Prof. Issa Shivji: Nilihudhuria birthday ya Mwalimu, sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha

Prof. Issa Shivji: Nilihudhuria birthday ya Mwalimu, sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha

Miaka 96 na 70 kuna tofauti kubwa,
kumpa zawadi haimaanishi yeye hana uwezo ,ni kuonesha jinsi gani mnamthamini na kumpongeza kufikia umri ambao ni wachache wanapata bahati ya kuufikia
Juzi kwenye mkutano wa wazee, watoto wameambiwa wawalee wazee wao.

Lakini Rais Mwinyi wa Zanzibar yeye hahusiki kumlea mzee wake.

Wabongo ni wajinga na waoga ila siyo kwamba hawajui kinachoendelea.
 
mwambie profesa.
ZAMA ZIMEBADILIKA.
Kipindi cha Nyerere sio cha Samia.

Someni na haya ndio utoe majibu
 
Majibu yangu NI Yale Yale.
Mwambie profesa Zama zimebadilika.
Kipindi cha Nyerere sio cha Samia

Someni na haya ndio utoe majibu
 
Issa Shivji nae kaanza kuongea?
Alivyo jifanya bubu wakati wa Magufuli? Keshasahau?
Shivji ni communist..failed ideology...
Kuna hawa wazee bado tu wanataka tuishi kama miaka ya 80 sababu Nyerere hakufanya hivi basi sote tufanye kama Nyerere. Miaka hiyo pesa za mishahara tu ilikuwa shida.

Ila jamani nchi kuna watu wana roho za korosho wanamuonea wivu mpaka mzee wa miaka 96. Je kama kuna watu wametoa hiyo pesa wamempa Mama ampe mzee watasemaje.

Halafu hizo gari 20 JPM alipewa zawadi na mfalme wa Morocco. JPM wakati wake alikuwa anatembea na mabunda anawapa watu njiani lakini wazee kama hawa roho za korosho walikuwa wameufyata kimya.
 
Gari linataka kuwatoa roho watu

Ova
 
Nadhani alipaswa kutoa hela zake sio umma. Yote haya bado wanatoa hela za umma tu.

Sasa Kama anaweza kumpa mwenzake 460 milion, yeye anaweza kujipa shilling ngapi?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Labda wamekusidia waje kulitumia wana , wajukuu na vilembwe vyake!

Imeshangaza!

Mtu ambaye mwanae ni Rais?!
 
Kwenye nchi zenye wanaojielewa ilipaswa hata thamani ya hiyo gari iwekwe hadharani Umma ujue kodi zao zinavyotumika.

Kuna wananchi hata zahanati ya karibu hakuna vijijini huko.

Kwenda hospitali ya Wilaya ni kama kwenda mkoani.

Barabara mbovu.

Wanakijiji hadi wachange usafiri sivyo mgonjwa au Mama mjamzito atabebwa machela.

Wakifika hospitali vifaa tiba hakuna.

Hakuna utrasound , mitungi ya gas ya wagonjwa ambao wanahitaji kupumua kwa gas kwa muda wakati akiendelea na dawa ili baada ya muda anaanza kupata nafuu kadiri anavyotumia dawa hakuna.

Mgonjwa anaandikiwa dawa akanunue Phamacy.

Wabunge wao hawafuatilii, n.k

Ukitafakari inauma !

Wengine anaumwa tumbo tu inashindikana kufanyiwa sufficient investigation,

Madaktari wakutosha specialists hakuna,

Anaambiwa apelekwe rufaa hospitali ya mkoa au Muhimbili, uwezo wa nauli hawana wanakata tamaa mgonjwa anarudishwa nyumbani kijijini hadi anakufa ! [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1999, ambayo ilirekebishwa mwaka 2005, inaeleza kuwa Rais Mstaafu anapomaliza kipindi chake cha uongozi, hupata mafao ya mkupuo.

Ingawa kiwango cha mshahara wa Rais wa Tanzania ni siri, sheria hiyo inaeleza kuwa mafao yao hukokotolewa kwa kuzingatia mshahara wa juu aliowahi kupata miezi aliyofanya kazi.

Kiwango cha mafao hayo hukokotolewa kwa kutumia kanuni za kiwango cha asilimia itakayopangwa na mamlaka husika.

Mbali ya mafao yake ya kazi, Rais Mstaafu hulipwa posho ya kila mwezi kiasi cha asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani. Kiasi hicho ni sawa na Sh80 kwa kila Sh100 anayopata Rais aliye madarakani.

