Prof. Issa Shivji: Nilihudhuria birthday ya Mwalimu, sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha

Prof. Issa Shivji: Nilihudhuria birthday ya Mwalimu, sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha

Hata lingekuwa na thamani ya milioni 5, si haki kumpa huyo anayepokea posho 80% ya mshahara wa rais wakati wafanyakazi wakinyimwa nyongeza kwa visingizio vya ukosefu wa fedha.

Vi wapi vipaumbele vya nchi?!
Siungi mkono mzee Mwinyi kupewa zawadi, napinga tabia za watanzania kumeza habari kama inavyokuja zenye premise zisizo sahihi.

Ile Benz ata kama aijaonekana vizuri kutambua kama brand new au mtumba wa mwaka gani haswa; lakini kwa haraka haraka tu aina thamani ya tsh 450 million.
 
Tulisema, Uzanzibar na ubara unatamalaki. Mkabishia. Wameanza na mapato ya muungano kwa asilimia na leo benzi, keshokutwa utasikia arume kapewa ndege.
Alianza mwendazake kumpa nyumba kwanza mukaufyata sasa mama anamalizia tu., kama kodi zenu zinakuume sana kavunjeni majengo ya TRA kule Zanzibar na muache kukusanya kodi ambazo zinakuja kuwasaia huko bara kulipana mishahara yenu na kujenga barabara zenu.
 
"Nilihudhuria 70th (1992) birthday ya Mwalimu. Sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha. Alipokuwa anaondoka, mama mmoja kampa portrait yake aliyechora mama huyo mwenyewe. Akamambia msaidizi wake apokee. Zawadi ya Benz kwa Mzee wetu ikanishtua kidogo."

-- Issa Shivji kupitia Twitter

Sijui kwa nini wazo la Vijana kuwa na Baraza/Jumuia yao rasmi nje ya vyama vya siasa linapuuzwa hasa na serikali.

Vijana hawawezi kuwa wamoja kupitia Jumuia za vyama kwa kuwa Jumuia hizi zinawagawa kuliko kuwaunganisha!

Magufuli alimjengea KIKWETE nyumba.

Magufuli alimjengea MWINYI nyumba.

Rais Suluhu amemnunulia MWINYI Gari la Anasa, aina ya Benz.

Hivi Marais hao wastaafu wenye kulipwa nusu ya Mishahara ya Rais aliyeko madarakani Wanashida hizo?

Hawamudu gharama?

Mr mkiki

Kama sikosei suala la viongozi wakuu wastaafu kujengewa nyumba ni suala la kisheria sio maamuzi ya mtu flani. Na Rais aliyepo madarakani anatimiza takwa hilo la kisheria.
Na kwa sheria hizo hizo serikali inalo jukumu la kuwatunza/kuwalea viongozi wastaafu kwa mujibu wa nafasi zao. Rais ametoa ufafanuzi kwa nini anambadilishia mzee Mwinyi gari, lakini kwa bahati mbaya tumezoea kulalamika na kulaumu. Matokeo yake tumeacha lengo muhimu nakujikita kwenye zawadi ili tupate njia ya kulaumu.
 
Hii nchi inaumiza sana. Viongozi hawapo Serious kabisa na maisha ya watanzania hawa maskini. Unampa mtu ambaye hajawahi kuwa na shida maisha yake yoye Zawadi ya Benzi lenye thamani ya Tsh Mil 450.

Mwinyi ambaye ana majumba,magari,na kila kitu na watoto wake wenyewe walikuwa hawashindwi kumpa zawadi kama hiyo. Mtoto wake ni Rais wa Zanzibar.

Ameona pesa za Wazanzibar zitumike kwenye mambo ya msingi ila kodi za Wabara mama Samia anaona zinafaa kumnunulia Ali H. Mwinyi Benz. Msomeni Prof. Shivji

View attachment 1778664

Mama hapa katereza. Hata lile la nyumba ya JK nalo ni fyongo.

Tusijenge mazingira wezeshi ya kuja kubatilisha mambo kinunda nunda kwenye serikali zijazo!
 
Kusema kwl hata Mimi nilikwazika kuna watoto huko vijijini bado wanakaa chini nusu ya billion ni mtaji wa mama ntiilie wangapi twende nacho turudi nacho hivi familia ya mwinyi mwenye MTT rais pia walishindwa kwl kumpa baba yao hiyo gari ya chinichini... Meku was genius kasuku aliwapa yet ilikuwa bado ni zawadi ya heshima nyumba on utaratibu maana mtasema mbona meko alikuwa anawajengea...basi ingeshindikana bora wangenunua nayo barakoa tugawiwe tu million hizo nyingi mno jamani tuache utani.
 
Naanza kuamini kuwa sehemu sahihi ya mwanamke ni jikoni na chumbani tu
Na yule aliyetoa nyumba kwanza kumpa mzee mwinyi atakuwa mtu sahihi kwa wapi chooni au wapi? em kokomoka
 
Kwa maoni yangu zawadi sio jambo la msingi sana kujadiliwa,

nadhani hata yeye mwenyewe Mzee wetu Babu yetu wa Taifa Mzee Ruksa atafarijika zaidi akiona tunajikita kujadili MAUDHUI ya kitabu chake alicho kiandika badala ya kujadili ZAWADI aliyo pewa.
 
