TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
Tutasimama kwa "miguu yetu". Tumeishaamua kupata tunacho kitaka kama nchi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Halikushinda jopo la wanasheria, pale ilitembea siasa tu. Joburg tulisaidiwa tu na Cyril Ramaphosa, sikuona argument toka kwenye jopo letu ya kushawishi kisheria ku turn down madai ya mkulimaBado nina imani na jopo letu la mawakili, Natumai watashinda hata hili kwani sio mara yao ya kwanza kushinda kesi wakiwa nje ya nchi yetu [emoji123]
Mkulima effect au kitu gani tena?
Haya mambo ya ndege zetu kukamatwa sasa yametuchosha, vipi kuhusu usalama wa ndege zetu kutua London?.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi Kabudi amesema ndege ya Tanzania Bombardier Q400 iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa nchini Canada na kesi ipo Mahakamani
NDEGE NYINGINE YA TANZANIA YAKAMATWA CANADA
- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema ndege aina ya Bombardier Q400 imekamatwa
- Ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni imekamatwa na kesi ipo Mahakamani
"Mhe. Rais ndege yetu aina ya Bombadier ambayo ilipaswa ifike Tanzania kutokea Canada imekamatwa na mtu yule yule ambaye aliikamata ndege yetu kule Afrika ya Kusini." - Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje.
======
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 imakamatwa nchini Canada.
Amesema aliyesababisha Bombardier kukamatwa ni Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini ambaye alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini akidai fidia ya dola 33 milioni.
Kesi hiyo ilisababisha Mahakama hiyo kuizuia ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kuondoka nchini humo Agosti, 2019.
Steyn, anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980. Hata hivyo, Septemba 3, 2019 mahakama hiyo iliamuru ndege hiyo iliyokuwa imezuiwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo kuachiwa baada ya Serikali kushinda kesi bila kutoa fedha yoyote.
Akizungumza leo Jumamosi Novemba 23, 2019 mjini Dodoma katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi, Profesa Kabudi amesema, “ndege imekamatwa na kesi ipo mahakamani. Aliyesababisha ni yuleyule (Steyn) aliyesababisha ndege yetu kuzuiwa Afrika Kusini.”
Profesa Kabudi amesema kuendelea kwa vitendo hivyo ni hujuma za mabeberu wasiofurahishwa na maendeleo nchini.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyewaapisha mabalozi hao, Profesa Kabudi amesema, “tulikwenda mahakamani tukamshinda (Afrika Kusini) akakata rufaa na wiki iliyopita tukamshinda tena, huyohuyo sasa amekimbilia Canada amekamata ndege ya Bombardier Q400 ambayo ilikuwa ifike nchini.”
“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”
Amesema Balozi wa Tanzania nchini Canada aliitwa nchini na kuelezwa jinsi nchi isivyofurahishwa na kukamatwa kwa ndege zake kila zinapokaribia kuja kuondoka nchini humo.
“Nimemwambia sio tu kwamba tunasikitika bali tunakasirishwa, na tunafikiri mheshimiwa rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu kama hivyo sio wao peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kununua ndege Canada, hata Brazil wanatengeneza ndege,” amesema Profesa Kabudi.
Amesema wameandaliwa wanasheria kwenda Canada kuipigania ndege hiyo.
Kushikiliwa kwa ndege hiyo kunarejesha kumbukumbu ya ndege nyingine ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017 kutokana na madai ya Sh87.3 bilioni zilizokuwa zikidaiwa na kampuni ya kikandarasi.
Chanzo: Mwananchi
“Jambo linalosikitisha ndege zilizokuwa zinatoka Marekani aina ya Dreamliner mbili hazikukamatwa zimefika lakini kila ndege inapotakiwa kuondoka Canada tunashangaa hao matapeli wanajuaje na ndege zinakamatwa.”
Anataka mhimili uluojichimbia uingilie katiHaya mambo ya ndege zetu kukamatwa sasa yametuchosha, vipi kuhusu usalama wa ndege zetu kutua London?.
Dawa ya deni siku zote ni kulipa, hili la kukamatwa ndege zetu kuna watu wanaliona kama ni jambo la ajabu, lakini kuna watu ndani ya serikali hii hii, walitoa angalizo mapema kabisa kuhusu madeni chechefu, lakini wale wa kujimwambafy wakajifanya miamba na kutia pamba masikioni.
Prof. Kabudi anailaumu Canada kuruhusu ndege zetu kukamatwa, hata zisingekatiwa Canada zingeruka wapi?, wakati watu wana amri halali ya attachment!.
P
“Nimemwambia sio tu kwamba tunasikitika bali tunakasirishwa, na tunafikiri mheshimiwa rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu kama hivyo sio wao peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kununua ndege Canada, hata Brazil wanatengeneza ndege,” amesema Profesa Kabudi.
Akiwa awamu NNE, akiwaikusema nchi hii aiwez kununua ndege Kwa sababu ya Madeni menu sana. Akiwa viburnum nchi ainaweza kununua ndege zaidi ya Tano. Majani ratio ni Madeni ya nchi na ATCLDigrii nne (4) nenda kaokoe jahazi View attachment 1269890
Unaandika utadhani umekalia kijina cha moto.Tundu Lisu ndio injini behind kukamatwa ndege kanada kupitia kampuni yake ya uwakili aliyoajiriwa.Yeye ndie technocrat wao wa kisheria wa kuikomoa serikali ya Tanzania wa kesi za wadai wa kimataifa wanaoidai Tanzania .Hana uzalendo mjinga mkubwa
"The pumpkin of the old homestead must not be uprooted"- Okot P' Bitek in "Song of Lawino"....is a country bumpkin.
Mwehu tu huyo Achana naye. Wanaacha Kupambana na kutatua Tatizo eti wanalikimbia tatizo.Jamaa unaijua miradi mingapi ambayo Canada wana mkono wao?
Punguza sauti mzee baba asisikie maana alivyo na hasira tusije tukawaimbia hao jamaa parapanda imelia bure!Au ukute wao ndo wanatengeneza hizi trip ili wapige mahela