Prof. Kabudi: Ndege ya Tanzania, Bombardier Q400 imekamatwa Canada na kesi ipo Mahakamani

Prof. Kabudi: Ndege ya Tanzania, Bombardier Q400 imekamatwa Canada na kesi ipo Mahakamani

Huu umbeya sasa, unajishushia hadhi yako kama kiongozi wa JF, yaani walipwe watu pesa waandamane?
ukiwekewa ushahidi wa vijana kulipwa ili wakapige mayowe kwenye ubalozi wa S.Africa utakuwa tayari kujiondoa jf ?
 
Dawa ya deni kulipa
Kumbe, hapa stori kwa macho ya TheCitizen
"The story behind ATCL plane seizure in South Africa"

Kumbe aliahidiwa kufidiwa pesa yake tangu mwaka 2014 lakini hakupata chake.
Sijui kama ni kweli.
Ila kwa nini hawakumaliza deni?
Kama ni kweli - basi. Tusishangae.
 
,endelea kuuza Bia Kenya mwanaume mzima unahama Tanzania kwenda Kenya kuwa bar maid then unasema Tanzania watu wako wapumbavu wa wazazi wako wako hapa

State agent
Tanzania ni taifa la wapumbavu sijawahi kuona
Screenshot_2019-11-06-02-41-20.jpeg
 
Kuandamana wana haki. Wapeleke taarifa police, kisha police watautaarifu ubalozi kuhusu protesters na dhumuni Lao, halafu watafanya maandamano yao. Kwenda ubalozini bila kuutaarifu ubalozi itachukuliwa ni uvamizi, na mtambue hawa si kama South Africa waliowaonea aibu. Vienna convention ya diplomatic relations itadeal na nyinyi labda mjitoe UN, vinginevyo mjiandae kushughulikiwa.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi Kabudi amesema ndege ya Tanzania Bombardier Q400 iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa nchini Canada na kesi ipo Mahakamani

NDEGE NYINGINE YA TANZANIA YAKAMATWA CANADA

- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema ndege aina ya Bombardier Q400 imekamatwa

- Ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa na kesi ipo Mahakamani

"Mhe. Rais ndege yetu aina ya Bombadier ambayo ilipaswa ifike Tanzania kutokea Canada imekamatwa na mtu yule yule ambaye aliikamata ndege yetu kule Afrika ya Kusini." - Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje.

======

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 imakamatwa nchini Canada.

Amesema aliyesababisha Bombardier kukamatwa ni Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini ambaye alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini akidai fidia ya dola 33 milioni.

Kesi hiyo ilisababisha Mahakama hiyo kuizuia ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kuondoka nchini humo Agosti, 2019.

Steyn, anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980. Hata hivyo, Septemba 3, 2019 mahakama hiyo iliamuru ndege hiyo iliyokuwa imezuiwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo kuachiwa baada ya Serikali kushinda kesi bila kutoa fedha yoyote.

Akizungumza leo Jumamosi Novemba 23, 2019 mjini Dodoma katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi, Profesa Kabudi amesema, “ndege imekamatwa na kesi ipo mahakamani. Aliyesababisha ni yuleyule (Steyn) aliyesababisha ndege yetu kuzuiwa Afrika Kusini.”

Profesa Kabudi amesema kuendelea kwa vitendo hivyo ni hujuma za mabeberu wasiofurahishwa na maendeleo nchini.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyewaapisha mabalozi hao, Profesa Kabudi amesema, “tulikwenda mahakamani tukamshinda (Afrika Kusini) akakata rufaa na wiki iliyopita tukamshinda tena, huyohuyo sasa amekimbilia Canada amekamata ndege ya Bombardier Q400 ambayo ilikuwa ifike nchini.”

“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”
Amesema Balozi wa Tanzania nchini Canada aliitwa nchini na kuelezwa jinsi nchi isivyofurahishwa na kukamatwa kwa ndege zake kila zinapokaribia kuja kuondoka nchini humo.

“Nimemwambia sio tu kwamba tunasikitika bali tunakasirishwa, na tunafikiri mheshimiwa rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu kama hivyo sio wao peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kununua ndege Canada, hata Brazil wanatengeneza ndege,” amesema Profesa Kabudi.

Amesema wameandaliwa wanasheria kwenda Canada kuipigania ndege hiyo.

