Prof. Kabudi: Ndege ya Tanzania, Bombardier Q400 imekamatwa Canada na kesi ipo Mahakamani

Huu umbeya sasa, unajishushia hadhi yako kama kiongozi wa JF, yaani walipwe watu pesa waandamane?
ukiwekewa ushahidi wa vijana kulipwa ili wakapige mayowe kwenye ubalozi wa S.Africa utakuwa tayari kujiondoa jf ?
 
Dawa ya deni kulipa
 
Kuandamana wana haki. Wapeleke taarifa police, kisha police watautaarifu ubalozi kuhusu protesters na dhumuni Lao, halafu watafanya maandamano yao. Kwenda ubalozini bila kuutaarifu ubalozi itachukuliwa ni uvamizi, na mtambue hawa si kama South Africa waliowaonea aibu. Vienna convention ya diplomatic relations itadeal na nyinyi labda mjitoe UN, vinginevyo mjiandae kushughulikiwa.
 
Msamiati wa "hujuma za mabeberu" umepamba moto siku za karibuni kuvuta "hisia za kizalendo".

Hao mabeberu wanaodaiwa kuhujumu Tanzania wameibuka leo? "Political scientists" watakwambia kuwa nchi za Bara la Afrika zilizokuwa zinatawaliwa na wakoloni zina uhuru wa bendera. Kuna Ukoloni Mamboleo ambako, pamoja na mambo mengine, ni kutawaliwa kitamaduni na kiuchumi, na kunyonywa rasilimali (neocolonialism). Hali hiyo itapungua tu kwa nchi kujitosheleza katika baadhi ya mambo.

Ni wakati wa wanasheria kusafiri nje ya nchi kwa gharama kubwa kwenda kutetea taifa. Maswali ya kutaka uelewa: Tanzania kama taifa haiweki kumbukumbu ya madai na madeni yetu ili ulipaji wake uwekewe mikakati na ufuatiliwe?

Serikali izifanyie kazi kumbukumbu za tunavyodai na tunavyodaiwa kama zipo. Iache kulialia kutafuta huruma. Kesi ya madai iliyofunguliwa Afrika Kusini ilitawaliwa na ilimalizwa kisiasa.

Ni wakati wa kutegesha masikio yetu Canada kusikia hatma ya Bombardier Q 400.
 
Tanzania maandamano yamekatazwa
 
Sijui kwa nini, yaani naona sawa tu haya madege kukamatwa! Ni kipaumbele cha mtu mmoja, bunge lenyewe pengine halipitishi hiyo baketi ya kununua madege! Mkulima asipangiwe cha kufanya......
Yes, kule kuminya nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi ni kwaajili ya kununua ndege ambazo hazikupangiwa bajeti.
 
Hotuba yenyewe ya Prof kabudi imejaa tamathali za semi nyiiingi eti ni njama za mabeberu wakishirikiana na baadhi ya viongozi..KWELI???Yaani prof mzima wa sheria unatunga uongo wa kumtuliza mh.Rais?yaani anataka tuamini kuzuiwa kwa ndege ni suala la canada na Tz?halafu bado tena akasema kuwa ni mtu yule yule tulio mshinda South Africa ndio ameenda tena Canada,Yaani prof wa sheria na sijui LLB za udzm nimemvua vyeo sema tu anafanya kazi ili muheshimiwa asione kama alibugi step kumuweka pale.
 
1⅕ Hawa wanyama pori hawatakuelewa mzalendo wetu. Moyoni mwao ni wafu.
Kwa maneno mengine unaweza sema hiyo ni mizoga inayotembea na isiyoweza kuwaza. Ni mazombi hayo.

Thinking capacity yao equetion yake is equal to ZERO. It is a constant funktion:
Y = 0, while X => infinity.
No oscillation on the Oscilloscope.

