Asante kwa kunifungua, nimeishia pale pale aliposema Mkapa aliuza Tanesco, akiwa amesahau kuwa Tanesco haijawahi kuuzwa
Seems like you're misinformed!
Mkapa aliiweka TANESCO under the management contract ya NetGroup ya SA. Na kwa tabia za Mkapa, hiyo ilikuwa ni mwanzo tu kwa sababu hata NMB alianza kuiweka chini ya management contract ambapo CEO alikuwa John Giles!
Bank ilivyo-break even na kuanza kutengeneza faida, Mkapa akaiweka NMB sokoni kwa madai kwamba benki inaitia hasara serikali kwa sababu bado inategemea ruzuku ya serikali!
Kwavile wenzetu hawapendi ubabaishaji, Mr. Giles akatamka hadharani kwamba si kweli eti benki inatengeneza hasara! Na hapo hapo akabwaga manyanga, akarudi zake US!
na ni Mkapa aliyewahi kufuta deni la Taifa
Alifuta deni la taifa?!
Tatizo la wafuasi wa Magu you're very less informed na ndo maana mlikuwa mnadanganywa kirahisi!!
Mkapa hakufuta deni, bali alifanikisha matakwa ya IMF, WB na Paris Club ambao back 1995 hata kabla Mkapa hajawa rais, taasisi hizo zikakubaliana zifute madeni kwa nchi maskini kabisa duniani. Nchi ambazo ziliingizwa kwenye huo mpango ni 38 including Tanzania!
Google mwenyewe Heavily Indebted Poorest Countries ili ujiongezee maarifa!!!
kisha MSOGA theory ikaturudisha MWINYI era ambayo ilibidi ifute tena ila kuanza upya! Hajui kuwa kuna msemo ulikuwa maarufu kuwa UKAPA UMEPANDA CHATI na matokeo yake 10k shilling ilikuwa na thamani mpaka ilipofikia kwenye awamu ya LAKI SI PESA, kisha tukarudi kwenye zama za 1000 kuitwa elfu moja badala ya buku!
Asante.
Hiyo shilingi ilipanda thamani against nini?!
Sasa kama shilingi ilipanda thamani, how come tena watu walalamike "Ukapa umepanda chati"?! Nini maana ya hiyo kauli kama sio watu walikuwa wanalalamikia ugumu wa maisha kutokana na kutokuwepo kwa pesa kwenye mzunguko?
This's what happened...
Mkapa alifunga ajira... fanya surveys hata hapa JF watu wa-comment walioajiriwa enzi za Mkapa kama majority hujakuta ni polisi peke yao ambao alikuwa anawaajiri ili wapambane na CUF pamoja na NCCR!!
Mkapa aliuza mashirika ya umma na hivyo wafanyakazi wengi kukosa ajira na kipato!!!
Mimi mwenyewe niliajiriwa na taasisi ya kifedha mwishoni mwa utawala wa Mkapa, na hapo ndipo nilipokuja kufahamu mishahara wanayolipwa watumishi wa umma!!!
Yaani mishahara waliyokuwa wanalipwa, only God knows walikuwa wana-survive vipi!
Sasa mtu amefunga ajira! Wale waliokuwa kwenye ajira wanapoteza ajira baada ya mashirika kuuzwa! Mishahara yenyewe ndo hivyo tena!! Nini kilifuata?! Pesa mtaani ikaadimika, na automatically mfumuko wa bei ukashuka!! Lakini ushukaji huu ulichangiwa na kutokuwepo kwa pesa kwenye mzunguko, na ndo maana watu walikuwa wanalia UKAPA!