Post ya CIA imenifikirisha: Wamelisifia Ziwa Malawi (Ziwa Nyasa) pasipo kuitaja Tanzania!

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
2,375
Reaction score
4,784
Wakati wenye mamlaka wakiwa busy kuponya majeraha ya MO29, kwa kuyakanusha na kupindua taarifa za ukweli; wenye dunia yao huko duniani, hawachoki kuitafiti dunia na ku shape geopolitics kulingana na taarifa sahihi za kiuchunguzi.

Jana niliingia Instagram, kwenye post ya CIA, nikakuta wameweka taarifa nzuri nzuri kuhusu Ziwa Malawi (sisi tunalijua kama ziwa Nyasa), ikiwemo hii kwamba: ni ziwa lenye fish species nyingi kuliko ziwa lolote lile duniani, na ni ziwa la nne kubwa duniani lenye fresh water.

Binafsi hiyo ya fresh water nilikuwa naijua, ila hii ya kwamba Ziwa Nyasa lina species nyingi kuliko ziwa lingine lolote duniani, sikuwahi kuijua.

Kwa sababu kwa wenzetu CIA pia ina muunganiko wa kikazi na Makampuni ya kimarekani; nimejiuliza itakuwaje pindi makampuni ya kimarekani yatakapoanza uwekezaji wao pale Ziwa Malawi. Je, hii hatua haita chechemua mgogoro mpya wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi?

Kilichonishangaza zaidi ni kwamba: kwenye post hiyo ya CIA, hawakugusia kabisa kwamba Ziwa Malawi lipo pia nchi ya Tanzania kwa sehemu kubwa. Na waligongelea msumari kwa kusema, "Malawi's Lake Malawi." Je, haiwezi kuwa ni turufu kwa Malawi, kwamba mataifa makubwa yanajua tayari kwamba Ziwa Malawi lililopo upande wa Tanzania, pia ni mali ya Malawi? Na kwa sababu tayari Tanzania kupitia CCM imewabagaza wazungu; je, Tanzania itaweza kujihesabia haki ya umiliki wa ziwa Malawi lililopo upande wa Tanzania, pindi mgogoro ukirudi upya, kama dalili zinavyoonesha?

Screenshot_20251219-223455_Chrome.jpg

Wenu,
MC
 
View attachment 3518251

Wenu,
MC
Hawa wapumbavu Malawi mbona wanataka ipanda nchi kichwani ? Wajue hii nchi sio ya ccm , ni ya wananchi wakileta vyoko vyoko tutawapa kichapo cha mbwa koko nipo tiyari kwenda mstari wa mbele , kama mwananchi tetea taifa langu si la wezi wale ,pumbavu Malawi .

Kama Malawi wanalitaka ilo ziwa Nyasa wayahamishe maji yasifike Tanganyika , hawa wapuuzi naona wanataka kutuzoea ,JWTZ nipe tenda niwaoneshe hawa washenzi
 
Sisi si tunazubaa na kushangaa Tu, ngoja wenye agenda zao wazipitishe... Kuna vitu vikiwa vya kufoji inabidi uvishikilie Kila wakati na hakuna kulala, huko Middle East Israel kuna vitu anafoji na anavishikilia visimponyoke, hawalali hata kidogo, China ameshikilia vitu vya kufoji kwenye baadhi ya maeneo nao hawalali na hakuna wa kutia pua, even Rwanda anafoji mambo kule DRC na halali na wala hachoki...Naamini hata Sisi tunashikilia sehemu zetu za kufoji vizuri.
 
Unaleta taarifa hii hapa sasa hivi ili iweje?

Lengo lako ni nini?
Imepostiwa jana na CIA. Sina lengo lolote ila nimesikitishwa na CIA kuto acknowledge kwamba sehemu kubwa ya Ziwa Malawi (Ziwa Nyasa) lipo Tanzania.
 
Taarifa hizi mwanzo wake ni huko huko Malawi; na hii siyo mara ya kwanza kwa taarifa za aina hii kuletwa hapa JF. Hiyo nembo ya CIA isikupe mchecheto wowote. CIA siyo chombo cha kipuuzi kama kinavyotumiwa hapa.
 
Hawa wapumbavu Malawi mbona wanataka ipanda nchi kichwani ? Wajue hii nchi sio ya ccm , ni ya wananchi wakileta vyoko vyoko tutawapa kichapo cha mbwa koko nipo tiyari kwenda mstari wa mbele , kama mwananchi tetea taifa langu si la wezi wale ,pumbavu Malawi .

Kama Malawi wanalitaka ilo ziwa Nyasa wayahamishe maji yasifike Tanganyika , hawa wapuuzi naona wanataka kutuzoea ,JWTZ nipe tenda niwaoneshe hawa washenzi
Maslahi na Ziwa Nyasa ni kufa au kupona. Ila cha kusikitisha ni kwamba wakati sisi tumezubaa, wenzetu Malawi wanasukuma kete usiku na mchana.
 
Taarifa hizi mwanzo wake ni huko huko Malawi; na hii siyo mara ya kwanza kwa taarifa za aina hii kuletwa hapa JF. Hiyo nembo ya CIA isikupe mchecheto wowote. CIA siyo chombo cha kipuuzi kama kinavyotumiwa hapa.
Mkuu hii habari imepostiwa na CIA kwenye instagram page yao. Naelewa janja ya Malawi kwamba kwa miaka mingi wamekuwa wakijenga narrative kwamba lile ni ziwa lao. Na ninaona kwamba hiyo narrative imefaulu.

Uongo wa wamalawi uliorudiwa mara nyingi unaanza kujeuka kuwa ukweli. Siku tukizinduka itakuwa too late kuipindua hii narrative.
 
Back
Top Bottom