Prof. Janabi: Mbinu za kuepuka kuzeeka mapema

Prof. Janabi: Mbinu za kuepuka kuzeeka mapema

Kwahiyo Janabi hapo alipo anajiona kijana? Eti wote ndio tunaelekea huko kwenye uzee đŸ˜€đŸ˜€

BTW Janabi nilikuwa namuona mjanja kumbe nae anavaa hayo mapete ya Kiswahili? He is cancelled.
Au na yeye yumo kwenye lile kundi la wehu pale mawasiliano ….la Good morning billionairessssssssssđŸ˜‚đŸ˜‚đŸ˜‚ ukute hiyo pete kaipata uko …
 
Tatizo lipo kwenye namna ya kuacha Vyakula vyenye wanga ,ugali,wali,mikate,maandazi,mihogo, ndivyo vilivyo karibu nasi na vinaendana na budget zetu
Tunaachaje Kwa mfano
Kwenye food intake kula nusu ya ugali and then ongeza kiwango cha mboga za majani ambazo hazina mafuta.
 
Kwa hizo mbinu ningetegemea Janabi awe na babe face lakini yeye ndio amekongoroka na ngozi kupauka kama ya marehemu ama kama vile ana miaka 90.

Janabi aache watu waishi. Kuchukua tahadhari za kawaida kwenye maisha ni jambo jema ila Janabi anataka tuwe extreme, ngozi zetu zikose nuru kama marehemu haiwezekani.
Weka picha yako na umri wako tukuone, mfananishe na Kikwete tuone kama wanatofautiana sana.
 
Mkurugenzi mtendaji wa hospitali kuu ya taifa ya Muhimbili, Profesa Janabi ameelezea mbinu za kuepuka kuzeeka mapema ambapo ameelezea kama ifuatavyo;

1. Tembea hatua 10,000 kwa siku
2. Kula kwa wastani
3. Punguza wanga
4. Epuka vitu vyenye sukari
5. Epuka sigara, pombe
7. Pata muda kidogo wa kupumzika

Akaongezea, vitu hivyo haviitaji hata senti 5 ya gharama. Akasema tena watu hawafi kwa sababu ni wazee, watu wanakufa kwa sababu ni wagonjwa, ukisoma vitabu vya dini watu walikuwa wanaishi miaka zaidi ya 100.

Leo hii unaweza kukutana na mtu anamiaka 40 na mwingine 30 ukafikiri yule mwenye miaka 30 ndio ana miaka 45.

Sikiliza zaidi.

View attachment 2955861
Anatuchanganya

Screenshot_2024-04-07-09-45-07-937_com.kiwibrowser.browser.jpg
 
Mkurugenzi mtendaji wa hospitali kuu ya taifa ya Muhimbili, Profesa Janabi ameelezea mbinu za kuepuka kuzeeka mapema ambapo ameelezea kama ifuatavyo;

1. Tembea hatua 10,000 kwa siku
2. Kula kwa wastani
3. Punguza wanga
4. Epuka vitu vyenye sukari
5. Epuka sigara, pombe
7. Pata muda kidogo wa kupumzika

Akaongezea, vitu hivyo haviitaji hata senti 5 ya gharama. Akasema tena watu hawafi kwa sababu ni wazee, watu wanakufa kwa sababu ni wagonjwa, ukisoma vitabu vya dini watu walikuwa wanaishi miaka zaidi ya 100.

Leo hii unaweza kukutana na mtu anamiaka 40 na mwingine 30 ukafikiri yule mwenye miaka 30 ndio ana miaka 45.

Sikiliza zaidi.

View attachment 2955861
Huyu jamaa kituko sana...uprofesa wa ujanja ujanja matokeo yake ndio haya..talking cheap issues kwa ajili ya popularity kwa watu wajinga
 
Dada,
Unakuta mtu ameyavaa kama sita hivi, kuna za bahati, mara kufukuza majini, mara za kuita majini mazuri n.k đŸ¤£

Ushamba tu
Maelekezo ya majini hayo!!hao wanalindwa na majini na hayo mapete ni sehemu ya ulinzi na kismati cha pesa!!

Mapete yamesomewa kunuti za kutosha!!hatma ni akhera wote hao huko kuzimu !!
 
Maisha haya hayana formula, kula bata uwezavyo.... mi shahidi kuna watu wanaishi kwa kufuata hayo maelekezo na hakuna matokeo mazuri, hao wanao kiuka wapo fiti balaa
 
Kwa hizo mbinu ningetegemea Janabi awe na babe face lakini yeye ndio amekongoroka na ngozi kupauka kama ya marehemu ama kama vile ana miaka 90.

Janabi aache watu waishi. Kuchukua tahadhari za kawaida kwenye maisha ni jambo jema ila Janabi anataka tuwe extreme, ngozi zetu zikose nuru kama marehemu haiwezekani.
Kutembea hatua 10,000 ni sawa na kutembea kilometers 8. Wee kuweza daily?
 
Sema mtu asipokunywa pombe anakuwa na karoho kabaya kamejikunja muda wote korosho ikasome
This is very true,nimefanyakazi sehemu tano tofauti tofauti yaani ukikutana na mlokole au swala tano wanakuwa na roho mbaya SHETWANI anasubiri.
 
Nilikwenda kijiji kimoja kinaitwa Kimara Iringa nikamkuta kaka yake rafiki yangu nilishangaa kuona ni kijana kuliko rafiki yangu
 
Janabi mwwnyewe sura imepauka utadhani sio profesa wa afya. Hii ni kutokana na mwili kukosa lishe hivyo ngozi inafubaa na kukosa nuru.

Kufuata kanuni za afya ni jambo jema ila sio kuwa mtumwa kwa dunia kwa sababu ya lishe.

Kila jambo hapa duniani lafaa ila hakikisha unadhibiti kiasi kwa ajili ya afya yako

Kuna watu wengi tu hawaishi kama Janabi ila wana afya imara na bora kuliko huyo Janabi mwenyewe.

Hapa duniani zakuambiwa nawe changanya na za kwako.

Kwa namna anavyo amini Janabi leo, yumkini kuna maisha na vyakula kwa dunia ya leo hawezi kuwapatia watoto wake akiamini kuwa vitawadhuru afya lakini vyakula hivyohivyo pengine ndivyo vimemkuza akiwa kinda mikononi mwa mama yake.

Sipingani sana na Janabi kwenye suala la lishe ila napingana na nadharia zake za kutia chumvi masuala ya lishe ambayo hata yeye mwenyewe kiuhalisia huwa hayaishi.
Kakosa lishe au sio?
 
Back
Top Bottom