Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Bi nafsi kuhuasu hili la madini JPM alifanya vizuri, maana alitetea mali za wa Tanganyika ilhali yeye ni Rais wa Tanzania.
Tuwe wakweli, madini sio mali ya Tanzania/Muungano, bali ni mali ya Tanganyika. Kiuhalisia kuvunja mkataba wa Tanganyika ni hadi Tanganyika mwenyewe, ila kuusaini kumpa muekezaji tunasaini kwa niaba ya wananchi wa Tanganyika.
Kwani serekali haina pesa ya kununua karasha na kuchimba madini yenyewe? Kama uwezo upo wa kifedha kwanini haifanyi?
Mali isiyo ya muungano, ki mataifa huiuzi wewe raisi wa muungano bila makubaliano ya wewe na mwenye mali, utaishia kuuza kwa mwekezaji akupe kesh mkononi. Vipi utamlaumu raisi wa muungano kwa jambo ambalo sio la muungano? TUWE WAKWELI.
Wa Zenji tunawaona wajinga wakidai kero za muungano ziishe na tunawaita wabishi, ilhali wanatutetea.
Ki mataifa wanajua fika kuwa kuna mali za Tanganyika mbali, mali za Zanzibar mbali na Muungano/Tanzania mbali.
Raisi wa Muungano anahisika na mambo ya Muungano, hayo mengine ni sio yake, ila kwa 7bu ukubwa ni jalala sawa na tumtupie tu.
 
Ni Ni kweli, huu ushabiki usianze kuuona leo tu maana ulianza pale wataalam wa sheria walipotahadharisha kwa nia njema lakini mkawageuza kuwa wasaliti na kuwachafua ktk taifa,

Kwa sasa hapa siyo ushabiki bali tunawakumbusha kuwa mliwachafua watu kwa ushujaa wa kijinga na leo hapa jf mliyemchafua asafishike kwa ukweli wake na nia yake njema kwa taifa vilivyomgharimu maisha hata kunusurika kifo.

Kuhusu mikataba, ni kweli ilikuwa na matatizo ya mikataba kabla ya Magu ambayo tayari maamuzi ya kesi yalikuwa yalishatolewa, alichofanya Magu ni kukiuka hata hayo maamuzi ya mahakama hapa yeye pia ni mhusika.
 
Conspiracy theory ni ile unaambia rais amekufa kwa ugonjwa wa moyo au Covid. Mkuu tuna Uhuru wa habari na haki ya kuijeleza, kwa nini mnashindwa kuchanganya na za kwenu?
Yaani official cause of death ni conspiracy? Kwamba Rais Hana daktari, ndugu hawajui ukweli? Kwamba hakuwa na Pacemaker? Mbona kabla hajafariki sikusikia kelele kuwa kapewa sumu in fact wafuasi wake walikua wanakanusha haumwi Wala Hana tatizo. Cha kushangaza alipokufa ndio eti wanajua sana what happened kabla hajafa? With all due respect Please don't be part of such a band wagon.
Ni kweli lawama zipo kwa Mzungu kwa sababu sisi ni kama mwanamke Malaya, siku zote ushawishi wa mwanamme ndio humfanya mwanamke akatembea nje ya ndoa, japo mmewe pia anaweza kuwa na mapungufu yake lakini hampi haki ya kutembea nja ya ndoa.
Sio kweli, ni kutafuta scapegoat. Hata masuala ya ushoga tunalaumu wazungu tunasahau huko Zanzibar shida hiyo ipo miaka mingi lakini hakuna hatua zinachukuliwa. Same to ufisadi, ni matrillion yanatapanywa Kila mwaka na wizara zetu Cha kushangaza tukiibiwa kwenye madini tunasema ni mabeberu. Kwani huko kwingine MSD, Immigration, REA n.k Kuna mabeberu?? Tujifunze ku take responsibilities kwa matatizo yetu wenyewe.

Hivi unajua kitengo Cha kukagua hizo MNCs pale TRA kina watu 23 pekee? Alafu tukiibiwa tunadai ni mabeberu wakati sisi wenyewe hatuko serious na usimamizi.
 
Mpaka leo, Prof. Mruma anaeleza wazi kuwa anakereka sana akiikumbuka report ile, na kitendo cha baadhi ya watu kumwita profesa wa makinikia.
Huu ndio unafiki wa wasomi wetu, kwanini usijiuzulu?. Mbona huko nje wakipishana maamuzi mmoja anajiondoa kuliko kufanya kitu shingo upande ukijua repurcussions zake.
 
Tazama records ya Uuzaji madini kwa Tanzania. Mwaka 2019 ndio tuliuza dhahabu nyingi tani 55 kwa mwaka, leo tumeshuka hadi tani 43 ni sababu gani ikiwa sheria ni zile zile mbovu..
Mkuu wewe ni msomi, extractive industry kama ilivyo commodity market yoyote Ina incur volatility kwenye soko la kimataifa. Hata mauzo ya 2019 ni sababu ya soko kuwa na bei nzuri maana sisi shida yetu haikuwa uzalishaji Bali mgawanyo wa Mapato. Correlation is not causation....
 
Alipolipwa haraka haraka Symbio mabilioni nikajua tayari mchezo umeshaanza !! Wajanja kazini ! Na watu wanashabikia eti wanafikiri wanamkomoa Mwendazake 😅😅🙏🙏🙏
Hizo kesi mbona zimeanza tokea JPM yupo hai. Na Kabudi amewahi kataa ziongelea bungeni eti kuwa akitoa kauli yoyote atahatarisha hoja za serikali kwenye kesi zile.
 
Hahahah mkuu sijui nicheke kwanza. Unaona Sasa, Kitila anapokosoa maamuzi ya serikali unasema sababu amekosa ulaji na mambo kama hayo. Kwanini Mpina naye akipiga kelele usione na yeye ni sababu ya kuwa nje ya serikali?

NB: Najua utasema sio mtazamo wako ila unaongelea unafiki wa Kitila kusema wenzie wakati naye amefanya kile kile. Lakini nachosema ni kwamba basi Kitila na Mpina wawe treated equally kwamba wote ni wanafiki au wote ni wapambanaji. Otherwise na wewe utaingia kwenye kundi la unafiki unalomweka kitila.

Kitila Mkumbo
 
Symbion walishtaki sasa hivi wamerudi mtamboni kuzalisha Umeme na sii ajabu hata IPTL umerudi kinyemela..
Misinformation mkuu.... Madai yalikuwepo tokea mwendazake yupo hai. Ni kama tu yule mkulima wa Sauzi akilipwa sahivi mseme wameleta madai kisa wameona nchi ni shamba la Bibi!!! Ku enforce hukumu ya mahakama ndio kilichofanyika lakini kesi ilishaanza JPM akiwa Rais.
 

Kwahiyo Kitila naye huko bungeni anachoongea ni kuonyesha chuki yake dhidi ya Magufuli? Mbona mna uwezo mdogo wa kutetea hoja kwa kuchomekea neno mna chuki na Magufuli?!
 
Umeongea ukweli
 
..kuna makampuni yalishitaki wakati Magu yuko hai.

..umesahau suala hilo liliibukia Bungeni Prof.Kabudi akatoa majibu ya kejeli na kizandiki kwa wabunge wa upinzani
Kuna ajabu kushtakiwa ukipigania haki zako?
 
Wkt mhe Lissu anayasema hayo si mlimwita kibaraka wa wazungu?? Haya sasa yako wp
 
Kweli kabisa ! Mimi siku zote najitahidi kusimama kwenye ukweli !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…