Prof. Issa Shivji: Nilihudhuria birthday ya Mwalimu, sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha


Hata ingekua mil 9, pesa za wananchi sio pesa za kuchezewa hovyo , bora wangenunuliana huko pembeni, sasa anatuambia hili iweje? Nchi ina shida kila sehem , c bora angeenda kugawia maskin
 
Loliondo aliwamilikisha waarabu kwa miaka mingapi? Huyu ni mhujumu uchumi aliyetakiwa kuwa jela badala ya kulipwa pensheni na watanganyika maskini.
Ukiamua kuwafuatilia marais wote utagundua kuwa kwa ujumla wao baada ya kutoka ikulu walitakiwa wakafungwe.

Hakuna rais msafi hata mmoja siku zote ni wachafu na wamejaa dhambi. Huyo alifanya kazi kubwa sana kwani aliikuta nchi ipo hoi bin taabani.

Mageuzi aliyofanya Mkapa msingi wake ulianza kuwekwa na huyu Mzee.
 
Ok, tujulishe thamani yake wewe unayeifahamu!
Kama nilivyosema awajalionyesha mabonet yote la nyuma na mbele kulitambua vizuri.

Shape yake inaelekea kuwa S class but you can’t pin point which year either way inaonekana ni tolea la zamani, ukichungulia alloy wheels na ndani kwenye break-pads cover unaona gari limetumika.

Kwa gari lile inategemea na specification zake bei inaweza kuwa kati £15-30K kama unaagiza used with low mileage.
 
Kwa maoni yangu zawadi sio jambo la msingi sana kujadiliwa,

nadhani hata yeye mwenyewe Mzee wetu Babu yetu wa Taifa Mzee Ruksa atafarijika zaidi akiona tunajikita kujadili MAUDHUI ya kitabu chake alicho kiandika badala ya kujadili ZAWADI aliyo pewa.

Mother Teresa ana Tabia ya kujipendekeza sana hadi anaboa, anajifanya malaika anatak kumlizisha kila mtu ,
 
Hata ingekua mil 9, pesa za wananchi sio pesa za kuchezewa hovyo , bora wangenunuliana huko pembeni, sasa anatuambia hili iweje? Nchi ina shida kila sehem , c bora angeenda kugawia maskin
Hakuna sehemu nimesema mzee Mwinyi anastahili hiyo zawadi.
 
Msimamo wa dini ya Kiislamu katika jambo hili ni mkali sana. Huwezi kuchukua mali ya watu ukaitumia upendavyo.
Bwana mmoja aliwahi kwenda kwa Khalifa Omar bin Al Khattab, usiku. ( Omar alikuwa ndiye rais wa Waislamu wote wakati huo waliofikia takriban milioni 4 na mali zilizokadiriwa dola bilioni 7 (kwa sasa) wakitawala mataifa ya Rumi (wazungu) na Waajemi (Iran). Akamkuta anafanya mahesabu ya pesa zilizoletwa kama Zaka kutoka mikoa ya Syria na Yemen. Yule bwana akamwambia, nimekuja kwa mzungumzo nawe. Omar akamwuliza, mazungumzo binafsi au ya masuala ya umma? Akasema, ya binafsi. Omar akachukua ile koroboi ilyokuwa inawaka, akaizima. Akamwita bwana yule asogee, gizani. Yule akauliza, vipi, mbona umezima taa? Omar akasema, ndiyo, mafuta ya taa hii yamenunuliwa kwa mali ya umma, si mali yangu. Na wewe una mazungumzo nami ya haja zako binafsi. Nahofia Mwenyezi Mungu atakwenda niuliza juu ya matumizi haya ya mali ya umma!

Huo ndio Uislamu usiofuatwa!
 
Sasa munalinganisha ya Nyerere na sasa! Mbona nyumba aliyojengewa na wanajeshi alipokea?

Enzi ya Nyerere hakukuwa na birthday wala valentine musituzingue jamani.

Hiyo gari ya Mzee Mwinyi ni saizi yake baada ya matusi yote aliyotukanwa na vijana na hata kebehi aliyofanyiwa na Nyerere mwenyewe hadharani wakati alipokuwa anatawala.
Natumai ulisikia ile summary aliyotoa Profesa wa Kigoda jana.
 
Mzee Shivji ameniwahi, hata mimi nilitaka kuhoji "Hivi Mzee Julius kweli angekubali kupokea zawadi ya Benzi kama ile?"
Kwani wanapotoa, si wanapima kwanza mtu wanayemzawadia anamsimamo gani?

Ungeanzia wapi kumpa Mwalimu Benz halafu utegemee atakubali. Si utaaibika mwenyewe unayetoa?
 
Mujue kwanza SHS Ni nani.
Ni mtoto wa mwinyi kwa yule mama mwalimu ila hawakuishi pamoja
Kwa hiyo hii zawadi ya bethi dei imetolewa kwa daddy....mimi sikuwa na taarifa!
 
Wamebadilisha kitabu na Benz safi kabisa.

#Kazi iendelee
 
Hapa kwakweli mama kateleza kidogo. Kuna mahali watu hawana ambulance, wagonjwa wanabebwa na baiskeli. Mama anaenda tupa ela kwenye zawadi za gharama kiasi hiki.

Mama tunakupenda sana ila kwa hili sio sawa.
 
Kwani wanapotoa, si wanapima kwanza mtu wanayemzawadia anamsimamo gani?

Ungeanzia wapi kumpa Mwalimu Benz halafu utegemee atakubali. Si utaaibika mwenyewe unayetoa?
Mwalimu angeongea palepale na kukataa.
 
Hapa kwakweli mama kateleza kidogo. Kuna mahali watu hawana ambulance, wagonjwa wanabebwa na baiskeli. Mama anaenda tupa ela kwenye zawadi za gharama kiasi hiki.

Mama tunakupenda sana ila kwa hili sio sawa.
Hao wasiokuwa na hivyo vitu ni wanyonge na hii sio awamu yao, hao masikini wana roho mbaya sana kwa matajiri sasa awamu hii wakae mbali.
 
Nadhani aliyemshauri amekosea Sana kweli pesa zetu wabara zinachesewa Sana kwa wafanyakazi hela hamna lkn kwa mwinyi pesa ipo kwa kweli inahuzunisha Sana katiba ni muhimu sana
 
Kama kodi zenu zinakuumizeni mbona hajawahi kuwahurumia Wazanzibar, TRA miaka yote wanakusanya kodi Zanzibar zinatumika kwa maendeleo ya bara tu? Mwacheni mama ndio kwanza anatimiza mwezi - mali ya babu jinga huliwa ni wajinga

Duuu kazi ipo.
 
Lina thamani ya sh ngapi?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…