Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Prof. Kabudi aieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania haijawahi kushindwa vita ya aina yoyote

Mkuu, nafikiri umesahau kwamba Profesa Kabudi atakuwa pia amefanya mawasiliano na Umoja House kutaka verifications ya kilichofanyika huko Brussels na masuala mengine

Kabla hajajitokeza tu "out of blue" kuongea, atakuwa amepitia kila kitu.

Huyu ni waziri wa sheria na katiba hivyo si kama sisi hapa wengine wakesha kueneza uongo mitandaoni.

Tatizo ni hao waandishi kutouliza anaposema "wahuni wachache" amaanisha nini?

Cha msingi serikali imeanza kujibu masuala haya khasa uzushi na upotoshaji unaofanywa mitandaoni na hichondicho watu kama mimi hapa nimekuwa nikisisitiza.

Sasa pia watoe majibu kwa vyombo vya habari vya kimataifa kwa kuanzia kupitia kwenye tovuti ya wizara.
 
Na Mmis sana Hayati Augustine Mahiga

Leo hii Katibu Mkuu wa Foreign ( kisima ch diplomasia) ni Bregadier Generali, Balozi nyingi sana tumepeleka Wanajeshi na vificho na vipenyo halafu Wana diplomasia waliobobea wamehamishiwa Halmashauri kwenda kuongeza 'Utendaji kazi'
 
Na Mmis sana Hayati Augustine Mahiga

Leo hii Katibu Mkuu wa Foreign ( kisima ch diplomasia) ni Bregadier Generali, Balozi nyingi sana tumepeleka Wanajeshi na vificho na vipenyo halafu Wana diplomasia waliobobea wamehamishiwa Halmashauri kwenda kuongeza 'Utendaji kazi'
Katibu mkuu jumatatu ilopita ametoa semina kwa wabunge Dodoma ya nguvu sana jamaa ameiva sana.
 
Namuunga mkono KABUDI SITAKI CHIEF MANGUNGO Tundu LISU na karl peters Amsterdam wanaotaka kugeuza HAO WABUNGE maruhuni wachache wa bunge la ulaya kugeuza bunge la ulaya kuwa Berlin CONFERENCE kuweka rehani madini yetu
 
Mkuu, nafikiri umesahau kwamba Profesa Kabudi atakuwa pia amefanya mawasiliano na Umoja House kutaka verifications ya kilichofanyika huko Brussels na masuala mengine
Hivi unaweza kuhoji wanacho ongea Wabunge wa EU? Mfano, Mbunge Msukuma au Kibajaji wakisema kuna mabeberu wa EU, unategemea Umoja House watahangaika nao.
Umoja House watahangaika na kauli ya Serikali Bungeni ambayo ni kauli rasmi. Je kuna kauli ya Bunge la EU?
Kabla hajajitokeza tu "out of blue" kuongea, atakuwa amepitia kila kitu.
Amepitia nini? Wabunge wakionge anapitia nini. Kama ni hivyo kila siku atafuatilia kauli za mabunge ya Dunia basi
Huyu ni waziri wa sheria na katiba hivyo si kama sisi hapa wengine wakesha kueneza uongo mitandaoni.
Si kweli , huyu alikuwa waziri wa katiba na sheria siku hizi ni wa mambo ya nje, huna habari!

Ndiyo maana tunasema kuna ku-panic. Ukifuatilia kauli yake anasema 'Tanzania ipo tayari kukaa mezani'
Hata hivyo kuna hoja mbili haziguswi, haki za binadamu na Bilioni 27 Euro ambazo ni pesa za EU
Tatizo ni hao waandishi kutouliza anaposema "wahuni wachache" amaanisha nini?
Si umesema ni waziri, sasa unashangaa nini?
 
Nilitaka kumaanisha yeye anafahamu sheria si amesomea na kuja kuwa mwalimu?

All in all, yeye ameongea na kama EU watajibu basi twangojea hio.

Kama hao wahuni wachache wataendelea kuongea huko mitandani pia tuvute subira.
 
Watu wanauana kila kukicha Duniani sio Tanzania tu... na hili mnasababisha wenyewe wapiga mayowe....mnainfluence vijana wasio na hili wala lile na kuwaaminisha yasiyokuwepo.....

Kila serikali Duniani ina dosari zake.....ukiwa na kundi lisilofikiria lkapata viongozi wahemkaji tarajia vifo.

Hoja ya kura ni mfu....ninachojua mimi hata kura ungehesabu wewe JPM angeshinda awamu hii.

Wanahamasisha watu afu wao wametulia nyuma ya Keyboard
 
Wanahamasisha watu afu wao wametulia nyuma ya Keyboard
Cha ajabu....mimi ninachojua kama kweli kinachoandikwa humu mitandaoni ndicho watanzania wanachopitia.

