Power Mabula: Mtu aliyetikisa enzi zake!

Power Mabula: Mtu aliyetikisa enzi zake!

kweli mtu kama power mabula-those days alihit sana-kama kuna mwenye picha yake japo atuwekee hapa tumuone tena
nakumbuka kulikuwa na nyimbo zake kama............mabula yeeee.....nyie MNAJIBU ...yeeeee......*4-
alikuwa akifika shuleni-hiyo siku vipindi vyote vinakufa-hakuna kinachofanyika tena.....ni kuchek shoo tu

Hahhaha Sahihi kabisa. Yani mwalimu wa zamu kabla hajatangaza uwepo wa huyu bwana taarifa zilikua zishatufikia siku nyingi .
 
IMG-20190323-WA0014.jpg
 

Attachments

  • IMG-20190323-WA0014.jpg
    IMG-20190323-WA0014.jpg
    59.4 KB · Views: 47
Na
Umenikumbusha enzi za mapawa na maprofesa (wanamazingaombwe). Power Mabula was one of my favourite, kulikuwa na power mwingine anaitwa Power Ngeta, huyu akija tulikuwa tunaimba "Power! Ngeta! Super! Kibongeeee!" Sijui yuko wapi naye huyu.

Kuna dogo tulikuwa tuko naye darasani alikuwa ni fundi wa kutengeneza mihuri (inayogongwa mkononi kama unatoka nje mara moja na utarudi), basi wale maprofesa wakija dogo naye anatengeza na kutugongea mikononi watu wanaotaka kuingia bila kulipia. Baadae ukitoka unampa shilingi 5 au unamnunulia vipande vya mihogo. Tulikuwa tunainjoi sana maisha yale.
Namkumbuka,,😂😂
 
Namkumbuka sana huyu jamaa kwani alivuma sana miaka ile.
aliokoka miaka ya 95/96 na alikuwa anapita kuhubiri na kuelezea namna alivyokuwa anatumia nguvu za giza kufanikisha mambo yake.
hadi sasa bado yupo kwenye wokovu.
Jina la Bwana lihimidiwe.
Alifariki last year



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah, nimesikitika sana hakuna pic ha hao mapawa hada ya pawa mabula nashukuru kwa iliyopo japo surahaionekani. Kina wanmieleka walikua wamevimba balaa, pic ha zao zilikua zinachapishwa kwenye magazeti sambamba na kumbi za sinema nakumbuka kwenye gazeti la Uhuru, Mzalendo na Mfanyakazi
 
Duh! umenikumbusha mbali kweli enzi za shule ya msingi.
Pia kulikuwa na profesa mmoja wa kihindi anakupa ndizi waila halafu anapasua tumbo live na kutoa ndizi iliyoliwa sijui walikuwa wanatudanganyaje? mazingaombwe ya zawadi za biskuts, chupi na vitu kibao watoto mnapewa duh kazi kweli
Huyu sio mchawi Juma wa Morogoro kweli?
 
hivi mzee morris nyunyusa bado yupo?alikuwa na issue ya kufuatilia copy right ya ule wimbo wake wa ngoma za taarifa ya habari sijui iliishia wapi. inasikitisha,inanifanya niwaze 30, 40 yrs to come nitakuwa wapi!

Ushakata 8 years, umeshajiona uko wapi?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
hivi mzee morris nyunyusa bado yupo?alikuwa na issue ya kufuatilia copy right ya ule wimbo wake wa ngoma za taarifa ya habari sijui iliishia wapi. inasikitisha,inanifanya niwaze 30, 40 yrs to come nitakuwa wapi!
Tuseme hupajui utakapokuwepo? Au unajitoa ufahamu tu?
 
Una uhakika unachogusa ni kichwa?
Usikate tamaa mkuu, anza kwa kuhesabu baraka zako (una afya njema, familia na marafiki wanaokujali na kukupenda, una akili timamu, uko huru, una mahali pa kulala). Halafu pigana kuibadili kesho yako. Yaani pambana ya ela yote mazee!
Mie tofauti mkuu, ni kama vile niliahidiwa kunyolewa kiduku lakini kila nikishika kichwa sigusi hata kipisi cha unywele,


Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una uhakika unachogusa ni kichwa?
Usikate tamaa mkuu, anza kwa kuhesabu baraka zako (una afya njema, familia na marafiki wanaokujali na kukupenda, una akili timamu, uko huru, una mahali pa kulala). Halafu pigana kuibadili kesho yako. Yaani pambana ya ela yote mazee!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ngoja nikomae maana wa mwisho ndio mshindi.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sijui kama bado yupo hai yule Mzee, nimekumbuka enzi za shule na entertainment tofauti za wakati huo zilizokua zikiletwa shule
Nini ilikua Siri ya nguvu za mzee yule? Sijamsikia kitambo.
 
Back
Top Bottom