Killmonger
JF-Expert Member
- Jan 11, 2015
- 2,021
- 2,242
kweli mtu kama power mabula-those days alihit sana-kama kuna mwenye picha yake japo atuwekee hapa tumuone tena
nakumbuka kulikuwa na nyimbo zake kama............mabula yeeee.....nyie MNAJIBU ...yeeeee......*4-
alikuwa akifika shuleni-hiyo siku vipindi vyote vinakufa-hakuna kinachofanyika tena.....ni kuchek shoo tu
Namkumbuka,,😂😂Umenikumbusha enzi za mapawa na maprofesa (wanamazingaombwe). Power Mabula was one of my favourite, kulikuwa na power mwingine anaitwa Power Ngeta, huyu akija tulikuwa tunaimba "Power! Ngeta! Super! Kibongeeee!" Sijui yuko wapi naye huyu.
Kuna dogo tulikuwa tuko naye darasani alikuwa ni fundi wa kutengeneza mihuri (inayogongwa mkononi kama unatoka nje mara moja na utarudi), basi wale maprofesa wakija dogo naye anatengeza na kutugongea mikononi watu wanaotaka kuingia bila kulipia. Baadae ukitoka unampa shilingi 5 au unamnunulia vipande vya mihogo. Tulikuwa tunainjoi sana maisha yale.
Alifariki last yearNamkumbuka sana huyu jamaa kwani alivuma sana miaka ile.
aliokoka miaka ya 95/96 na alikuwa anapita kuhubiri na kuelezea namna alivyokuwa anatumia nguvu za giza kufanikisha mambo yake.
hadi sasa bado yupo kwenye wokovu.
Jina la Bwana lihimidiwe.
Huyu sio mchawi Juma wa Morogoro kweli?Duh! umenikumbusha mbali kweli enzi za shule ya msingi.
Pia kulikuwa na profesa mmoja wa kihindi anakupa ndizi waila halafu anapasua tumbo live na kutoa ndizi iliyoliwa sijui walikuwa wanatudanganyaje? mazingaombwe ya zawadi za biskuts, chupi na vitu kibao watoto mnapewa duh kazi kweli
Anaitwa power jabir computer kababayeekuna jamaa anaitwa kababayee nae alikuwa noma sana.
hivi mzee morris nyunyusa bado yupo?alikuwa na issue ya kufuatilia copy right ya ule wimbo wake wa ngoma za taarifa ya habari sijui iliishia wapi. inasikitisha,inanifanya niwaze 30, 40 yrs to come nitakuwa wapi!
Ushakata 8 years, umeshajiona uko wapi?
Sent from my iPhone using JamiiForums
Tuseme hupajui utakapokuwepo? Au unajitoa ufahamu tu?hivi mzee morris nyunyusa bado yupo?alikuwa na issue ya kufuatilia copy right ya ule wimbo wake wa ngoma za taarifa ya habari sijui iliishia wapi. inasikitisha,inanifanya niwaze 30, 40 yrs to come nitakuwa wapi!
Tuseme hupajui utakapokuwepo? Au unajitoa ufahamu tu?
Niko kileleni baba. God is just too good!
Asante kwa kujali na kunifuatilia.
Wewe je, umejiona uko wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mie tofauti mkuu, ni kama vile niliahidiwa kunyolewa kiduku lakini kila nikishika kichwa sigusi hata kipisi cha unywele,
Sent from my iPhone using JamiiForums
Una uhakika unachogusa ni kichwa?
Usikate tamaa mkuu, anza kwa kuhesabu baraka zako (una afya njema, familia na marafiki wanaokujali na kukupenda, una akili timamu, uko huru, una mahali pa kulala). Halafu pigana kuibadili kesho yako. Yaani pambana ya ela yote mazee!
Sent using Jamii Forums mobile app
Umenikumbusha Power Bernado!Sijui kama bado yupo hai yule Mzee, nimekumbuka enzi za shule na entertainment tofauti za wakati huo zilizokua zikiletwa shule
Nini ilikua Siri ya nguvu za mzee yule? Sijamsikia kitambo.