Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Hivi wewe unaelewa maana ya uwekezaji au unatoa hadithi za bulicheka kufanya utafiti wa madini kama lithium unajua ni million ngapi dollari unajitaji?? Mafuta tu shell walikuwa na boti inatumia dollari milioni 2 kwa siku imepaki hapo Dar kwa mwaka alafu leo unasema mwekezaji alitekeleza eneo huo ujinga ndio utakao wapa Tanzania hasara mpaka waamke. Kuwekeza maana yake ni kwamba unaweza kusubiri kitega uchumi chako kipate soko sasa kama hakuna soko unamnyanganya aliewekeza kwanza ummpe huyo aliekuja sasa wakati soko lipo ndio sababu Tanzania migogoro na wawekezaji haitoisha kama watu hawaelewi maana ya uwekezaji na haki za mtu kuwekeza. Huyo mpya mwambie awasiliane na aliewekeza kwanza na sio kumnyanganya aliewekeza kwanza na kumpa mpya kama mtwara Dangote na Azam shamba la miwa bagamoyo
 
Wewe acha kutetea ujinga kana kwamba wewe ndiye unayejua tu peke yako vipi kesi iliyosababisha ndege ya kwanza kukamatwa ilikuwaje ? Je ni utafiti?

Ama kuhusu wanasiasa kukosoa watangulizi ktk serikali mwasisi ni nani kama siyo huyo Magu unayetaka asikosolewe?

Muwe mnapima pande zote kabla ya kutoa hoja zenu.
 
Lisu unanpenda hee huyu ndo mwanasheria pekee anarikodi gan kwenye haya mambo au ndo Lesbia mwenzenu maana hamuachi kumtaja taja kila kona
Sijui hilo jina la 'zithromax' uliliokota wapi kwa akili kama unazoonyesha hapa!
Mwenye ufahamu wa mambo yanayohusu hilo jina hawezi kuwa na akili za kipuuzi namna hii.
 
Hapana.

Natamani sana pangekuwepo na mada ihusuyo hili jambo la wasomi kushindwa kutimiza majukumu yao kwa nchi yao na tukaujadili kwa kina.
"Kutoa ushauri" kwa kiongozi husika hakuji kwa njia moja. Na siyo lazima iwe mtu kwa mtu..

Taratibu za uongozi wa nchi haufanyiki kiholela, ukifanywa na mtu mmoja kwa kujiamria tu anachotaka yeye. Kuna mikutano mingi tu inayofanyika huko ndani na nje ya shughuli za serikali ambako wasomi hawa wanaweza kuwasilisha mawazo yao na kuchukuliwa/kuingizwa katika taratibu za utendaji wa nchi.
Wasomi wetu wamewasilisha machapisho wapi, hata nje ya serikali yakihusu nyanja walizosomea zinazoihusu nchi yetu moja kwa moja?

Kwa hiyo, hoja yako ya "msomi kuogopa kuwasilisha ushauri kwa kuogopa kuonekana kuwa ni 'threat'" siyo sahihi.
 
Jamani Tundu Lissu ajengewe tu mnara wa kumbu kumbu! Haya alionya hizi vimburu wanajifanya kuzungumza sasa!
 
Sijui hilo jina la 'zithromax' uliliokota wapi kwa akili kama unazoonyesha hapa!
Mwenye ufahamu wa mambo yanayohusu hilo jina hawezi kuwa na akili za kipuuzi namna hii.
Huyo ni Zinjanthropus bado hajawa binadamu
 
Najua kwa nini huoni tofauti kati ya hao wawili.
Mimi naina tofauti kubwa sana kati yao, kama ya usiku na mchana.
 
Duuhh mtamkumbuka sana Tundu Antipas Lissu, kile ni kichwa ambacho sijui kwann serikali inashindwa kumtumia
 
Najua kwa nini huoni tofauti kati ya hao wawili.
Mimi naina tofauti kubwa sana kati yao, kama ya usiku na mchana.
Unaweza nipa tofauti Moja?
Kikubwa nachoona Kitila alikua upinzani muda mrefu ila Mpina alikua CCM maisha yake yote so madudu yote anayajua kwa undani. Why alipokua waziri hakuchukua hatua, Leo Hana kitengo ndio alie lie? Bora kitila atajitetea alikua mgeni serikalini so asingeweza furukuta.
 
Kwanza inabidi uelewe tunajadili vitu gani. MADENI YA TAIFA (National debts) yatokanayo na mikopo sii madeni yanayojadiliwa hapa. Pili, ardhi alopewa Bakhresa ilikuwa haijaendelezwa kwa zaidi ya miaka 30 yani lilikuwa pori, ulitaka JPM afanye nini?

