwashirikisha wengine alichosimamia, na hao wengine kwa kuwa kuna mtu anasimamia mambo, wao walikuwa wakibembea tu. Haya digo limewaangukia, hawajui la kufanya!
 
Bongo watu hawa value kabisa taaluma za watu......si ajabu impact ya wataalamu wetu haionekani kwa hizi dharau, eti mil. 2 ndo mtu anaona mtaalamu kalipwa pesa ndefu....
Mimi nimepiga hesabu watu 125 nilipata kwa kila mtu alichezea kwenye 1. 6 sioni kama ni nyingi
 
....halafu ninaona kuna watu wawili watatu barazani humu wanaliunga mkono hili...!
Ajabu sana!
Ungekuwa ww unatengana na familia unarudi home watoto wamelala usingeona hii posho ni kubwa. swali ww ungezikataa maana ulikuwa ni desturi tangia miaka kibao ilifutwa lini ?
 
Makampuni ya kigeni huwa wanashangaa sana na kuchoshwa na hili la posho.
Wanashindwa kuelewa hata mimi nashindwa kuelewa, eti kikao cha kujadili kazi zao waandaliwe na bahasha.

Vilevile bungeni, posho za kikao huku wana mishahara, kisha Africa tunataka tuwe kama ulaya, huku fedha zote zinalipa wachumia tumbo, haziendi kwenye miradi ya maendeleo.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mkuu, umeandika jambo moja la maana sana hususan hapo uliposema "angalau kuishi maisha ya hadhi yao".

Mkuu, watu hatufanani umuhimu wetu katika taifa. Katika nchi yoyote ni lazima kuwe na kundi la "elites" watakaokuwa wanawaongoza wenzao ndio maana wengi wao wanakaa Oysterbay na Masaki. Hao jamaa (Wakurugenzi na Mameneja) ni assets sana kwa taifa.

Watu hatufanani hata siku moja.
Mkuu vipi zile interview zako ulizokuwa unatutaka tukuombee ulipata kazi?
 
Hizo wanaziita honoraria, kimsingi nchi hii wataalamu na wasomi wanalipwa mishahara kiduchu sana ukilinganisha na elimu zao. Kwa hiyo zikitokea hizo fursa za viposho ndo wanaponea hapo angalau kuishi maisha ya hadhi yao, vinginevyo wataishia kubanana uswahilini na kwenye daladala.
Kwahiyo walimu, manesi na ma secretary hawakusoma?
 
Back
Top Bottom