Maisha yao, yale ya wazazi wao, mabibi na mababu zao, watoto na ndugu zao wengine hayana maana kwao. Maisha ya mabeberu kwao ndiyo furaha.
 
ukiwekewa ushahidi wa vijana kulipwa ili wakapige mayowe kwenye ubalozi wa S.Africa utakuwa tayari kujiondoa jf ?
Sasa huo ushahid umeuficha uvunguni ili mimi nijiondoe JF? Watanzania wengine mnafurahisha sana. Wacha majungu weka ushahidi.
 
Reactions: Oii
.
Napenda kuona viongozi wa upinzani na wa chama tawala wakiraruana kwa hoja nzito kwa maendeleo ya watanzania tupingane, tukosoane tusemane kwa mambo yetu ya ndani na lengo likiwa moja tu kutaka Tanzania mpya ya maziwa na asali.
Wapinzani wanararuliwa risasi na mapanga, wamejaa magerezani. Umoja na uzalendo huo utatoka wapi mkuu?
 
Very true
 
Hotuba ya Palamagamba Kabudi ni kama vile anaongea na watoto wadogo, kugombeza na kuongea kwa ukali hakusaidii kurekebisha na kufundisha.

Inaonekana huyo Palamagamba anajaribu kujipendekeza kwa Rais ili asitukanwe mpumbavu tena na Magufuli.

Ni hotuba ya hovyo kabisa, kama zile hotuba za bwana yule. Bwana Magamba kasema ndege imeshikwa na yule yule aliyeshika ikiwa South Africa.

Formula ni rahisi sana. Bwana Steyn anawadai fedha kwa mali zake zilizoibwa na serikali ya Nyerere, tunaojua na tuliokuwepo wakati huo tuliona na tunaelewa utaifishaji wa ovyo wa mali ya watu binafsi, kulikuwa na madhara makubwa ya utaifishaji wa mali za watu, wengi wa watu ambao mali zao walizopata kihalali walijiua kama shock waliyopata baada ya kufilisiwa.

Hizo mali zilizofilisiwa zimeisaidia vipi serikali ya Tanzania? Wawekezaji wengi wameogopa kuja, mali nyingine zilizotaifishwa zilirithishwa kwa viongozi wa serikali kitu ambacho ni wizi mtupu.

Kuhusu suala la Steyn, Huyu bwana alikopa fedha Bank mwaka 1977 akanunua mashamba makubwa, ndege nne au sita, na mamia ya matrekta na mashine zingine za kilimo, mifugo na majengo, wafanyakazi wengi waliajiriwa.

Hivyo Nyerere alivyomnyang'anya Bw. Steyn mashamba yake aliyomiliki kihalali watu wengi walipoteza ajira.

Steyn baadaye walikubaliana na serikali na mahakama kuu ya Tanzania ikaamuru alipwe kiasi kilichopangwa, alilipwa kidogo mwishoni mwa mwaka 1983 na akaendelea kulipwa wakati wa Mwinyi na Kikwete.

Sasa iweje serikali ya Magufuli ikatae kumlipa pesa ambayo ni malipo halali?

Palamagamba Kabudi anafahamu kabisa kuwa hilo deni ni halali na Bw. Steyn siyo tapeli kama unavyodai.

Kwa ushauri wangu bwana Palamagamba Kabudi usIipende kujipendekeza ili kuuficha ukweli, ukweli uwe ukweli.

Mlipeni bwana Steyn fedha zake la sivyo ndege hizo hazitakuwa salama, zitakapoenda zitakamatwa tu.

Waziri Mkuu wa Canada alishawaambia yeye hawezi kuingilia mahakama, sio serikali ya Canada iliyokamata ndege ila ni amri ya mahakama hivyo serikali haina amri itakayokinzana na mahakama.

Mambo ya kuiamulia na kuingilia mahakama au bunge ni Tanzania tu na wala sio nchi nyingine. Nilifikiri Bw. Kabudi anafahamu hilo kwa sababu yeye anajua sheria kuliko bosi wake, lakini naona anamfurahisha mkubwa wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…