Kama raia wanachukuliwa ardhi zao wakishindwa kuziendeleza mnaona sawa lakini Mzungu ni kosa! Hivi nyie watu mkoje? Mmerogwa au!
 

Wapi umeambiwa leseni zilifutwa sababu ya performance? Umeambiwa walifuta leseni baada ya kubadili regulations mwaka 2018 so it doesn't have to do anything na performance indicators.

Kingine kama Kuna clause ya mkataba imekiukwa anaye determine ni settlement/arbitary sio mmoja wa parties. Yaani unaamka asbuhi unasema "umeniibia" unavunja mkataba? Hapana mnapeleka shauri la kuvunja mkataba na mnaeleza msingi kisheria ni upi ndio unavunja. Hata talaka husemi umemuacha mtu kichochoroni huwa mnaenda huko mahakamani.

Jamani mambo ya kitaaluma msiingize siasa.
 
Sikuwa na sababu ya kufanya hivyo, ingawa hilo liliniijia akilini nilipobandika hayo maneno; na bado sioni sababu muhimu ya kufany hivyo kwa sasa nikijua kwamba haya sasa yamekuwa kama malumbano na siyo mjadala tena.
 
Uwezi kazi kwanini uachiwe umiliki tu, hizo kesi watashindwa sio kwa sababu serikali ilikosea, wameingia na kuvuruga strategy waliyoikuta na kufanya mambo kwa staili wanayoijua wao wenyewe.
Imebadilika vipi wakati Kabudi Bado anaongoza timu za kufanya majadiliano ya mikataba kwenye eneo la madini. Ama unamaanisha Kabudi ni underperforming maana hata juzi mikataba imesainiwa na zile kampuni za Australia na Kabudi ndio alipewa credit.
 
Wasomi waliookotwa jalalani au unazungumzia wasomi wapi??
 
Mkuu kwa nchi ilivyokubwa.. JPM hakuona mapori huko mbele ya Bagamoyo.. Au Msata..?
Sasa kulikuwa na ulazima gani mpaka tunastakiwa na tunatakiwa kulipa..
 
Unaweza kuleta ushahidi ata wa picha kuonyesha hiyo migodi ikiwa imeendelezwa ata kidogo.
Sasa kesi wameshindaje kama Wana makosa? Au unadhani mahakama za nje unaweza shinda kesi bila facts on the table?

Hizo picha kama hakuna hao serikali ya Tanzania si wangeshinda kesi asubuhi tu!!

Hata ukimkuta mtu anakuibia Kuna procedure za kisheria. ukimpiga alafu ukampeleka kituoni tayari kesi inakugeukia hata kama ulikua na haki.

Tatizo lenu CCM ni kukurupuka Kila wakati badala ya kushirikisha akili. Nilishangaa sana mnabadili sheria nzito hivyo kwa hayo ya dharura? What was the rush? Kwani mkijipa wiki nzima mngepoteza Nini? Oneni Sasa mmekurupuka mnatuletea hasara.
 
Wanashinda hizo kesi zama hizi tu huko nyuma hakukuwa na mambo ya hovyo; si ajabu ata awa contest hayo madai kama walivyowapa Symbion hela kirahisi tu.


Halafu sijui case gani una refer nyingine bado hazina maamuzi.
 
Leta huo ushahidi sheria mpya ndio zilivunja hiyo mikataba.

Sikatai serikalini kuna vimeo wengi hasa kwenye kuingia mikataba but give them some credit.

Hakuna mwekezaji wa nje anawekeza kwa muda mrefu nchi yoyote hasa kwenye developed nations bila ya kuweka ‘stabilisation clause’ wanajua government changes na mikataba yao huwa na corruption kwenye kuipata.

Hiyo clause inailinda kampuni dhidi ya sheria mpya baada ya wao kuingia kwenye mkataba, ndio sababu moja wapo iliyochelewesha majadiliano ya LNG awakutaka kuwekeza kwa sheria za Muhongo zilizopelekwa kwa hati ya dharura kwa sababu zilikuwa na mipaka ya kuvuna kutokana na recoverable reserve amount zilizopo kwenye kila kisima. Wao walitaka waendelee na sheria zilezile walizopatia vitalu.

Kwa hivyo huko serikalini wanajua sheria mpya sio applicable kwenye existing contracts, hizo aziwezi kuwa sababu za kuvunja hiyo mikataba; huyo Kitila anaropoka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…