Preta njoo nikutongoze, wengine tulieni mjifunze

Preta njoo nikutongoze, wengine tulieni mjifunze

Dah......aisee......kama nahisi kukubali vile.......

Preta nikubali usione aibu,
Kuitwa vampire isiwe sababu,
Humu JF kuna mijitu ya ajabu,
Lakini wewe mpenzi ni kama dhahabu

Mimi ni yatima nionee huruma,
Pia ni bikra skuwa na demu uko nyuma,
Kila nkitongoza ilikuwa inabuma,
Lakini kwako mpenzi ntakuwa imara kama chuma..

We ni mzuri, jina lako ni preta,
Nikikupata hapa JF ntapeta
Najua huwezi kunipwerepweta,
Japo snitch wanaponda, na uzushi kuleta

Preta ooooh pretaaaaaa nikubalieeeee

Preta oooh pretaaa usinizingueeee
 
Habari wakuu,

Mimi ni mgeni humu naomba knena. . Sorry nimesahau U hapo kwenye knena. . . Ilitakiwa kuwa kunena, yaani kuongea....

Naomba nitumie fursa hii adhwiim na jukwaa lenu kumtongoza binti mrembo aitwaye Preta ...

Maana pm kwake zipo nyingi kiasi hatapay attention kwangu...Naomba wengine muwe watazamaji ispokuwa kwa anayejijua mtaalam wa kutongoza namruhusu anisaidie...

Preta my love, naomba uwe serious apa uache yale majibu yako yakiboya...

Please, njoo mpnz
Utapigwa dogo.....kucha na meno yako chunga sana
 
Preta nikubali usione aibu,
Kuitwa vampire isiwe sababu,
Humu JF kuna mijitu ya ajabu,
Lakini wewe mpenzi ni kama dhahabu

Mimi ni yatima nionee huruma,
Pia ni bikra skuwa na demu uko nyuma,
Kila nkitongoza ilikuwa inabuma,
Lakini kwako mpenzi ntakuwa imara kama chuma..

We ni mzuri, jina lako ni preta,
Nikikupata hapa JF ntapeta
Najua huwezi kunipwerepweta,
Japo snitch wanaponda, na uzushi kuleta

Preta ooooh pretaaaaaa nikubalieeeee

Preta oooh pretaaa usinizingueeee

Mapenzi ni kujituma, si uonewe huruma
Wewe hata si yatima, mali nyingi umechuma
Tochi yako naizima, gizani mpaka kiama
Huruma ni kwa walemavu na wasiojiweza, sio kwenye mahaba

Tengeru ni karibu, upweke katu hutaona
Njoo kwangu unitibu, maumivu nitapona
Tafanya taratibu, gusa kila kona
Preta achana na Vimpire_hunter, jina lake na avatar vinatisha.

Sooth maanaye mkweli, mi jina langu thabiti
Ninayo tamu asali, na kuna pipi kijiti
Achana nae wa mbali, ni kigumu kizingiti
Nitafute Tengeru Sokoni, siku ya mnada

Sina hata benzi, naamini sio kigezo
Pata na la dhati penzi, natilia sana mkazo
Hao sugu kwa uzinzi, kwao huo ndio mchezo
Preta, we will meet somewhere, someday in Arusha-I hope!
 
Kaka umejichanganya kuanza mashairi, huo ni uwanja wangu wa nyumbani!!

Uwanja wa nyumbani kwako, haunikoseshi preta
Hebu ishia zako, usilete za kuleta
Kauze mitumba yako, huko sokoni haji Preta
Na hayo mashairi yako, wala hayanipi presha

Preta ni wangu mimi, subiri uone mwisho wa uzi
Atanikubali mimi, hadanganywi na wanuka ushuzi
Mengine hapa sisemi, nasubiri uniuzi
Takupa tungo za semi, mpaka ukose usingizi

Preta nampenda sana, japo sjawai kumwona
Kimpata ntamtunza sana, mtoto apate kunona
Arusha mtalia sana, si tutabaki kuwang'ong'a
Wacha nsiseme sana, dushe lisijesimama

Pretaa oooooh pretaaaaa usimskize Soooooth

Pretaaa oooh pretaaa nipe mavituuuuuuuth
 
Umetisha mkubwa, subiri majibu ya NECTA😀
 
Wauzaji wa mitumba, hata si watu dhalili
Ashakum! we mshamba, umeonyesha dalili
Mitumba ni adimu pamba, kuzivaa ni kama zali
Kwenye mitumba hakuna saresare, kila mtu hutoka tofauti

Preta hahitaji matunzo, anahitahi nzito huba
Kwao wanao uwezo, anapata mahitaji si haba
Hongo huleta mzozo, pesa pelekea kahaba
Hapa ni raha na utamu tu, pesa ni majaliwa-leo zipo kesho hazipo

Hamuchelewi kudai, mlivyotoa kwa hiari
Wewe mfano hai, umemdai Asha tayari
Umeruka juu kama Tai, anzisha kwangu hatari
Mbona wewe hujarudisha ulivyopewa, mpaka ukawa unahonga?

Wakujua kwa mromboo, nyama choma ya mbuzi
Nyama mpaka kokolikoo, hapana fanya ajizi
Waisikia tu moshonoo, hujafanya uchunguzi
Huko ndo kuna raha zetu sie wa 'Sokoni'

Preta kwako hoi hoi, moyo wangu watweta
Achana na huyo goigoi, maombi rasmi naleta
Kwa mwingine sitoi, kwako sana nitapepeta
Shughuli naiweza, kila siku hata ukitaka
 
Kubali tu hakuna namna jamaa ameandaa haya mashairi mda mrefu sana. Na unaweza usiyapate jama haya maisha yako yote aisee.

Duc in Altum
Nasikia zenji moto unawaka
 
Back
Top Bottom