#COVID19 President Samia hires Tony Blair to help in the fight against COVID-19, and rebuild the country's reputation

#COVID19 President Samia hires Tony Blair to help in the fight against COVID-19, and rebuild the country's reputation

Mkuu

Huyo jamaa tangu nimjue mlengo wake nimetokea
kumwona mutu wa hovyo sana......

Huyo ni msoga pure, linakujaga na hoja zake za
kutetea upuuzi, Upuuzi yaani upuuzi.....

Quote zake huwa hata sihangaiki nazo, Hili Taifa ni
Taifa la Watanzania na siyo Taifa la familia zao na
marafiki zao mabeberu.

Atakupotezea muda kwa maandishi yake marefu
na quotation za kwenye Encarta.......

Shukrani!
Asante kwa kunifungua, nimeishia pale pale aliposema Mkapa aliuza Tanesco, akiwa amesahau kuwa Tanesco haijawahi kuuzwa na ni Mkapa aliyewahi kufuta deni la Taifa kisha MSOGA theory ikaturudisha MWINYI era ambayo ilibidi ifute tena ila kuanza upya! Hajui kuwa kuna msemo ulikuwa maarufu kuwa UKAPA UMEPANDA CHATI na matokeo yake 10k shilling ilikuwa na thamani mpaka ilipofikia kwenye awamu ya LAKI SI PESA, kisha tukarudi kwenye zama za 1000 kuitwa elfu moja badala ya buku!

Asante.
 
Nadhani taasisi za vyama ndio taasisi zenye vijana wa ovyo kupindukia yaani wao vyama kwanza ndio nchi baadae ukitazama matendo na mawazo yao unajiuliza hawa viumbe hizi tabia wamerithi Tanzania ya wapi. Sabaya, mdude ni mifano hai yaani vyama ndio majiko ya kuzalisha vijana wahuni.
 
Chige hawezi kukuelewa yeye akili zake ni kama za mabavicha wengine wanaohisi maendeleo yao yataletwa na mzungu
Huyo Magu aliacha lini kutegemea Wazungu? Unajua nyie ni watu wa ajabu sana!! Yaani kutokwenda Uzunguni kwenu ndo tafsiri ya kutotegemea wazungu?!

Nimewauliza ni lini aliacha au kukataa misaada toka kwa wazungu... mbona hamjibu?
 
Rais SSH hayupo katika hilo kundi, elimu yake ya kuunga unga. Ana inferiority complex.
Yuko kwenye ndoa ya mitala, vipi maamuzi yake kwa nchi? Kwa maamuzi yake, angekuwa kwenye ndoa hiyo?

Julius alisema, hatutaki raisi ambaye atashauriwa na mkewe usiku kisha asubuhi tunapewa tamko kuwa ni sheria.
 
Unaona sasa! Kwani aliyesema Blair kaletwa ku-rebuild reputation ni mimi?

Una-rebuild vipi kitu ambacho kilikuwa intact?

Na kama hakikuwa intact nani kasababisha kutokuwa intact?

Na kama reoutation iliondoka, lazima irejeshwe!!

Btw, huo uovu ninaotetea ni upi?!

Narudia, mwambieni mleta mada aweke ripoti kamili! Tony Blair Institute hawawezi kuchukua pesa kwa Tanzania!! Narudia, ikiwa taasisi iliwekwa kitimoto kwa kuchukua pesa kwa Saudi Arabia nchi ambayo haina shida, kwa akili yako unatarajia watakuwa stupid wachukue pesa kwa nchi maskini?

And FYI, Tanzania ni moja tu kati ya nchi zaidi ya 10 za Afrika ambako TBI wanafanya kazi! Najia hii habari kwanu chungu kwa sababu kwa mara nyingine inathibitisha Magu aliivuruga nchi!!

Kuhusu Samia, YEEEEEES, endelea KUUMIA lakini akifanya jambo zuri tutamuunga mkono, especially anapofanya jambo la kurekebisha mafyorofyongo ya Magu!!
Hahahhaha... Maneno mengi!

