Mayor Quimby
JF-Expert Member
- Mar 13, 2021
- 4,950
- 10,977
Unaweza kuleta ushahidi ata wa picha kuonyesha hiyo migodi ikiwa imeendelezwa ata kidogo.Mpango upi wakati wanadai cost za damages!! kilichobakia ni utekelezaji wa uhukumu sio kupewa leseni. Yaani miaka 5 Sasa hajachimba kitu Leo alainike kisa amerejeshwa nchini? Zile cost za miaka 5 atazifidia nani?
Haya makampuni kweli ni yakinyonyaji lakini ni CCM wenyewe mmeingia hii mikataba so mnapoivunja msitumie ujuaji maana hela za hongo mmekula alafu mnakiuka makubaliano mnategemea Nini?
Hizo leseni wengine walipata toka enzi za Mkapa na hakuna cha maana walichofanya.It doesn't matter, makubaliano ni makubaliano. Kama mlijua mkataba wa kihuni kwanini mslisign? Yaani mnakubaliana alafu baadae unakuja kukiuka makubaliano. Lazima ulipe fidia!!
Kuna procedure, ni sawa na mtu hajachukua Hela benki miaka 5 waka assume amekufa kumbe yupo nje ya nchi. Siku anarudi anataka Hela zake unadhani hatoshitaki?
Zimefutwa sababu ya regulations kubadilika na ndio kesi ya msingi Iko hapo. Kwanini ulete sheria mpya alafu unataka compliance kwa leseni ambazo umeshatoa na muda wa kuhuisha bado. Mlikubaliana say standards Fulani alafu baada ya miaka 3 uje na regulations mpya zenye standards mpya then una revoke licence kisa mtu Hana vigezo vipya!! Mahakamani utaanguka tu.
Na Uwezekano wa kuendelea kupigwa kama kawaida yetu upo palepale !!Tatizo la Watanzania huwa wanarukia sentesi moja na kuipa uzito mkubwa badala ya kusoma taarifa nzima inalenga kuzungumzia kitu gani.
Nina hakika Prof. Kitila kaeleweka vibaya kwa sababu, hoja yake hakuzungumzia kesi hizi zimetokana na makosa ya kuwanyang'anya liseni Wawekezaji bali hoja yake ni Ushauri uliotolewa wakati wa kusaini mikataba ya madini miaka ya nyuma na sasa.
Makosa haya ndio yalosababisha leo tuna kesi hizo 3 akilenga uwepo wa madini adimu kabisa ambayo Marekani walienda South katika mkutano wa madini na kueleza malengo yao. Hii ni tahadhali kwetu juu ya maamuzi na Ushauri atakao pewa rais.
Akatahadhalisha zaidi kuwa madini hayo tunayo na tuwe makini sana haswa washauri wa rais wamwelekeze vema na sii kwa Ushujaa wa kibabe tukatoka na ZERO! Mfano wa wasomi wanao disco!
Hizi lawama zote kwa Prof. Kitila sijui kina Paramagamba ni mchepuko wa kuondosha hoja muhimu sana aloweka Prof. Kitila kuhusu mikataba mipya ya madini ambapo alikuwa akiunga mkono bajeti ya wizara ya Madini lakini akiongezea kuwa hizo asilimia 16 za sheria mpya tulonayo hazijatosheleza kabisa mchango wa sekta ya madini nchini.
Hizi kesi 3 kati ya 7 mnazopigia kelele ni mpango mpya wa Wawekezaji hao warudi nchini. I bet, watarudishwa kama ilivyo Symbion na Wawekezaji wengine kina IPTL walofungua kesi zao za madai ndani na nje ya nchi ili wapate kurudi katika Biashara zao.
Hakuna jipya chini ya jua..
Kesi za namna hiyo kwa wenzetu wengine wasio na uzalendo huzitumia kama ni Fursa !! Na ndicho tunacho tahadharisha !! Lakini huenda tunajisumbua tu maana Uzalendo uliobakia ni msamiati wa kizamani !!Hizo leseni wengine walipata toka enzi za Mkapa na hakuna cha maana walichofanya.
Achilia mbali sheria na regulations mkataba pia una ‘performance clause’ umepewa eneo uchimbe madini; sio ulihodhi tu.
Uwezi kazi kwanini uachiwe umiliki tu, hizo kesi watashindwa sio kwa sababu serikali ilikosea, wameingia na kuvuruga strategy waliyoikuta na kufanya mambo kwa staili wanayoijua wao wenyewe.
