unazijua mortuary zilipo na utajiskiaje ndugu yako anatolewa wodini akikokotwa juu ya kitanda mpka chumba cha maiti ambacho kipo zaidi ya mita 300 kutoka wodini. kwangu naona janabi yupo sahihi ni kuweka mifumo sawaUfie wodini, mwili ubebwe na ambulance kwamba hizo gari zinaingia wodini? Najua mortuary ziko huko huko ndani ya majengo.
Hawa wasomi mbona wanatuchanganya?
Ndio ili ujue kuwa utabebwa na Ambulance endapo likitokea la kutokeaKwanza hii nayo ni habari ya kutangazwa??
Mkuu hebu tuelezee vizuri na sisi tulioko mkoani kwani mochwari hapo muhimbili ziko mbali sana na maeneo ya huduma za matibabu ni kwa umbali gani mfano??Mortuary muhimbili iko mbali na unakouguzwa, janabi hataki upitishwe hadharani ukiwa mfu watu wakuone
Akili kisoda hana lolote, yaani utoe maiti wodini upeleke mortuary kwa Ambulance ? Duuuuuh hao ndio wasomi. Kwanza Ambulance haibebi maiti ni gari ya wagonjwa labda mgonjwa afe akiwa anawahishwa kwenye huduma.Ameagiza miili ya marehemu kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa gari la wagonjwa (Ambulance), badala ya utaratibu uliokuwepo wa kusukuma vitanda ili kutoa heshima kwa marehemu kwa njia hiyo.
Prof. Mohammed Janabi aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), pia amesema Wagonjwa waliotoka Kitengo cha Dharura watabebwa na gari la wagonjwa kupelekwa wodini.
Kwa mujibu wa Prof. Janabi, mabadiliko hayo yanalenga kuwapunguza kazi na mizunguko kwa Wagonjwa na Watendaji wa idara zinazopokea wagonjwa Hospitalini hapo pamoja na kuboresha huduma za Afya.
=======================
Miili ya marehemu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), sasa itapelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa gari la wagonjwa Ambulance’, badala ya utaratibu wa kutumia vitanda.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof Mohammed Janabi, wakati alipokuwa anawaaga wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), alisema mabadiliko mengine ni wagonjwa wanaotolewa katika kitengo cha dharura watabebwa na Ambulance kupelekwa wodini.
“Ambalo tumeanza nalo leo ni kwamba bahati mbaya ikitokea mgonjwa amefariki mwili wa marehemu utachukuliwa na Ambulance kwenda kuhifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti.
“Wagonjwa waliotoka kitengo cha dharura watakuwa wanabebwa na gari la kubebea wagonjwa kupelekwa wodini.
“Kwa sababu ni hospitali kubwa, kwanza tutaanza kuboresha kwa wafanyakazi, itakuwa rahisi mwili kubebwa na Ambulance, kuliko kusukuma, kukiwa na vifo, mwili mmoja uko Kibasila, mwingine uko Sewahaji wanachoka wafanyakazi. Pia kutoa heshima kwa marehemu tunawahifadhi kwa njia hiyo,” amesisitiza Prof Janabi.
Amesema miongoni mwa vipaumbele vyake ni kuboresha huduma za afya na kuiendekeza Muhimbili kuwa hospitali ya Taifa.
Habari LEO
Kwa miguu mtu atakunywa chai vikombe viwili na vitumbua vinne na kumaliza na bado hujafikaMkuu hebu tuelezee vizuri na sisi tulioko mkoani kwani mochwari hapo muhimbili ziko mbali sana na maeneo ya huduma za matibabu ni kwa umbali gani mfano??
Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
Kikubwa aboreshe maslahi ya wafanyakazi, watu walipwe extra duty allowances zao kwa wakatiMwamba namkubali sana Muhimbili lazima ibadilike sana chini ya uongozi wake.
Au milango imepanuliwa vya kutosha ambulance kufika hadi kitandani kwa mgonjwa au marehemu. Ahahahahaha!!!Ufie wodini, mwili ubebwe na ambulance kwamba hizo gari zinaingia wodini? Najua mortuary ziko huko huko ndani ya majengo.
Hawa wasomi mbona wanatuchanganya?
Punguza ujuaji, yeye anajua kuliko weweUfie wodini, mwili ubebwe na ambulance kwamba hizo gari zinaingia wodini? Najua mortuary ziko huko huko ndani ya majengo.
Hawa wasomi mbona wanatuchanganya?
Jibu hoja, acha ushamba
Mamndenyi itakuwa shemeji yetu alikutenda vibaya Sana mbona wanyaki watu safi tuu kasoro ya mmoja usigenelarize kwa woteNimekuelewa, ndo maana una akili kubwa kuliko wote wa kabila lako