Prof. Janabi: Mbinu za kuepuka kuzeeka mapema

Prof. Janabi: Mbinu za kuepuka kuzeeka mapema

Mkurugenzi mtendaji wa hospitali kuu ya taifa ya Muhimbili, Profesa Janabi ameelezea mbinu za kuepuka kuzeeka mapema ambapo ameelezea kama ifuatavyo;

1. Tembea hatua 10,000 kwa siku
2. Kula kwa wastani
3. Punguza wanga
4. Epuka vitu vyenye sukari
5. Epuka sigara, pombe
7. Pata muda kidogo wa kupumzika

Akaongezea, vitu hivyo haviitaji hata senti 5 ya gharama. Akasema tena watu hawafi kwa sababu ni wazee, watu wanakufa kwa sababu ni wagonjwa, ukisoma vitabu vya dini watu walikuwa wanaishi miaka zaidi ya 100.

Leo hii unaweza kukutana na mtu anamiaka 40 na mwingine 30 ukafikiri yule mwenye miaka 30 ndio ana miaka 45.

Sikiliza zaidi.

View attachment 2955861
He looks very young
 
More like a scaremongering campaign than a health advice.

Yeye na mkewe kama wapo happy na wembamba na kwenye kufikia adhma yao wameamua kutokula aina maana nchi nzima wawe vimbao-mbao kama wao.

Dokta wa hovyo sana badala ya kufundisha watu kula balanced diet na kutoa elimu hiyo yeye kila siku anaambia watu leo wąsile hiki kesho wasile kile; jamaa hovyo kweli.

Worst kwenye elimu yake simsikii akito hata basic knowledge za pathophysiology ya hayo magonjwa anayodai yanasababishwa na ivyo vyakula walau mtu aelewe kwanini vina madhara.

Unamwambia mtu atembee step 10,000 a day at the same time unamwambia asile vyakula vyenye starch, sasa ana burn nini mwilini na hiyo nguvu anaitoa wapi wakati vyakula vyote vinavyotengeneza glucose na kuupa mwili nguvu ushazuia, fatty acids pia za ku-burn hakuna.

Yes hivyo vyakula vina madhara na faida zake pia; muhimu kuelewa ni kiasi gani unatakiwa kula kwa siku sio kuacha kabisa unless tayari una maradhi ambayo ukila hivyo vyakula ni shida.

Useless advice
 
Janabi anaeleweka vizuri kwa watu wa high class life, watu choka mbaya life hawatamuelewa kwa sababu vitu hivyo/vyakula hivyo huvipata kwa bahati/nadra sana, na wakivipata huvifakamia kwa kuvila wakidhani hawatavipata tena kwa muda wote
Hebu fikiria, choka mbaya anatoka mwabepande kwa mguu mpaka kariakoo, hapo tayari ni zaidi ya hatua 10,000
hajaona breakfast na wala hajui kama mchana atauona, hapa tayari amekula kwa kiasi
Sukari ni anaionja kwenye chai ya rangi siku akipata kifungua kinywa
Chokambaya anafiti vizuri kwenye maelezo yake lakini bado mbishi
 
Dada,
Unakuta mtu ameyavaa kama sita hivi, kuna za bahati, mara kufukuza majini, mara za kuita majini mazuri n.k 🤣

Ushamba tu
Na hizi za Remmy Ongala ni za nini?

1712491190141.png
 
Kwa hizo mbinu ningetegemea Janabi awe na babe face lakini yeye ndio amekongoroka na ngozi kupauka kama ya marehemu ama kama vile ana miaka 90.

Janabi aache watu waishi. Kuchukua tahadhari za kawaida kwenye maisha ni jambo jema ila Janabi anataka tuwe extreme, ngozi zetu zikose nuru kama marehemu haiwezekani.
Wabongo hamkopeshi mtu,makavuu live live!![emoji23][emoji23]
 
mzee kapambana mpaka kafanikiwa kubadilisha image yake kwa jamii.

akili mingi sana.
 
Back
Top Bottom