Prof. Assad: Sitapiga tena kura labda mfumo uwe wa kidigitali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad amesema hatojisumbua tena kushiriki zoezi la kupiga kura.

Amesema hayo kwa hoja ya kwamba Watanzania huwa wanashiriki kupiga kura lakini hawashiriki uchaguzi. Kwa maana ya kwamba kura haina maana katika uchaguzi.

Aidha amesema ataweza kushiriki pindi mfumo mzima wa upigaji kura ukiwa wa kidigitali. Kwa kuwa ilivyo hivi sasa kuna udanganyifu mkubwa hivyo upigaji kura hauna thamani.
 
Labda kama hukumuelewa vizuri. Lakini kama ndio mawazo yake hayo Prof, ima anajitoa ufahamu makusudi ili tuje kuambiwa uko mradi mbeleni wa tume ya uchaguzi wa kura kupigwa kidigitali. Prof hajui ya Bush na Al-gore?

Kuiba kura kidigitali itakuwa rahisi sana maana kuchezea mfumo wa kidigitali hahitaji gharama wala manpower kubwa. Kutumia mfumo wa kizamani kama mataifa mengine inaweza kuwa na gharama kubwa sana. Zingatia suma na nduguze kudaiwa kushindwa kulinda tanzanite hawana imani nao tena, iko hofu ya kulipiza kuchafuliwa.
 
Marekani wanapiga kura kidigitali na bado wanatuhumiana wizi.Trump na Biden wanatuhumiana kuhusu hilo

Yawezekana Profesa anachomekea kupima upepo kuna watu wanajianda kuchota pesa kupitia mradi wa kigitali wa kupiga kura.Hii miradi hewa hewa hii isiyoguda maisha ya wananchi walio wengi kuns wakwapuaji wansjipanga hapo
 
Back
Top Bottom