Haya maumivu yako utaishi nayo kwa muda mrefu sana!
 
Tumekuwa taifa la vijana wajinga waliojaa propaganda bila kuwa na uwezo wa kufikiri kwa kina.Ukitazama nyuzi nyingi tunajadili mtu badala ya issues.Vyuo siku hz vinazalisha hopeless imbeciles wengi .
Mkuu ndio maana mimi juzi juzi nikasema kwa sasa mtu ukiwa na nafasi bora uibe tu ukale maisha!

Habari ya umeleta impact gani katika nafasi uliyonayo, hiyo haikuhusu.

Kujaribu kuwatete hawa wapumbavu wa tz ni kujichosha bure.
 
Huyo Magu aliacha lini kutegemea Wazungu? Unajua nyie ni watu wa ajabu sana!! Yaani kutokwenda Uzunguni kwenu ndo tafsiri ya kutotegemea wazungu?!

Nimewauliza ni lini aliacha au kukataa misaada toka kwa wazungu... mbona hamjibu?
Magu hakukataa misaada ila alikuwa very clear kwamba misaada yenye masharti ya ajabu kwa nchi na utu wa mtz ni bora isije.

Hatua kama hiyo kwa watu kama nyie mliona ni anahatarisha uchumi wa nchi.
 
Asante kwa kunifungua, nimeishia pale pale aliposema Mkapa aliuza Tanesco, akiwa amesahau kuwa Tanesco haijawahi kuuzwa
Seems like you're misinformed!

Mkapa aliiweka TANESCO under the management contract ya NetGroup ya SA. Na kwa tabia za Mkapa, hiyo ilikuwa ni mwanzo tu kwa sababu hata NMB alianza kuiweka chini ya management contract ambapo CEO alikuwa John Giles!

Bank ilivyo-break even na kuanza kutengeneza faida, Mkapa akaiweka NMB sokoni kwa madai kwamba benki inaitia hasara serikali kwa sababu bado inategemea ruzuku ya serikali!

Kwavile wenzetu hawapendi ubabaishaji, Mr. Giles akatamka hadharani kwamba si kweli eti benki inatengeneza hasara! Na hapo hapo akabwaga manyanga, akarudi zake US!
na ni Mkapa aliyewahi kufuta deni la Taifa
Alifuta deni la taifa?!

Tatizo la wafuasi wa Magu you're very less informed na ndo maana mlikuwa mnadanganywa kirahisi!!

Mkapa hakufuta deni, bali alifanikisha matakwa ya IMF, WB na Paris Club ambao back 1995 hata kabla Mkapa hajawa rais, taasisi hizo zikakubaliana zifute madeni kwa nchi maskini kabisa duniani. Nchi ambazo ziliingizwa kwenye huo mpango ni 38 including Tanzania!

Google mwenyewe Heavily Indebted Poorest Countries ili ujiongezee maarifa!!!
kisha MSOGA theory ikaturudisha MWINYI era ambayo ilibidi ifute tena ila kuanza upya! Hajui kuwa kuna msemo ulikuwa maarufu kuwa UKAPA UMEPANDA CHATI na matokeo yake 10k shilling ilikuwa na thamani mpaka ilipofikia kwenye awamu ya LAKI SI PESA, kisha tukarudi kwenye zama za 1000 kuitwa elfu moja badala ya buku!

Asante.
Hiyo shilingi ilipanda thamani against nini?!

Sasa kama shilingi ilipanda thamani, how come tena watu walalamike "Ukapa umepanda chati"?! Nini maana ya hiyo kauli kama sio watu walikuwa wanalalamikia ugumu wa maisha kutokana na kutokuwepo kwa pesa kwenye mzunguko?

This's what happened...