Licha ya posho hiyo, Rais hupewa ulinzi, msaidizi, katibu muhtasi, mhudumu wa ofisi, mpishi, dobi, mtumishi wa ndani, mtunza bustani, madereva wawili na gharama za mazishi atakapofariki.

Mafao mengine

Pamoja na malipo ya mkupuo anayopata Rais Mstaafu, pia anapewa pasi ya kusafiria ya hadhi ya kidiplomasia, yeye pamoja na mke au mume wake.

Rais pamoja na mke wake, pia hulipwa gharama za matibabu ndani au nje ya nchi.

Baada ya kustaafu rais pia hulipiwa matengenezo ya magari mawili yenye uzito usiopungua tani tatu, ambayo hutolewa na Serikali, ambayo pia hubadilishwa kila baada ya miaka mitano.

Kama hiyo haitoshi, Rais pia hujengewa nyumba mpya, ambayo ni lazima iwe na vyumba angalau vinne, viwili kati ya hivyo ni lazima viwe na huduma zote ndani (self-contained).

Aidha, nyumba hiyo ni lazima iwe na ofisi iliyokamilika na nyumba kwa ajili ya mfanyakazi wake.

Rais huyo mstaafu vilevile atagharimiwa gharama za mazishi pindi atakapofariki.

Makamu wa rais na mawaziri

Mafao hayo ya viongozi wa umma yanampa nafasi Waziri Mkuu mstaafu na makamu wa rais fursa kama anazopata Rais, isipokuwa wao hawajengewi nyumba, pia wanapata gari moja tu.

Makamu wa rais na waziri mkuu wastaafu wanapewa fedha za kulipa mishahara ya watumishi, mpishi, dobi, mfanyakazi wa ndani, mtunza bustani na dereva.

Sheria hiyo inawakinga pia wategemezi wa viongozi wastaafu, hasa viongozi hao wanapofariki.

Kinga ya wategemezi wa viongozi hao iliundwa katika marekebisho ya Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Siasa ya Mwaka 1999, ambayo ilitiwa saini na Rais mstaafu Benjamin Mkapa Juni 2005. Marekebisho yaliyotiwa saini na Rais Mkapa ni pamoja na kuwalipa mafao wajane na wagane wa viongozi wa juu wa kitaifa akiwamo rais, makamu wa rais na waziri mkuu.

Rais mstaafu akifariki dunia, mke au mume wake hupewa nyumba, posho kiasi cha asilimia 40 ya mshahara wa rais aliye madarakani.

Aidha, mjane au mgane huyo hutengewa fedha za matibabu ndani ya nchi na matengenezo ya gari analopewa na Serikali.

Pia hulipiwa mshahara wa kima cha chini kwa dereva na mtumishi wa ndani pamoja na hupewa usafiri wa kwenda mahali atakapoishi maisha yake yaliyosalia.

Mabadiliko hayo yalilenga pia kuhakikisha kuwa iwapo kiongozi husika alikuwa analipwa pensheni kwa ajira ya awali, malipo yake yataendelea kutumiwa na mjane.

Aidha katika kikao cha Bunge la Bajeti mwaka uliopita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema kuwa Serikali imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya matibabu ya wastaafu wanaopaswa kutunzwa na Serikali.
 
Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1999, ambayo ilirekebishwa mwaka 2005, inaeleza kuwa Rais Mstaafu anapomaliza kipindi chake cha uongozi, hupata mafao ya mkupuo...
Kwa mujibu wa sheria tulizotunga wenyewe haya ni haki ya mstaafu tena gari 2 kubadilishiwa kila baada ya miaka 5 sasa mtu mzima ana miaka 96 usiposaidia leo utamsaidia lini? tusome kwanza sheria zetu tulizojiwekea wenyewe. zile nyumba JPM kawajengea kwa mujibu wa sheria kama sheria mbaya mkazibadilishe. mwacheni mzee apumzike tuacheni na viroho vya kwanini.
 
kipindi hicho Nchi haikuwa na pesa kwa sasa tumeingia uchumi wa kati na Nchi yetu kwa sasa ni Tajiri linawezekana tuache kulaumu. suala la kutoa zawadi halipo kwenye katiba ya Nchi. tumuombee mzee wetu kwa kufikisha umri mkubwa
 
Mfano ulikuwa juzi hapa kwenye ugonjwa wa korona ,

Hospitali za mjini tu mitungi ya gas ilikosekana kikidhi mahitaji.

Je ni watu wangapi wamepoteza maisha kwaajili ya hilo?

Je ni wangapi wangeweza kuokolewa maisha yao wakapona iwapo wangepata huduma stahiki kwa wakati?

Sijui wamejifunza kitu kikubwa?
 
Back
Top Bottom