Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu

Prof. Assad: Niliondolewa kazini kinyume na taratibu kwasababu nilikuwa sifuati maelekezo ya Mtu

Magu alikuwa sahihi kabisa huyu mzee mara agombane na bunge mara achokonoe mambo ya ikulu...sasa naona maumivu ya kupigwa benchi hayajapona.

Hii ni nchi ukitaka uwa outshine wenye mamlaka lazima upigwe na kitu kizito.
Mwili nyumba akili kisoda..
 
Analazimisha kuonekana ni mtu msomi anaejielewa ana misimamo.

Bahati mbaya alikutana na Chuma.

Nilichokuwa nampendea yule baba JPM ukijifanya wewe ni wa muhimu sana kwenye hii nchi yeye anakuonesha namna ulivyo takataka tu na nchi inaweza kwenda mbele bila wewe hahahah.

Profesa uliondolewa na kidume sasa unalialia nini!!?
Na huyo kidume yuko wapi sasa hivi 😀 😀 kazi kweli kweli.
 
Bimkubwa amstiri huyu Mzee asije akajifia kihoro.

Akina Dr Dau wako kimya tu japo wana mengi ya kuongea ni kwa vile wanaona ni inconsequential kwa sasa.

Wapi Prof Safari na awamu ya tatu?
 
Aseme nae alifoji cheti na ndo maana ana nyodo sana.
Kazi.iliisha aache wengine nao wafanye,
Kama hakujiandaa basi elimu anayo afungue hata shule afundushe ili aendelee kujipatia kipato.

Wakiwa makazini wanashauri watu watumei akiri zao kujiajili lakini wao hawawezi.
Si ni VC wa chuo MUM hapo Morogoro?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu nae!

Sasa analialia nini anataka arudishwe au?
Hana pesa njaaa kali huu ni wakati wa yy kulea wajukuaaa toka alipo pata ajira take ya kwanza na mshahara wake wa kwanz bado tu anataka ajira serikarini afungue shule
 
uchumi wa katikati lakini hamuwezi kunywa hata chai ya maziwa ila enzi zao babaake aliweza kuwanywesha chai ya maziwa japo nchi ilikua hoi, hahaaa huyu mzee wamuache tu akatize, logic kama logic yaani halafu litakuja takataka flani hapam litapinga kisa liko kule chama mbogamboga
 
Huyu mzee Assad hafai, ni mjivuni sana na ni kati ya watu wasiojali utu wala huruma kwa wengine. Zamani nilikuwa simjui nilidhani ni mtu safi kwa sababu ni muislam na sijda juu lakini nilipomfahamu zaidi ndio nikajua huyu mzee hafai kuwa kiongozi.

Kwa sasa ni makamu mkuu wa chuo kikuu cha waislam Morogoro (MUM), amesababisha wanafunzi wengi walioshindwa kumaliza ada zao kuacha vyuo na wengine kurudia semester yote kwa sababu alikataa katakata kuwasikiliza sababu zao. Aliteuliwa kuwa makamu mkuu wa chuo kipindi kile 2019 ambapo covid ndio imepamba moto na wazazi hawakuwa vizuri kiuchumi kwa hiyo wanafunzi wengi waliomba kufanya mtihani bila kukamilisha ada lakini hili zee lilikataa kuwasikiliza.

Ni mzee mshenzi asiyefaa kukaa ofisi ya umma. Ana maringo sana mpuuzi huyu.
Sio kweli
 
Analazimisha kuonekana ni mtu msomi anaejielewa ana misimamo.

Bahati mbaya alikutana na Chuma.

Nilichokuwa nampendea yule baba JPM ukijifanya wewe ni wa muhimu sana kwenye hii nchi yeye anakuonesha namna ulivyo takataka tu na nchi inaweza kwenda mbele bila wewe hahahah.

Profesa uliondolewa na kidume sasa unalialia nini!!?
Ndugu,
Kauli (si hoja) hiyo ingekua yatokana na weledi, BASI nchi yetu ingekua yaanza kungoa nanga KIAKILI na kutoka kwenye ushabiki wa kijinga.
KWA bahati mbaya sehemu kubwa ya SISI waafrika weusi, kama wachawi, huwa tunashangilia zaidi matukio ya kukomoana/dhulma.
Ee Mungu tusaidie TUANZE KUJITAMBUA. AMEN
 
Ni mtu pekee kati ya wateule wa Magufuli aliyekuwa na uwezo wa kumkosoa waziwazi. Hakuwa mtu wa kulamba miguu na hiyo ndiyo sifa ya mwanamume.
Profesa Assad hakuwai kumkosoa Magufuli akiwa hai... nakumbuke pale ikulu aliulizwa kuhusu trilion 1.5 alisema kuwa hakuna iliyopotea.... baadae ndio akaanza kuogombana na bunge........na akaondolewa.... Assad hajawai kupambana na Magu hata siku moja ... Assad kaanza kusema baada ya Magufuli kufariki... mtu pekee aliyekuwa na uwezo wa kuongea Magu akiwa hai ni Tundu Lissu tuu
 
kwahiyo kwa akili yako ulitaka agombane naye hadharani na unajua kabisa alikua kichaa? tumia akili ndugu nimesema kwenye simu alikua anampiga spana mbayaaa kabisa, hata ingekua wewe lile dubwana na wazimu wake silingekuua palepale kwa mkono wake tena bila kuamuru walinzi
 
Acha kumsingizia Prof bwana awezi kumtukana au kumsema Rais akiwa hai... Prof kasema yoye hayo baada ya chuma kufariki.... nchi hii ilikuwa ina wanaume wawili Lissu na Magu tuu
 
Kwa hiyo anataka arudishwe kwa sababu hakumakiza muda wake? Ili amalizie
Mwendazake alivunja Katiba ya JMTZ ndio hoja.
Kwa katiba iliyopo alieichezea katiba anabaki salama na majigambo mengi. Jaji Mkuu kwa vile alikuwa anakaimu nae akanyamaza hata hivyo sasa hivi katuthibitishia kuwa nae anaogopa KATIBA mpya.
 
Back
Top Bottom