Mkapa alifunga ajira... fanya surveys hata hapa JF watu wa-comment walioajiriwa enzi za Mkapa kama majority hujakuta ni polisi peke yao ambao alikuwa anawaajiri ili wapambane na CUF pamoja na NCCR!!

Mkapa aliuza mashirika ya umma na hivyo wafanyakazi wengi kukosa ajira na kipato!!!

Mimi mwenyewe niliajiriwa na taasisi ya kifedha mwishoni mwa utawala wa Mkapa, na hapo ndipo nilipokuja kufahamu mishahara wanayolipwa watumishi wa umma!!!

Yaani mishahara waliyokuwa wanalipwa, only God knows walikuwa wana-survive vipi!

Sasa mtu amefunga ajira! Wale waliokuwa kwenye ajira wanapoteza ajira baada ya mashirika kuuzwa! Mishahara yenyewe ndo hivyo tena!! Nini kilifuata?! Pesa mtaani ikaadimika, na automatically mfumuko wa bei ukashuka!! Lakini ushukaji huu ulichangiwa na kutokuwepo kwa pesa kwenye mzunguko, na ndo maana watu walikuwa wanalia UKAPA!
 
Magu hakukataa misaada ila alikuwa very clear kwamba misaada yenye masharti ya ajabu kwa nchi na utu wa mtz ni bora isije.

Hatua kama hiyo kwa watu kama nyie mliona ni anahatarisha uchumi wa nchi.
Masharti ya ajabu ajabu kama yapi?! Ya kudumisha demokrasia na utawala bora, au?!
 
Same old story...

Nimeuliza hapa mara kadhaa lakini sijajibiwa, labda unisaidie wewe!!

Sote tumeona alivyo-deal na Accacia, tena cha ajabu ali-deal na makinikia ambayo yana-account only 30% ya mapato ya Acacia. Je, unataka kusema ni Acacia peke yake ndio waliokuwa wanaiibia Tanzania?

Maajabu haya...

Umekopa pesa kwa sababu nyingine, halafu unataka usamehewe madeni kwa sababu nyingine?

Na kama kweli aliamini madeni yanazidi kudidimiza, kwanini aliendelea kukopa huku akiaminisha watu kwamba ni pesa za ndani?! Magu alikopa Standard Chartered Bank na Credit Suisse!

Hivi mnaelewa maana ya kukopa kwenye private financial institutions?!

Magu alijaa janja janja tu! Kama vile kujifanya kuwaponda mabeberu huku akiaminisha wafuasi wake kwamba hatuwahitaji, lakini anapita mlango wa nyuma anapokea misaada ya hao hao mabeberu, huku akienda kukopa kwa hao hao mabeberu!!

Kama mtu anataka kukupa msaada una haki ya kuomba msaada utakao kufaa na sio kukupa maumivu zaidi…

Kukopa sio dhambi ni matumizi ya huo mkopo ndio shida…JPM alikuwa anatekeleza miradi…miradi mingine pesa yetu mingine mikopo alikuwa anasema kwa uwazi kabisa…unasema vyote vilikuwa planned na waliopita walishindwa nini kutekeleza?! Kupanga kila mtu anapanga issue kutekeleza..

Mzee Mwinyi said it all …”kijana wetu vitu vilivyotushinda miaka 30 kavitekeleza kwa miaka mitatu” …unaongea nini hapa mkuu..
 
Former British Prime Minister Tony Blair has made two official visits to Tanzania since Samia Suluhu Hassan assumed the presidency in March this year after the sudden death of her predecessor, John Magufuli.

Government officials say that the Tony Blair Institute for Global Change has been hired by President Samia to handle two of her administration’s key projects: the fight against Covid-19 and rebuilding Tanzania’s international reputation.

In July, Blair paid his first courtesy call to Tanzania where he and President Samia discussed how to combat the Covid-19 pandemic.

Blair said his institute is responsible for facilitating the testing and distribution of vaccines, and may help Tanzania to access top vaccine producers.