Kushikiliwa kwa ndege hiyo kunarejesha kumbukumbu ya ndege nyingine ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017 kutokana na madai ya Sh87.3 bilioni zilizokuwa zikidaiwa na kampuni ya kikandarasi.

Mabalozi walioapishwa katika hafla hiyo ni Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati (Misri), Mohamed Abdallah Mtonga (Abu Dhabi), Jestas Abouk Nyamanga (Ubelgiji), Ali Jabir Mwadini (Saudi Arabia) na Dk Jilly Elibariki (Burundi).



Chanzo: Mwananchi
Msamiati wa "hujuma za mabeberu" umepamba moto siku za karibuni kuvuta "hisia za kizalendo".

Hao mabeberu wanaodaiwa kuhujumu Tanzania wameibuka leo? "Political scientists" watakwambia kuwa nchi za Bara la Afrika zilizokuwa zinatawaliwa na wakoloni zina uhuru wa bendera. Kuna Ukoloni Mamboleo ambako, pamoja na mambo mengine, ni kutawaliwa kitamaduni na kiuchumi, na kunyonywa rasilimali (neocolonialism). Hali hiyo itapungua tu kwa nchi kujitosheleza katika baadhi ya mambo.

Ni wakati wa wanasheria kusafiri nje ya nchi kwa gharama kubwa kwenda kutetea taifa. Maswali ya kutaka uelewa: Tanzania kama taifa haiweki kumbukumbu ya madai na madeni yetu ili ulipaji wake uwekewe mikakati na ufuatiliwe?

Serikali izifanyie kazi kumbukumbu za tunavyodai na tunavyodaiwa kama zipo. Iache kulialia kutafuta huruma. Kesi ya madai iliyofunguliwa Afrika Kusini ilitawaliwa na ilimalizwa kisiasa.

Ni wakati wa kutegesha masikio yetu Canada kusikia hatma ya Bombardier Q 400.
 
Kuandamana wana haki. Wapeleke taarifa police, kisha police watautaarifu ubalozi kuhusu protesters na dhumuni Lao, halafu watafanya maandamano yao. Kwenda ubalozini bila kuwataarifu utachukuliwa ni uvamizi, na mtambue hawa si kama South Africa waliowaonea aibu. Vienna convention ya diplomatic relations itadeal na nyinyi labda mjitoe UN, vinginevyo mjiandae kushughulikiwa.
Tanzania maandamano yamekatazwa
 
Hotuba yenyewe ya Prof kabudi imejaa tamathali za semi nyiiingi eti ni njama za mabeberu wakishirikiana na baadhi ya viongozi..KWELI???Yaani prof mzima wa sheria unatunga uongo wa kumtuliza mh.Rais?yaani anataka tuamini kuzuiwa kwa ndege ni suala la canada na Tz?halafu bado tena akasema kuwa ni mtu yule yule tulio mshinda South Africa ndio ameenda tena Canada,Yaani prof wa sheria na sijui LLB za udzm nimemvua vyeo sema tu anafanya kazi ili muheshimiwa asione kama alibugi step kumuweka pale.
 
1⅕
Kweli wabongo wafadhilaka wapundaka acheni chuki linapokuja suala la utaifa ni lazima tuache tofauti zetu tuwe kitu kimoja ndio maana wazungu ni rahisi sana kututawala sababu wanajua visokorokwinyo ni wengi hata maandiko matakatifu yanasema it’s better to have hundreds enemy’s than having one fool brother ndio maana wakoloni ilikuwa rahisi kututawala
Hawa wanyama pori hawatakuelewa mzalendo wetu. Moyoni mwao ni wafu.
Kwa maneno mengine unaweza sema hiyo ni mizoga inayotembea na isiyoweza kuwaza. Ni mazombi hayo.

Thinking capacity yao equetion yake is equal to ZERO. It is a constant funktion:
Y = 0, while X => infinity.
No oscillation on the Oscilloscope.

