Prof. Janabi: Nakula mara mbili kwa siku

Ulaji nao inategemea na kazi mtu anayofanya. Kwa hiyo mpasua mawe/ mfyatua tofali ale mara mbili Kwa siku. Au wale wanaokokota baskeli na maroba ya mkaa wale mara mbili Kwa siku Tena kaugali ngumi kama wanavyosemaga
 
Watu wa pwani huwaona watu wa bara kuwa hawajui kula wali. Ukipangwa nao kula sinia moja unatakiwa ule mpaka tumbo lijae pande zote na usibakishe hata punje moja, yaani ule mpaka tumbo lijitokeze kama kitambi. Masheikh wa pwani watakudharau kama utakula wali/pilau kizembe
 
Mimi kuna siku nilisema nifuate huo ushauri wa kula matunda usiku nikanunua matunda mengi ya wiki nzima. Cha kushangaza niliyamaliza siku hiyohiyo niliyonunua. Nikaachana na huo mpango.
watu tunakula lunch sahani nzima ya matunda mchanganyiko na tunashiba kwa muda mfupi tu njaa inauma tena. Hawahawa kina janabi wanaona kula matunda mchanganyiko kwa wakati mmoja si vizuri, wanashauri ule tunda moja tu. Kumeibuka wauza matunda kutuchanganyia matunda mengi tofauti katika sahani moja wataalamu wa mambo ya lishe hawataki tule michanganyiko hiyo kwa wakati mmoja wakidai kuna madhara, wanataka tule tunda moja tu, tena kidogo. Ukila zaidi ukajaza tumbo itabidi ujazo wa ziada utoke ama kwa kuharisha au kutapika mwili unataka kile kiasi kinachohitajika
 
Huku kwetu kuna namna ya kienyeji kusaidia watu waliokula chakula kingi mpaka kinawapa shida tumboni kiasi cha kutishia uhai wao. Ni hao wafakaniaji wa vyakula vingi wanavyokula kwa wakati mmoja wanashiba mpaka wanataka kufa. Huwa wanasaidiwa kwa kufungwa kamba miguuni na kuning'inizwa kichwa chini kisha unyoya wa kukuku mrefu huingizwa mdomoni kuelekea koromeoni na huchokonolewa. Wakichokonolewa wanatapika chakula kilichozidi na tumbo hukaa mkao wake wa kawaida, hapo wanakuwa wamepona na hatari ya kuvimbia kiasi cha kutishia kufakufa. Hiyo ni njia ya kienyeji kutapishwa kwa lazima baada ya kulakula vyakula vingi kwa pamoja bila nidhamu ya kula
 
Wengine hula milo miwili si kwa kupenda ni vile usawa umekaba
 
Huyu nae anapenda promo sana. [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kweli ukimwangalia Hana afya ama labda ni macho yangu. Lkn Hana afya Janabi
 
Try to imagine the use of sugar despite of those home stead uses sugar is more than that ingekua kama mnavyoeleza ni kama mtu akigusa sukari tu its boom kesho au keshokutwa tunazika lets use our little understanding kila kitu kina madhari kisipotumika kwa kiwango kinachotakiwa
 
Kweli ukimwangalia Hana afya ama labda ni macho yangu. Lkn Hana afya Janabi
Utapiamlo ama?
Badala ahangaike kutafuta dawa ya malaria yeye kakazana kutupa ushauri wa kula huyu vipi
Utafikiri mwalimu wa shule kumbe professor πŸ˜‘
 
Ndio mana amekonda....😜
Lakini tuvumiliane tu maana kwasasa nchi haina umeme, sukari wala dola..😒
Lakini nikifuata ishauri wa huyu baba, mwa J anaweza akaniua kitandani mbwa yule kwanza aliniambukiza uti grade one...🀨
Huyu ni wewe au nimekufananisha kaka mkubwa😁😁
 
Huyu mzee kuna vitu anatupotosha sana binafsi simtilii maanani tangu alipotoa kauli sukari si muhimu
Kusema ukweli sukari inanenepesha.nimejifanyia uchunguzi.

Kuna kipindi nilijaribu kwa miezi mitatu kuacha sugar nilipunguza zaidi ya kg 8
 
Matatizo tuliyonayo wabongo toka tunazaliwa hadi kufa ni diet tosha. Sasa ndiyo ule eti yai kwanza bei ya yai hapo nimeshapata dagaa mchele wa nyumba nzima yai lingine unga wa ugali fikiria tupo 5 zidisha 500 mara 2 mara 5 ni kama 5000. Hapo sijapata nguna na dagaa mchele kweli? tena nashiba vizuri .Tatizo watanzania wengi hali ya mifuko ni duni hatuwezi fata maisha ya wenzetu , mtu unaamaka asubuhi huna pesa hujui utaipata siku hiyo kazi ya kuitafuta pesa yenyewe ni mtihani mzito then unataka nianze panga muda wa kula na mayai sijui juice wakati chai tu ya bila sukari siwezi mudu. Siyo kama hatutaki kula vizuri au kwa wakati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…