Credits: The Africa Report
Hatukubali!! Kwanza tuambiwe the terms under this deal!! Toni bleya ni satanist!! We have turned back from depending on God in this fight against covid 19 to depending on a satanist!! Hapo tunategemea nini?? Mama with due respect, on this aspect you are leading us astray na dhamiri yako inajua hivyo ndio maana hakuna taarifa rasmi iliyotolewa baada ya ujio wa huyu mwabudu shetani!!
Ujue watanzania tunamwomba sana Mungu na mama uamuzi huu utakupa taabu sana!! Utaitesa sana dhamiri yako!! Hutakuwa na amani maisha yako yote na hutafurahia nafasi yako ya urais na utatamani afadhali usingeipata!! Mungu atakupinga!! Rais wangu nakupenda, nakuheshimu lakini katika hili hapana !!! Litaiumiza Tanzania na wewe binafsi utaumia sana!! Kindly please break the contract if any!!
 
Masharti ya ajabu ajabu kama yapi?! Ya kudumisha demokrasia na utawala bora, au?!
Hayo hajawahi kuwa masharti ya ajabu ajabu.

Bali mashrti ya ajabu ajabu ni pamoja na kutaka nchi iruhusu mashoga.
 
Kama mtu anataka kukupa msaada una haki ya kuomba msaada utakao kufaa na sio kukupa maumivu zaidi…

Kukopa sio dhambi ni matumizi ya huo mkopo ndio shida…JPM alikuwa anatekeleza miradi…miradi mingine pesa yetu mingine mikopo alikuwa anasema kwa uwazi kabisa…unasema vyote vilikuwa planned na waliopita walishindwa nini kutekeleza?! Kupanga kila mtu anapanga issue kutekeleza..

Mzee Mwinyi said it all …”kijana wetu vitu vilivyotushinda miaka 30 kavitekeleza kwa miaka mitatu” …unaongea nini hapa mkuu..
Points
 
Kama mtu anataka kukupa msaada una haki ya kuomba msaada utakao kufaa na sio kukupa maumivu zaidi…
Mkopo kutoka private financial institutions unakosa vipi maumivu?!
Kukopa sio dhambi ni matumizi ya huo mkopo ndio shida…JPM alikuwa anatekeleza miradi…miradi mingine pesa yetu mingine mikopo alikuwa anasema kwa uwazi kabisa…unasema vyote vilikuwa planned na waliopita walishindwa nini kutekeleza?! Kupanga kila mtu anapanga issue kutekeleza..
Hakuna ambacho walishindwa!!

Tuchukulie SGR kwa mfano... kila kitu kilikamilika mwishoni mwa utawala wa Mzee wa Soga! Feasibility study ilishakamilika, na Mkandarasi alishapatikana!!

Sasa hapo utaita "sasa walishindwa nini kutekeleza"?! Tena niliwahi kumsikia Mzee wa Msoga siku za karibuni akisema "kwavile muda wangu ulikuwa unaelekea kwisha, nikawaagiza wasianze huo mradi kwa sababu unakuja utawala mwingine"

Mfano mwingine, barabara za Dar es salaam! Hadi pesa ilishatolewa tangu May 2015 lakini zikaja kujengwa na Magu!! Hivi hapo utasema "walishindwa nini"?

Mifano ipo mingi lakini itakuwa tunajaza server bila sababu!!
Mzee Mwinyi said it all …”kijana wetu vitu vilivyotushinda miaka 30 kavitekeleza kwa miaka mitatu” …unaongea nini hapa mkuu..
Kama kipi? Kuhamia Dodoma, au?! Nasikia Phillip Mpango kautangazia umma kwamba kumbe hata Contractor wa Mradi wa Bwawa la Nyerere hana sifa, matokeo yake kazi karibu zote ana-subcontract!!

