Prof. Kabudi ataka Elimu ya Biblia itolewe shuleni kuanzia Chekechea hadi Sekondari na Biblia zigawiwe Bure ili kulinda Maadili

Prof. Kabudi ataka Elimu ya Biblia itolewe shuleni kuanzia Chekechea hadi Sekondari na Biblia zigawiwe Bure ili kulinda Maadili

Waziri wa Katiba na Sheria Prof Kabudi ametaka Elimu ya Biblia iingizwe Kwenye mitaala ya kuanzia Chekechea hadi Sekondari

Prof Kabudi amesema zitengwe fedha za kuchapisha Biblia Ili zigawiwe Bure Kwa wanafunzi Katika Jitihada za kulinda Maadili yanayoporomoka

Kabudi amesema hayo kwenye Ibadan ya kumuweka wakfu askofu Mbwaga wa Kanisa la Baptist

Source Mwananchi

Mlale Unono

Kanisa Moja Takatifu La Mitume 🌹
Unaacha kutoa elimu ya fedha unatoa elimu ya takataka?

Mnataka pesa mmiliki pekeenu watoto wetu waje kurithi makoti yetu?
 
mimi nimesoma hivyo hivyo, tangu kidato cha kwanza hadi cha nne...bible knowledge lazima kusoma kwa kila mtu alafu kila baada ya miezi sita tulikuwa tunagawiwa biblia mpya..ya kiswahili na kiingereza kila mtu. Full upendo yaani
Hahhaha nilikuwa nazivutia bangi kipindi hicho nipo shule moja hivi tukishuka jumamosi bondeni misokoto ya kutosha
 
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Kabudi ametaka Elimu ya Biblia iingizwe Kwenye mitaala ya kuanzia Chekechea hadi Sekondari

Prof Kabudi amesema zitengwe fedha za kuchapisha Biblia Ili zigawiwe Bure Kwa wanafunzi Katika Jitihada za kulinda Maadili yanayoporomoka

Kabudi amesema hayo kwenye Ibadan ya kumuweka wakfu askofu Mbwaga wa Kanisa la Baptist

Source Mwananchi

Mlale Unono

Kanisa Moja Takatifu La Mitume 🌹
UPorofesa unakaribia kuisha muda wake wa matumizi! Mwenye kunielewa anielewe!!
 
Bodi ya Elimu ya jimbo la Texas Marekani imepitisha muswada wa kufundisha Biblia kwenye shule za Serikali. Mpango huu wa kuingiza mafundisho ya Kikristu kwenye mitaala ya elimu ni wa chama cha Republicans cha Rais Donald Trump.

----
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amewataka viongozi wa dini ya Kikristo nchini, kuungana na kuanzisha programu maalumu ya mitaalaa ya elimu ya mafundisho ya Biblia kuanzia elimu ya awali, msingi na sekondari kwa lengo la kulinda maadili kwa vijana.

Amesema kuanzishwa kwa masomo hayo kuende sambamba na kutenga fedha kwa ajili ya uchapaji na ugawaji wa Biblia bure, zenye mtaalaa mmoja wa kufundisha baina ya dhehebu moja na jingine na kutoa ajira kwa walimu wa dini nchini.

Profesa Kabudi ametoa wito huo leo Jumamosi, Novemba 23, 2024 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu mteule wa Kanisa Baptisi Kanda ya Kusini Magharibi, Mchungaji Sylvester Mbwaga.

“Nasema hivyo kwa sababu dunia imebadilika kutokana na kukua kwa teknolojia za utandawazi, hali inayosababisha watu kufika mbali kwa kuamini Mungu hayupo jambo ambalo sio sahihi,” amesema.

Profesa Kabudi amesema lengo la kusisitiza uanzishwaji wa mitalaa ya elimu ya Biblia shuleni ni kuokoa vijana kuporomoka kimaadili na kuingia kwenye upepo mbaya.

Chanzo: Mwananchi
 
Si Kila profesa ni profesa, wengine ni profesa kabudi.

Huyu ni Mtu anayezungumza hayo pasipo kufahamu/kutambua au kuwa na uelewa wa Kina wa Historia ya Homo Sapiens, Religion/dini, Comparative religion, Ethics (philo+S) na Technology & Uchumii (From thirds world country to first world country).

Anafanya ni Mkumbuke Padre Mmoja katika somo la Religion & bible knowledge Shule ya Upili.. Miaka ya nyuma huko.

Na maswalii kadha wa kadhaa,

1.kuna mgawanyo wa vitabu katika agano la Kale, sehemu kuu nne nazo ni:-
A) vitabu vya Sheria.
B) Vitabu vya hekima,
C) vitabu vya historia..
D) vitabu vya Manabii.


2. Eleza namna kiebrania kinavyoandikwa..

3.Types of sinners,

A)Heart hardened sinner's (Wadhambi wenye mioyo migumu)

B)Self righteous sinners.

C) Complacent sinners.

D) Repentant sinners .

4.let us make man in our own image after our likeness (Gen1:26).
A) identify the speaker.......
B) Give One reason as to Why the speaker used the prural form...

Kabudi kazingumzia pia Ethics,

Ethics/Morals/Maadili ambapo Dini/Religion imejimilikisha kwa Asimilia Mia, ambacho si kitu sahihi/Si fact's, Si kwelii,.

Wanasiasa Wengi hutumia dini kutimiza malengo Yao,

Katika poor country, kama Tanzania, Dini imekuwa faraja na kimbilio kwa Matatizo mengi ya raia, ambayo yangeweza kumalizwa na Uwepo wa uchumii imara/Bora na Elimu ya kiwango Bora.

Finally, God/god's & money na Nations Great great inventions za homo sapiens..
Ni matengenezo/Man made za Human being.
 
Inakuwaje Japan, Biblia na Quran hazipo kama Tanzania lkn bado Wana maadili! Kabudi Aache kupiga siasa
 
ni muhimu mno elimu hiyo ikatolewa huko huko makanisani kwa wenye imani hiyo pamoja na biblia bure, nadhani itapendeza zaidi na kuepusha usumbufu kwa wasio husika 🐒
Jukumu la kufundisha maadili ni wazazi hayo mambo mengine mbwembwe tu

Ova
 
Serikali haina dini ila raia wana dini zao, ili mradi wasivunje sheria. Sasa kila mtu atakuja na kitabu chake cha imani, atasambaza mashuleni ili imani yake ienee, huu ni uuuungwana?
 
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Kabudi ametaka Elimu ya Biblia iingizwe Kwenye mitaala ya kuanzia Chekechea hadi Sekondari

Prof Kabudi amesema zitengwe fedha za kuchapisha Biblia Ili zigawiwe Bure Kwa wanafunzi Katika Jitihada za kulinda Maadili yanayoporomoka

Kabudi amesema hayo kwenye Ibadan ya kumuweka wakfu askofu Mbwaga wa Kanisa la Baptist

Source Mwananchi

Mlale Unono

Kanisa Moja Takatifu La Mitume 🌹
Nilidhani atatoa hoja ya kufutwa MOU yeye kama waziri wa sheria
 
wangeanzia magogoni kwa binti kiziwi,we huwez kusema kifo ni kifo tu kama umemeza mhogo mkavu...
 
Back
Top Bottom