Prof. Assad: Sitapiga tena kura labda mfumo uwe wa kidigitali
Labda kama hukumuelewa vizuri. Lakini kama ndio mawazo yake hayo Prof, ima anajitoa ufahamu makusudi ili tuje kuambiwa uko mradi mbeleni wa tume ya uchaguzi wa kura kupigwa kidigitali. Prof hajui ya Bush na Al-goore?

Kuiba kura kidigitali itakuwa rahisi sana maana kuchezea mfumo wa kidigitali hahitaji gharama wala manpower kubwa. Kutumia mfumo wa kizamani kama mataifa mengine inaweza kuwa na gharama kubwa sana. Zingatia suma na nduguze kudaiwa kushindwa kulinda tanzanite hawana imani nao tena, iko hofu ya kulipiza kuchafuliwa.

kachemsha
 
Yalifaa kusemwa toka ujana maana hayajaanza leo [emoji753]
Shetani akizeeka anakuwa Malaika Kuna siku Maela na Kaijage watasema hivi na tutawashangilia[emoji86]
 
Mbona hakukuwa na mabadiliko kabla yake?

Je. Unakumbuka Msee wa Msoga a.k.a JK alianzisha mchakato wa Katiba Mpya CCM haohao wakauvuruga...??
Jiwe alipoingia akakataa kuhuisha mchakato akidai swala la Katiba Mpya ATI HALIMO KWENE ILANI YA CCM....Nonsense!!!
Mwenda zake alipaswa kuulizwa wakti Bunge Maalumu la Katiba linakaa, JK alikuwa akitekeleza Ilani ya Chama gani???
 
Yalifaa kusemwa toka ujana maana hayajaanza leo [emoji753]
Shetani akizeeka anakuwa Malaika Kuna siku Maela na Kaijage watasema hivi na tutawashangilia[emoji8]

Uliwahi kusoma wapi Upuuzi Kama huo ati SHETANI AKIZEEKA ANAKUWA MALAIKA...??? There's nothing like that anywhere in the Bible.....!!! The Devil is a devil and an Angel is an angel. Period!
Hivo tuondolee hapa ujinga wako wa kutaka kupotosha Neno la Mungu!!
 
Je. Unakumbuka Msee wa Msoga a.k.a JK alianzisha mchakato wa Katiba Mpya CCM haohao wakauvuruga...??
Jiwe alipoingia akakataa kuhuisha mchakato akidai swala la Katiba Mpya ATI HALIMO KWENE ILANI YA CCM....Nonsense!!!
Mwenda zake alipaswa kuulizwa wakti Bunge Maalumu la Katiba linakaa, JK alikuwa akitekeleza Ilani ya Chama gani???
Kumbuka JK ndo alikuwa Mwenyekiti mda ule na alikuwana uwezo wa kumaliza mchakato wote, maana alikuwa na Dora pia alikuwa anamiliki CCM. Swali kwa nini alikwepa kumalizia katiba. Yeye ndo anajua yupo tumuulize na ulivyosema CCM ndo waliharibu atatakuwa anajua.
 
Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad amesema hatojisumbua tena kushiriki zoezi la kupiga kura.

Amesema hayo kwa hoja ya kwamba Watanzania huwa wanashiriki kupiga kura lakini hawashiriki uchaguzi. Kwa maana ya kwamba kura haina maana katika uchaguzi.

Aidha amesema ataweza kushiriki pindi mfumo mzima wa upigaji kura ukiwa wa kidigitali. Kwa kuwa ilivyo hivi sasa kuna udanganyifu mkubwa hivyo upigaji kura hauna thamani.
Aanzishe na yeye chama Cha siasa ili akishinda aje afanye anachofikiri ni sahihi
 
Huyu mwamba hakika ni mtu sahihi!! Pia kwanini dini ya kislam upo makini hivi?
Kwa kuwa kwenye uislamu,tunaamini na kuona dunia ni sehemu ya kupita tu,hatutaishi milele,kwa hiyo lazima tuishi vizuri,tutende haki kwa yeyote,hatuwezi hua tutaandika lini,wapi,na saa ngapi,na Nani atakusaidia kwenye kukuzika.
 
Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad amesema hatojisumbua tena kushiriki zoezi la kupiga kura.

Amesema hayo kwa hoja ya kwamba Watanzania huwa wanashiriki kupiga kura lakini hawashiriki uchaguzi
Prof anachanganya "kujisemea yeye" na kuwasemea watanzania: hama moral authority ya kutusemea- aendelee kukisemea tuuuuu
 
CAG Mstaafu Prof Mussa Assad amesema hatapiga kura nchi hii hadi tutakapomudu kupiga kura Kidigitali na kuiona mubashara kura Yako inaenda kwa mlengwa

Assad amesema nchi hii tunapiga kura lakini hatuchaguani

Eid al Adh'haa Njema!
Huyu mwamba wakati huo Tulimuita MJ Assad pale udsm akiwa kijana mdogo sana

Akiongea kwa besi na sauti ya kujiamini sana
Utamsikia

Debit: Cash
Credit:Credit Machinery Account

Alikuwa msela sana anatembea kwa kudunda dunda tunamuita mzee wa USA na alikuwa anagonga english ya Marekani vibaya sana

Debit and credit has got no meaning but it depend on assumption of the user although all assets have debit balance when they increase

Watu wengi walihudhuri kipindi cha Assad Ac 100 na Ac 101

Wale wazee wa PCM na PCB halafu mnaingia Business ilikuwa raha sana ,umetoka huko hujui Debit wala credit ndio unalikuta kwa MJ Assad(Mus Juma Assad)

Huyu mwamba alikuwa ni Seminar leader chini ya Sister wa kikatoliki akiitwa sister Baptister pale FCM yaani facult of commerce and Management sasa vijana wanaita UDBS

Mwamba akifika darasani anatembea kwa kudunda dunda na sandles kubwa

ASSAD alikuwa msela nondo fulani hivi anaongea kimarekani

Huyu alikuwa mzee wa teknolojia sana na master mind wa excell enzi hizo watu hawajui hata maana ya power point

Miaka inakimbia sana eti leo ni Prof mstaafu wakati sisi tulimuacha Seminar leader pale UD
 
Mzee keshashiba ubwabwa wake sasa anaropoka tu. Mwambie, sisi tutaendelea kupiga kura. Kura yake moja haisaidii chochote.
Namuona hapo chini ukipeleka ufagio kwa Asad na ndio akakuambia hayo.
FB_IMG_1688038903829.jpg
 
Hata Mimi supigi kura asee.

Unaamka mapema kwenda kujipanga mstari Kama unawahi foleni ya maji ,unamchagua kiongozi wako Safi alafu unakuja kusikia nchi nzima wameshinda sisiem. Yani siyo jimboni kwako pekee,bali Tanzania nzima wameshinda chama kimoja tu,sisiem.

Hakuna uchaguzi wa namna hiyo,nipo sambamba na CAG.
 
Back
Top Bottom