Hata hivyo niweke wazi jambo moja! Sina matatizo na Bwawa la Nyerere lakini JPM angekuwa amefanya uamuzi wa busara zaidi kama angeelekeza nguvu kwenye gas kuliko Bwawa la Nyerere kwa sababu economic impact ya gas ni kubwa mara dufu ya Bwawa la Nyerere!
 
Hayo hajawahi kuwa masharti ya ajabu ajabu.

Bali mashrti ya ajabu ajabu ni pamoja na kutaka nchi iruhusu mashoga.
Sasa lini nchi iliwahi kupewa mkopo/msaada kwa masharti ya kuruhusu ushoga?
 
Kashachemsha mama, dunia imeishamjua kuwa hana msimamo,anaendeshwa na washikaji wake wa zamani
Mama kama habari hii ni ya kweli basi utakuwa umeshatuuza sisi na watoto wetu na wajukuu wetu na vitukuu wetu!! Vizazi yote watafanyakazi ili kulipa mikopo hii ya corona hewa miaka nenda rudi!! Kama ni kweli umetuuza mama! Umetuuza mama! Na wewe Mungu atakushughulikia!! With due respect!! Tutakuwa watumwa wa mabeberu miaka nenda rudi! Leo chanjo moja kesho booster endelevu!!
 
... yule mtu aliiharibu sana nchi! Anatafutwa expert wa kurekebisha aliyofanya "shujaa" ushujaa wa wapi huo? Nakubaliana na Dr. Anthony Diallo kwa 100%.
Watanzania tumekuwa wasahaulifu sana ama hatusomi makala mbalimbali za masuala ya utawala na dunia inavyoenda hivi hamjui Tony Blair kazi yake ni kuzikuwadia kampuni za kitapeli kupata kandarasi nchi za kiafrika hasa hivi vinchi maskini?hiyo kampuni yake ya ushauri imeziingiza matatani nchi kibao zilizoshauriwa na huyu beberu, halafu huyu huyu ndio mwizi mkubwa na yumo kwenye orodha ya walioficha pesa kwenye ripoti ya Pandora Papers, Blair ananuka rushwa kokote anakoenda, nilipomuona kaanza kuja Tanzania nikajua tu hapa kuna jambo na Blair ni rafiki wa bwana yule Vasco Da Gama wa enzi zile nina wasiwasi hizi ndio karata zake Vasco Da Gama wetu. Na mwisho hatuulizi hyu beberu atalipwa pound ngapi kwa maana tusidanganyike kuwa anafanya hiyo kazi bure, huyu beberu huwa anatoza kiasi kikubwa sana cha pesa na sijui kama serikali imepitisha fungu la kumlipa huyu mheshimiwa huko bungeni kwa maana pesa anayolipwa si ya mchezo na halipwi kwa pesa yetu ya madafu. Tunategemea beberu ndie aw mshauri wetu wakati hajui lolote kuhusu nchi yetu!
 
Mkopo kutoka private financial institutions unakosa vipi maumivu?!

Hakuna ambacho walishindwa!!

Tuchukulie SGR kwa mfano... kila kitu kilikamilika mwishoni mwa utawala wa Mzee wa Soga! Feasibility study ilishakamilika, na Mkandarasi alishapatikana!!

Sasa hapo utaita "sasa walishindwa nini kutekeleza"?! Tena niliwahi kumsikia Mzee wa Msoga siku za karibuni akisema "kwavile muda wangu ulikuwa unaelekea kwisha, nikawaagiza wasianze huo mradi kwa sababu unakuja utawala mwingine"

Mfano mwingine, barabara za Dar es salaam! Hadi pesa ilishatolewa tangu May 2015 lakini zikaja kujengwa na Magu!! Hivi hapo utasema "walishindwa nini"?

Mifano ipo mingi lakini itakuwa tunajaza server bila sababu!!

Kama kipi? Kuhamia Dodoma, au?! Nasikia Phillip Mpango kautangazia umma kwamba kumbe hata Contractor wa Mradi wa Bwawa la Nyerere hana sifa, matokeo yake kazi karibu zote ana-subcontract!!

