Prof. Assad: Sitapiga tena kura labda mfumo uwe wa kidigitali
CAG Mstaafu Prof Mussa Assad amesema hatapiga kura nchi hii hadi tutakapomudu kupiga kura Kidigitali na kuiona mubashara kura Yako inaenda kwa mlengwa

Assad amesema nchi hii tunapiga kura lakini hatuchaguani

Eid al Adh'haa Njema!
My president is Black- Young Jeezy ft Nas
 
Nchi hii punguani inaonekana mpo wengi.

Mtu kama wewe kwa upeo na akili yako ilivyo, huwezi kuelewa logic ya statement ya prof. Assad. Ni wake tu wenye akili inayofanya kazi ndio wataelewa.
Kwahiyo wewe ni mmoja wa hao wake zake wanaoweza kuelewa?
 
Namuunga mkono mia kwa mia, fisiemu wanafanya upuuzi sana kunajisi chaguzi.

Kama vipi tuache kupiga kura wawe wanachaguana tu huko ndani ya chama chakavu.
 
CAG Mstaafu Prof Mussa Assad amesema hatapiga kura nchi hii hadi tutakapomudu kupiga kura Kidigitali na kuiona mubashara kura Yako inaenda kwa mlengwa

Assad amesema nchi hii tunapiga kura lakini hatuchaguani

Eid al Adh'haa Njema!
Hivi Bado ni machungu tu ya kuondolewa USIAJI??
 
Huyu mwamba wakati huo Tulimuita MJ Assad pale udsm akiwa kijana mdogo sana

Akiongea kwa besi na sauti ya kujiamini sana
Utamsikia

Debit: Cash
Credit:Credit Machinery Account

Alikuwa msela sana anatembea kwa kudunda dunda tunamuita mzee wa USA na alikuwa anagonga english ya Marekani vibaya sana

Debit and credit has got no meaning but it depend on assumption of the user although all assets have debit balance when they increase

Watu wengi walihudhuri kipindi cha Assad Ac 100 na Ac 101

Wale wazee wa PCM na PCB halafu mnaingia Business ilikuwa raha sana ,umetoka huko hujui Debit wala credit ndio unalikuta kwa MJ Assad(Mus Juma Assad)

Huyu mwamba alikuwa ni Seminar leader chini ya Sister wa kikatoliki akiitwa sister Baptister pale FCM yaani facult of commerce and Management sasa vijana wanaita UDBS

Mwamba akifika darasani anatembea kwa kudunda dunda na sandles kubwa

ASSAD alikuwa msela nondo fulani hivi anaongea kimarekani

Huyu alikuwa mzee wa teknolojia sana na master mind wa excell enzi hizo watu hawajui hata maana ya power point

Miaka inakimbia sana eti leo ni Prof mstaafu wakati sisi tulimuacha Seminar leader pale UD
Kana alikuwa anasema ' it depend' badala ya ' it depends' basi huyo alikuwa anaongea english ya kijijini kwako wala si ya Marekani! Utamsifiaje kwa english chafu namna hii?
 
Back
Top Bottom