Huyu mwamba wakati huo Tulimuita MJ Assad pale udsm akiwa kijana mdogo sana
Akiongea kwa besi na sauti ya kujiamini sana
Utamsikia
Debit: Cash
Credit:Credit Machinery Account
Alikuwa msela sana anatembea kwa kudunda dunda tunamuita mzee wa USA na alikuwa anagonga english ya Marekani vibaya sana
Debit and credit has got no meaning but it depend on assumption of the user although all assets have debit balance when they increase
Watu wengi walihudhuri kipindi cha Assad Ac 100 na Ac 101
Wale wazee wa PCM na PCB halafu mnaingia Business ilikuwa raha sana ,umetoka huko hujui Debit wala credit ndio unalikuta kwa MJ Assad(Mus Juma Assad)
Huyu mwamba alikuwa ni Seminar leader chini ya Sister wa kikatoliki akiitwa sister Baptister pale FCM yaani facult of commerce and Management sasa vijana wanaita UDBS
Mwamba akifika darasani anatembea kwa kudunda dunda na sandles kubwa
ASSAD alikuwa msela nondo fulani hivi anaongea kimarekani
Huyu alikuwa mzee wa teknolojia sana na master mind wa excell enzi hizo watu hawajui hata maana ya power point
Miaka inakimbia sana eti leo ni Prof mstaafu wakati sisi tulimuacha Seminar leader pale UD