Hata hakuna haja ya kuwaambia andamana...wataingia barabarani wenyewe.

Na hawa wenzetu weupe....wanawasoma mitandaoni wanajua ndiyo hali inayoendelea Tanzania.
 
Unaweza jifariji kuwa vikwazo vitawahusu wengine ila ukae ukijua sisi walala hoi tukipigika vya kutosha nyie pia hamtakuwa salama. Tutawapigia kelele kila Kona, msipotusikiliza tutajua nyinyi ndo adui zetu namba one na huo ndo utakua anguko lenu.

Shetani katutega pabaya. Ukitenda hila na uovu jiandae kupokea matunda yake

Mitano tena itakua migumu
 
Our very own Comical Ali...
Shennx sana hili jamaa linaitwa ka-Bundi......ni bundi haswaaa...!!!
Ati WAHUNI WACHACHE.......!!!!Mweee!!!Bundi are u serious?
You must be joking!
One good question : KWANINI MMEKUBALI KUPOKEA MISAADA YA KUPAMBANA NA COVID-19 ILHALI MMESEMA TANZANIA HAKUNA CORONA BAADA YA MAOMBI YA SIKU 3 NA TAKWIMU HAKUNA??
Msiwafanye Watz na Jumuia za Kimataifa ni mazuzu. Ukweli wewe na Magufuli na CCM yenyu ndo mazuzu wakubwa!
 
Mkuu uchambuzi wako naona bado unaegemea tu kwenye utegemezi
Lini Africa itajitegemea yenyewe? Mbona akili zetu bado sana kiutegemezi?
In short Prof kasema tu ukweli, sisi ni taifa huru na ni hatutayumbishwa na kusitishiwa misaada

Wewe ndiye tatizo kabisa na hujaelewa zaidi.

Hivi hujiulizi ni sababu gani imemfanya waziri huyu wa mambo ya nje apanic kiasi hiki hata kukosa busara ya kutumia lugha ya kidiplomasia kutoa ujumbe wake?

Kwanza, hebu tuambie haya yanayoitwa "majibu ya Prof. Kabudi kwa mabeberu" anamjibu nani..?

Hivi hawa EU ama nchi yoyote mwanachama wa EU wametoa tamko lolote la kuchukua hatua fulani fulani kwa Tanzania kiwemo kukata misaada ya kibajeti?

Jibu obviously ni HAPANA, HAKUNA...!!

Ndiyo, HAKUNA. Kilichofanyika ni wabunge kuibua mjadala tu kuhusu Tanzania na kamwe hilo halijawa azimio la bunge zima la EU kwa ajili ya serikali za nchi wanachama wa EU kualifanyia kazi...

Kama ndivyo, hebu tujiulize kuna tatizo gani serikalini kwa sasa?

Kwanini Waziri anatoka na kutumia maneno makali na ya kejeli yasiyo ya kidiplomasia kwa EU huku akiwa hana taarifa sahihi na bila kufuata utaratibu wa kidiplomasia..?

Hii kamati imeibua jambo moja tu. Msaada wa €27,000,000 uliotolewa kwa Tanzania kusaidia kupambana na COVID 19...

Ni wazi kuwa wana taarifa kuwa hazijatumika kwa kusudi lake. Wanahitaji maelezo ya jinsi zilivyotumika na wakati huohuo wanawahoji watendaji wao wawape vigezo vilivyotumika kuipa Tanzania fedha hizo kwa sbb ni kama haikidhi vigezo hivyo...

Sasa badala ya serikali kutoa maelezo, inamtuma Prof. Kabudi kuchafua hali ya hewa zaidi ya hii iliyokwisha kuchafuka...!!

Kama Nyerere alirudisha fedha za Waingereza na Ujerumani miaka ile, basi Magufuli naye arudishe mwaka huu tuone...!!
 
Vita ya umasikini[emoji23] sasa kwanini tunasaidiwa mpaka leo. Tatizo kama hatufanyi vitu kama wataalam wetu kufanya tafiti za madawa au technologia tutabaki kuwa tegemezi.
 
Kukaa kimya ni kama wanakubali huo upuuzi unaongelewa, ni vyema kuwajibu mapema kila mtu aelewe ukweli, kuendelea kuacha upande mmoja tu kuongea ni ujinga, acha serikali na wao kujibu mashambulizi na kutoa ufafanuzi, kwa nini wapenzi wa CDM hawafurahii kuona serikali ikitoa ufafanuzi na kujibu upotoshaji?
 
Hivi waliopeleka marekebisho ya sheria ya takwimu baada ya mbinyo wa World Bank ni kina nani?

Halafu kwani misaada wanatulazimsha kupokea, si wawaambie hatuitaki tena ili tuwe nchi huru kweli
 
Back
Top Bottom