Nyerere kutotaka zawadi yoyote hakumaanishi ndio kipimo cha mtu kutokuwa na makuu. Mzee Mwinyi alijishusha na kujiuzulu uwaziri kwa makosa yaliyofanywa na waliokuwa chini yake mwaka 1975.

Wangapi wanaendelea kushikilia vyeo hata kama walio chini yao wanafanya makosa makubwa yenye kuathiri maisha ya mamilioni?.
 
Hata lingekuwa na thamani ya milioni 5, si haki kumpa huyo anayepokea posho 80% ya mshahara wa rais wakati wafanyakazi wakinyimwa nyongeza kwa visingizio vya ukosefu wa fedha.

Vi wapi vipaumbele vya nchi?!
Waoneeni huruma na Wazanzibar wanakusanya kodi kupitia TRA zinaenda kutumika kwa maendeleo ya Tanganyika tu.,
 
Ile Benz ata kama aijaonekana vizuri kutambua kama brand new au mtumba wa mwaka gani haswa; lakini kwa haraka haraka tu aina thamani ya tsh 450 million.
Ok, tujulishe thamani yake wewe unayeifahamu!
 
Hii nchi inaumiza sana. Viongozi hawapo Serious kabisa na maisha ya watanzania hawa maskini. Unampa mtu ambaye hajawahi kuwa na shida maisha yake yoye Zawadi ya Benzi lenye thamani ya Tsh Mil 450.

Mwinyi ambaye ana majumba,magari,na kila kitu na watoto wake wenyewe walikuwa hawashindwi kumpa zawadi kama hiyo. Mtoto wake ni Rais wa Zanzibar.

Ameona pesa za Wazanzibar zitumike kwenye mambo ya msingi ila kodi za Wabara mama Samia anaona zinafaa kumnunulia Ali H. Mwinyi Benz. Msomeni Prof. Shivji

View attachment 1778664
Hakuna mshituko. Mambo ni yaleyale. Mama keshasema: "Mimi na Magufuli ni wamoja".
 
Mkuu IS hata wakati wa dhalimu alikuwa akiongea kupitia Twitter kuonyesha kutoridhika kwake na yule dikteta katika mambo mbali mbali.
Issa Shivji nae kaanza kuongea?
Alivyo jifanya bubu wakati wa Magufuli? Keshasahau?
Shivji ni communist..failed ideology...
 
Kwa maoni yangu zawadi sio jambo la msingi sana kujadiliwa, tunapoteza malengo na makusudio.

nadhani hata yeye mwenyewe Mzee wetu Babu yetu wa Taifa Mzee Ruksa atafarijika zaidi akiona tunajikita kujadili MAUDHUI ya kitabu chake alicho kiandika badala ya kujadili ZAWADI aliyo pewa.
 
Nyerere kutotaka zawadi yoyote hakumaanishi ndio kipimo cha mtu kutokuwa na makuu. Mzee Mwinyi alijishusha na kujiuzulu uwaziri kwa makosa yaliyofanywa na waliokuwa chini yake mwaka 1975.
Loliondo aliwamilikisha waarabu kwa miaka mingapi? Huyu ni mhujumu uchumi aliyetakiwa kuwa jela badala ya kulipwa pensheni na watanganyika maskini.
 
Hili la Mzee Mwinyi kupewa zawadi ya gari aina ya Benz, eti tu kwa sababu ya kuonewa huruma ya tabu anayoipata wakati wa kupanda na kushuka halijakaa vizuri. Huruma ya namna hii ilipaswa kuwa ya kifamilia zaidi wala si kupitia kodi za wananchi wengi wao wakiwa ni maskini wa kutupwa.

Wote tu binadamu na tunafanya makosa. Ila pia tuna nafasi ya kujifunza kupitia makosa yetu. Rais wetu ni mtu mwema sana na mwenye upendo mkubwa, lakini jambo hili lisimfanye akapitiliza hata kwa kufanya mambo binafsi yenye kuingiliana na majukumu makubwa aliyokabidhiwa kikatiba.

Mother Teresa kesho utasikia Katuuza kwa wakenya. Huyu mama wakat anaapishwa nilijua tu urais sio kalama yake. Anafanya maamuzi ya kimama Mama kila sehem , yupo yupo tu hana msimamo
 
hivi rais wa nchi kutoa zawadi ya gari nayo imekuwa nongwa!?....gari kwa rais?!..
 
Loliondo aliwamilikisha waarabu kwa miaka mingapi? Huyu ni mhujumu uchumi aliyetakiwa kuwa jela badala ya kulipwa pensheni na watanganyika maskini.
wewe ni miongoni mwa watu mliokuwa mnahujumu utawala wa mzee mwinyi. chuki na fitina ni kitu kibaya sana hapa duniani, badilika.
 
Back
Top Bottom