Mkuu ngoja nikueleweshe... Hayo madai ya toka mwaka 1974 yalikuwa yakilipwa kidogo kidogo kila mwaka,Ni muhimu kwanza kutambua kesi hizo 7 ni za madai gani? Kama mtakumbuka ndege yetu ilizuiwa Canada na South kwa madai ya mwaka 1974. Je, hilo lilikuwa kosa la nani?
Kitendo tu cha kukosoa hatua za serikali hadharani ni makosa it doesn’t matter raisi angekuwa Lissu, Zitto, Magufuli, Samia or whatever.Kesi za namna hiyo kwa wenzetu wengine wasio na uzalendo huzitumia kama ni Fursa !! Na ndicho tunacho tahadharisha !! Lakini huenda tunajisumbua tu maana Uzalendo uliobakia ni msamiati wa kizamani !!
Hao Wakora wataje..Hapana sisi wengine tunajaribu kutahadharisha tu kwamba tusishabikie Nchi kunyonywa na Mumiani kwa kisingizio cha jamaa yule alifanya makosa !! Yapo makosa aliyafanya lakini na Wakora huwa wanachukuaga advantage ya kuingiza madudu yao !! Ndicho kitu ninachojaribu kutahadharisha Mkuu !
Na wewe ulifungua kesi ya kuvunjiwa mkataba ?Mimi namfahamu vizuri nimefanya nae kazi nilikuwa simwogopi nilimwambia ukweli akanifukuza nchi kwa kutumia mawaziri wake hakudhubutu kuniambia mwenyewe kwa hiyo alikuwa ananiogopa kwa uwezo wangu na sio upumbavu
Siwajui lakini wapo !!Hao Wakora wataje..
Fursa !!Kitendo tu cha kukosoa hatua za serikali hadharani ni makosa it doesn’t matter raisi angekuwa Lissu, Zitto, Magufuli, Samia or whatever.
Wanasiasa wa nchi yeyote na wa vyama vyote standard of behaviour ni kuweka national interest fist, wanyukane kwenye mambo mengine.
Clearly mtu ana conditional/repudiatory breach ya mkataba, amefungua kesi kwenye mahakama za uonevu. Badala ya mtu msomi kusoma sababu za hiyo mikataba kufutwa alichoangalia ni nchi imeshitakiwa na kwenda kuropoka bungeni.
Kwanini tusione anatafuta fursa, inawezekana kabisa anafanya lobbying kwa niaba ya wawekezaji walipwe apewe chake.
Haya ni matokeo ya kuingiza siasa kwenye mambo ni kitaalamu.Prof. Kitila Mkumbo anadai Tanzania imeshtakiwa na makampuni ya madini, na mashauri hayo yanapelekea serikali kuingia hasara.
Prof anadai Wasomi walitoa ushauri ili kuwafurahisha viongozi badala ya kuwaambia ukweli kuhusu madhara ya kuvunja mikataba ya kimataifa.
Na ukojitoa, hakuna mwekezaji atakayekuja Tanzania kwa sababu mahakama zetu hizi za uzalendo wa Rais, haziaminiki.
Highly probableFursa !!
NdioNa wewe ulifungua kesi ya kuvunjiwa mkataba ?
Kuna ajabu kushtakiwa ukipigania haki zako?
Hata ukijitoa bado utawajibika kwa miaka kumi zaidi that’s what we call sunset clause kwenye mikataba ya BIT and am not referring MIGA which is an insurance that an investor has to have to protect thier investments so please 🙏🏿 you need to educate your self before you take the risk of investing in Tanzania..wengi wametoa maoni kwamba kama hatutaki kupelekwa ICSID, MIGA, etc, basi tutangaze kwamba tumejitoa na hatutambui vyombo hivyo kama alivyofanya yule jamaa wa Bolivia.
Walimalizana na mpaka Boss wao akaja Ikulu Dar na inasemekana hao acacia wakakubali watalipa baadhi ya pesa walizotakiwa kulipa !
Unaweza usisema lakini usisifu. Tatizo linakuja pale unaposifu.Nani alithubutu kusema haya ukiacha Lisu ambae aliponea kifo? Unajizima data si ndio? Inahitaji kujitoa mhanga na sio Kila binadamu ana huo ujasiri
Ndio maana tunasema tusikubali kuwa na ushabiki kama wa Simba na Yanga katika masuala ya rasilmali za Nchi !!..madai yetu yalikuwa usd 191 billion.
..tukakubali barrick watulipe kidogo kidogo usd 300 million.
..sasa jiulize kama huo sio ulaghai na ubabaishaji.
..mimi nahisi Magu na genge lake walichukua RUSHWA toka kwa Barrick.