Uwanja wa nyumbani kwako, haunikoseshi preta
Hebu ishia zako, usilete za kuleta
Kauze mitumba yako, huko sokoni haji Preta
Na hayo mashairi yako, wala hayanipi presha
Preta ni wangu mimi, subiri uone mwisho wa uzi
Atanikubali mimi, hadanganywi na wanuka ushuzi
Mengine hapa sisemi, nasubiri uniuzi
Takupa tungo za semi, mpaka ukose usingizi
Preta nampenda sana, japo sjawai kumwona
Kimpata ntamtunza sana, mtoto apate kunona
Arusha mtalia sana, si tutabaki kuwang'ong'a
Wacha nsiseme sana, dushe lisijesimama
Pretaa oooooh pretaaaaa usimskize Soooooth
Pretaaa oooh pretaaa nipe mavituuuuuuuth
Wauzaji wa mitumba, hata si watu dhalili
Ashakum! we mshamba, umeonyesha dalili
Mitumba ni adimu pamba, kuzivaa ni kama zali
Kwenye mitumba hakuna saresare, kila mtu hutoka tofauti
Preta hahitaji matunzo, anahitahi nzito huba
Kwao wanao uwezo, anapata mahitaji si haba
Hongo huleta mzozo, pesa pelekea kahaba
Hapa ni raha na utamu tu, pesa ni majaliwa-leo zipo kesho hazipo
Hamuchelewi kudai, mlivyotoa kwa hiari
Wewe mfano hai, umemdai Asha tayari
Umeruka juu kama Tai, anzisha kwangu hatari
Mbona wewe hujarudisha ulivyopewa, mpaka ukawa unahonga?
Wakujua kwa mromboo, nyama choma ya mbuzi
Nyama mpaka kokolikoo, hapana fanya ajizi
Waisikia tu moshonoo, hujafanya uchunguzi
Huko ndo kuna raha zetu sie wa 'Sokoni'
Preta kwako hoi hoi, moyo wangu watweta
Achana na huyo goigoi, maombi rasmi naleta
Kwa mwingine sitoi, kwako sana nitapepeta
Shughuli naiweza, kila siku hata ukitaka