Hata hivyo niweke wazi jambo moja! Sina matatizo na Bwawa la Nyerere lakini JPM angekuwa amefanya uamuzi wa busara zaidi kama angeelekeza nguvu kwenye gas kuliko Bwawa la Nyerere kwa sababu economic impact ya gas ni kubwa mara dufu ya Bwawa la Nyerere!
Gesi mkw*re alishaiuza siku nyingi hujui? Sheria ya kifisadi ya gesi ilipitishwa kwa hati ha dharula! Ukiuliza ni dharula ipi hakuna awezaye kukujibu! Mkw*re pia alijifunza kwa Mk*per!! Mkaper alisninikiza bunge lipitishe sheria ya kifisadi ya madini kwa hati ya dharula!! Tulipigwz sana!! Ashukuriwe Mungu sheria hiyo ilitenguliwa na JPM ,kwenye awamu ya tano na kupelekea baadhi ya mikataba ya madini kurejewa upya kama ile ya dhahabu!!
Wote hawa wawili mkw*re na mk*per walikuwa na dharula ya kuwahi kupiga kabla awamu zao hazijaisha!! Mwulize leo mk*per kama anafaidika na huo upigaji!! Na mwenzake anaelekea huko huko!! Sana sana wanaacha laana kwa vizazi vyao!!
 
Gesi mkw*re alishaiuza siku nyingi hujui?
SIO KWELI
Sheria ya kifisadi ya gesi ilipitishwa kwa hati ha dharula! Ukiuliza ni dharula ipi hakuna awezaye kukujibu! Mkw*re pia alijifunza kwa Mk*per!! Mkaper alisninikiza bunge lipitishe sheria ya kifisadi ya madini kwa hati ya dharula!! Tulipigwz sana!! Ashukuriwe Mungu sheria hiyo ilitenguliwa na JPM ,kwenye awamu ya tano na kupelekea baadhi ya mikataba ya madini kurejewa upya kama ile ya dhahabu!!
Wote hawa wawili mkw*re na mk*per walikuwa na dharula ya kuwahi kupiga kabla awamu zao hazijaisha!! Mwulize leo mk*per kama anafaidika na huo upigaji!! Na mwenzake anaelekea huko huko!! Sana sana wanaacha laana kwa vizazi vyao!!
I'm certain hujaisoma hiyo sheria lakini kwavile Wapinzani walisusia, basi umechukua neno lao bila kujua it's just politics!!
Hata nikikuuliza ni sheria ipi hiyo iliyotenguliwa na JPM sidhani kama utaitaja!!

Let's try: Sheria ya Mafuta na Gas ya 2015 inasemaje kuhusu mgawanyo wa raslimali ya gas?

FYI, nimesoma mwenyewe sheria ZOTE 3, na sio kwa kuhadithiwa kama mnavyofanya nyie wengine!!
 
Huyo Magu aliacha lini kutegemea Wazungu? Unajua nyie ni watu wa ajabu sana!! Yaani kutokwenda Uzunguni kwenu ndo tafsiri ya kutotegemea wazungu?!

Nimewauliza ni lini aliacha au kukataa misaada toka kwa wazungu... mbona hamjibu?
Hakuwahi kjkmba msaada. Mikopo aliyoomba nj ya maendeleo!! Siuo hii ya kukopa matrilioni kwa ajili ya kupambana na corona hewa! Wanalazimika kupika data za corona ili kupata mkopo!!! Hi i corona ingekuwepo kweli kuna mtu angebembelezwa kuvaa barakoa?? Barakoa zingegombaniwa! Zingepanda bei!! Watu wangetulia majumbani!! Lakini Mungu alishatuponya na corona toka 2020, halafu leo utukufu aje apewe satanist!!! Kufuru iliyoje!! Wanaonusika na maamuzi haya wajue kabisa watapambana na Mungu!!
 
Back
Top Bottom