Hujalipa bado oooh,ni wewe na familia yako kwako ada na kodi zinakupeleka puta.Hizo Habari ndio mnazipenda badala ya kushughulika na Ada na kodi za January
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hujalipa bado oooh,ni wewe na familia yako kwako ada na kodi zinakupeleka puta.Hizo Habari ndio mnazipenda badala ya kushughulika na Ada na kodi za January
Dawa ya DENI ni KULIPA.Mabeberu na michezo yao ya kishetani
Wamemshindwa kwenye karatasi sasa wanavizia mali zetu
Rais Magufuli funga Ubalozi wa Canada Ndani ya saa 72 ili watoe Maelezo
Kwanini hakukamata Dreamliner USA? Hii ni ndege ya pili inakamatwa Canada.Nasikitika jambo moja tu: waziri wanaonekana kuinyoshea kidole serikali ya Canada! Methinks this is unfair kwa mtu mwenye upeo tena Profesa wa sheria. Hili ni suala la mtu binafsi anajaribu kutumia sheria kupata haki. I stand to be corrected but I think this has nothing to do with government of Canada.
Hawezi huko ni maji marefu, hakuna wa kuogopa mimacho yake kule. Pili yeye ni mnobezi kwenye ualimu wa sheria na siyo Mahakamani.Kwa kutambua kua Prof. Kabuni ni mbobezi na nguli katika sheria, kwanini aogope kushindana na wanasheria wenza katika ulingo wa kimahakama.
Acheni sheria ichukue mkondo wake na hii ndo maana ya kuajiri wanasheria serikalini ili walinde maslahi mapana ya serikali na nchi kwa Ujumla.
hapo utakuwaunafuraha ajabu moyoni mwako???//..😆😆😆😆
Aiseee malala unachekeshaga sana.😆😆😆😆
Nani alikwambia Masogange alikamatwa na gunia la sembe?Kama mliwahonga majaji wa south mkashinda(rejea kesi ya marehemu masogange aliyekamatwa na gunia la sembe south africa na akaachiwa huru), Majaji wa Canada hawaongeki ,jiandaeni kulipa deni.
Wewe vipi hii habari haijakufurahisha?!Aiseee malala unachekeshaga sana.
Kule Afrika Kusini lazima Cyril Ramaphosa alitia nenoCanada hakuna Rushwa kama South Africa
Wewe tu ndiyo huna habari na issue ya Masogange. Kaa kimya usome ujifunze JF siyo lazima uandikeNani alikwambia Masogange alikamatwa na gunia la sembe?
Tuachane nao hao wakanada twende nchi zingine na hizo mbinu zinafanywa na kanada au tuvunje uhusiano nao na tumrudishe baloziWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi Kabudi amesema ndege ya Tanzania Bombardier Q400 iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa nchini Canada na kesi ipo Mahakamani
======
NDEGE NYINGINE YA TANZANIA YAKAMATWA CANADA
- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema ndege aina ya Bombardier Q400 imekamatwa
- Ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa na kesi ipo Mahakamani
#JFLeo
"Mhe. Rais ndege yetu aina ya Bombadier ambayo ilipaswa ifike Tanzania kutokea Canada imekamatwa na mtu yule yule ambaye aliikamata ndege yetu kule Afrika ya Kusini." - Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje.
===
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 imakamatwa nchini Canada.
Amesema aliyesababisha Bombardier kukamatwa ni Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini ambaye alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini akidai fidia ya dola 33 milioni.
Kesi hiyo ilisababisha Mahakama hiyo kuizuia ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kuondoka nchini humo Agosti, 2019.
Steyn, anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980. Hata hivyo, Septemba 3, 2019 mahakama hiyo iliamuru ndege hiyo iliyokuwa imezuiwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo kuachiwa baada ya Serikali kushinda kesi bila kutoa fedha yoyote.
Akizungumza leo Jumamosi Novemba 23, 2019 mjini Dodoma katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi, Profesa Kabudi amesema, “ndege imekamatwa na kesi ipo mahakamani. Aliyesababisha ni yuleyule (Steyn) aliyesababisha ndege yetu kuzuiwa Afrika Kusini.”
Profesa Kabudi amesema kuendelea kwa vitendo hivyo ni hujuma za mabeberu wasiofurahishwa na maendeleo nchini.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyewaapisha mabalozi hao, Profesa Kabudi amesema, “tulikwenda mahakamani tukamshinda (Afrika Kusini) akakata rufaa na wiki iliyopita tukamshinda tena, huyohuyo sasa amekimbilia Canada amekamata ndege ya Bombardier Q400 ambayo ilikuwa ifike nchini.”
“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”
Amesema Balozi wa Tanzania nchini Canada aliitwa nchini na kuelezwa jinsi nchi isivyofurahishwa na kukamatwa kwa ndege zake kila zinapokaribia kuja kuondoka nchini humo.
“Nimemwambia sio tu kwamba tunasikitika bali tunakasirishwa, na tunafikiri mheshimiwa rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu kama hivyo sio wao peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kununua ndege Canada, hata Brazil wanatengeneza ndege,” amesema Profesa Kabudi.
Amesema wameandaliwa wanasheria kwenda Canada kuipigania ndege hiyo.
Kushikiliwa kwa ndege hiyo kunarejesha kumbukumbu ya ndege nyingine ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017 kutokana na madai ya Sh87.3 bilioni zilizokuwa zikidaiwa na kampuni ya kikandarasi.
Mabalozi walioapishwa katika hafla hiyo ni Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati (Misri), Mohamed Abdallah Mtonga (Abu Dhabi), Jestas Abouk Nyamanga (Ubelgiji), Ali Jabir Mwadini (Saudi Arabia) na Dk Jilly Elibariki (Burundi).
Chanzo: Mwananchi
Mwehu wewe alichokamatwa nacho Masogange sio unga.Wewe tu ndiyo huna habari na issue ya Masogange. Kaa kimya usome ujifunze JF siyo lazima uandike
Hahahaha, Rafiki twende tukaongeze speed ya ulipaji kodi, tumlipe mkulima hela zakeOooh makubwa
Acha ramliNa zitakamatwa nyingi tu.
Hapo ndo shortcut inakuwa long cut.Cha ajabu pesa inayotumika kupambana kukwepa deni ni kubwa kuliko kulipa deni
Ripoti ya awali kutoka Afrika Kusini inasema wanawake wawili wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa OR Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.Nani alikwambia Masogange alikamatwa na gunia la sembe?
Ainisha maslahi ya Canada katika mradi wowote unaoujuaUnadhani na wao hawana maslahi yao ?wanakupa tu bure ?
Wewe umetusaliti...tupo tuna andamana apa ubalozi wa Canada kudai ndege yetu...Kama vipi waondokeMabeberu na michezo yao ya kishetani
Wamemshindwa kwenye karatasi sasa wanavizia mali zetu
Rais Magufuli funga Ubalozi wa Canada Ndani ya saa 72 ili watoe Maelezo