Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza katika Mahojiano yaliyorushwa Julai 8, 2026 na M & S Podcast amesema;
"Chama kikubwa kama CCM hata nafasi ya kuwa mjumbe wa kuandika ilani, hilo ni jambo kubwa sana. Sasa mimi sikuwa tu mjumbe, Kitila Mkumbo nikawa mwenyekiti.
Kuwa na uwezo ni jambo moja lakini kupewa fursa ya kuonesha uwezo ni jambo jingine kabisa. Ndiyo maana, baada ya kumshukuru Mungu huwa namshukuru sana Mheshimiwa Samia. Kwa sababu, amenipa fursa ya kuonesha uwezo. Kwa sababu asingenipa fursa, ningeandika dira saa ngapi? Wala Watanzania wasingejua kama naweza nikaandika ilani. Kwa hiyo nimepata heshima kubwa sana."