Maisha yao, yale ya wazazi wao, mabibi na mababu zao, watoto na ndugu zao wengine hayana maana kwao. Maisha ya mabeberu kwao ndiyo furaha.
 
ukiwekewa ushahidi wa vijana kulipwa ili wakapige mayowe kwenye ubalozi wa S.Africa utakuwa tayari kujiondoa jf ?
Sasa huo ushahid umeuficha uvunguni ili mimi nijiondoe JF? Watanzania wengine mnafurahisha sana. Wacha majungu weka ushahidi.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
.
Napenda kuona viongozi wa upinzani na wa chama tawala wakiraruana kwa hoja nzito kwa maendeleo ya watanzania tupingane, tukosoane tusemane kwa mambo yetu ya ndani na lengo likiwa moja tu kutaka Tanzania mpya ya maziwa na asali.
Wapinzani wanararuliwa risasi na mapanga, wamejaa magerezani. Umoja na uzalendo huo utatoka wapi mkuu?
 
Napenda kuwaambia hawa mazulumati haki za watu hazipotei tawala upita lkn taifa halipiti udumu milele.Awamu zijazo zitakuja kulipa madeni yote yaliyosababishwa na awamu ya hasara.Watu wametunza vielelezo wote waliobomolewa nyumba zao,fukuzwa kazi,bambikwa uhujumu uchumi,taifishiwa mali zao,wariporwa hela na mali zao,nk hawa wanasubiri ipite awamu hii ya kibabe itaingia ya waungwana hapo ndipo serikali itakoburuzwa Sana mahakamani watu wakidai haki zao.Tunaliona awamu zijazo zitapata tabu sana kulipa madeni.Kama ambavo mkulima anapigania haki yake
Very true
 
Hotuba ya Palamagamba Kabudi ni kama vile anaongea na watoto wadogo, kugombeza na kuongea kwa ukali hakusaidii kurekebisha na kufundisha.

Inaonekana huyo Palamagamba anajaribu kujipendekeza kwa Rais ili asitukanwe mpumbavu tena na Magufuli.

Ni hotuba ya hovyo kabisa, kama zile hotuba za bwana yule. Bwana Magamba kasema ndege imeshikwa na yule yule aliyeshika ikiwa South Africa.

Formula ni rahisi sana. Bwana Steyn anawadai fedha kwa mali zake zilizoibwa na serikali ya Nyerere, tunaojua na tuliokuwepo wakati huo tuliona na tunaelewa utaifishaji wa ovyo wa mali ya watu binafsi, kulikuwa na madhara makubwa ya utaifishaji wa mali za watu, wengi wa watu ambao mali zao walizopata kihalali walijiua kama shock waliyopata baada ya kufilisiwa.

Hizo mali zilizofilisiwa zimeisaidia vipi serikali ya Tanzania? Wawekezaji wengi wameogopa kuja, mali nyingine zilizotaifishwa zilirithishwa kwa viongozi wa serikali kitu ambacho ni wizi mtupu.

Kuhusu suala la Steyn, Huyu bwana alikopa fedha Bank mwaka 1977 akanunua mashamba makubwa, ndege nne au sita, na mamia ya matrekta na mashine zingine za kilimo, mifugo na majengo, wafanyakazi wengi waliajiriwa.

Hivyo Nyerere alivyomnyang'anya Bw. Steyn mashamba yake aliyomiliki kihalali watu wengi walipoteza ajira.

Steyn baadaye walikubaliana na serikali na mahakama kuu ya Tanzania ikaamuru alipwe kiasi kilichopangwa, alilipwa kidogo mwishoni mwa mwaka 1983 na akaendelea kulipwa wakati wa Mwinyi na Kikwete.

Sasa iweje serikali ya Magufuli ikatae kumlipa pesa ambayo ni malipo halali?

Palamagamba Kabudi anafahamu kabisa kuwa hilo deni ni halali na Bw. Steyn siyo tapeli kama unavyodai.

Kwa ushauri wangu bwana Palamagamba Kabudi usIipende kujipendekeza ili kuuficha ukweli, ukweli uwe ukweli.

Mlipeni bwana Steyn fedha zake la sivyo ndege hizo hazitakuwa salama, zitakapoenda zitakamatwa tu.

Waziri Mkuu wa Canada alishawaambia yeye hawezi kuingilia mahakama, sio serikali ya Canada iliyokamata ndege ila ni amri ya mahakama hivyo serikali haina amri itakayokinzana na mahakama.

Mambo ya kuiamulia na kuingilia mahakama au bunge ni Tanzania tu na wala sio nchi nyingine. Nilifikiri Bw. Kabudi anafahamu hilo kwa sababu yeye anajua sheria kuliko bosi wake, lakini naona anamfurahisha mkubwa wake.
 
Back
Top Bottom