Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Hayo makampuni yalingoja mpaka mwamba aondoke ndio wafungue mashtaka ya kuvunja mikataba ya madini ??!! Wakati akiwa Hai aliyevunja mikataba walikuwa wanamuogopa kumshitaki ??!! Ukistaajabu ya Musa ……….. !! Michongo inakuja !!

..walifungua kesi wakati yupo hai.

..umesahau ndege zilikamatwa mara ngapi wakati Magu akiwa madarakani?

..umesahau kwamba acacia walifungua kesi wakati Magu akijadiliana na barrick?
 
..Prof.Kitila anadai Tanzania imeshtakiwa na makampuni ya madini, na mashauri hayo yanapelekea serikali kuingia hasara.

..Prof anadai Wasomi walitoa ushauri ili kuwafurahisha viongozi badala ya kuwaambia ukweli kuhusu madhara ya kuvunja mikataba ya kimataifa.

Kwanini hakumshauri Magufuli hivi anakuja kuleta umbeya sasa??
 
..bombadier iliyokuwa imeshikiliwa Canada 2016/17 ilitokana na kesi ya Magufuli kuvunja mkataba wakati akiwa waziri wa ujenzi

..bombadier iliyokuwa imeshikiliwa Canada 2016/17 ilitokana na kesi ya Magufuli kuvunja mkataba wakati akiwa waziri wa ujenzi.
Sio kweli, kesi iihusiana na shamba la Msouth lilotaifishwa na Serikali.. Mambo mengine jamani acheni chuki zenu muwe wakweli.
 
Kuna Juha mmoja humu anajiita Eltwege aje asikie kijani mwenzie anavyokubaliana na Lissu, maana huwa anabwabwaja humu kuwa hawajashtakiwa, kwa uzuzu wake eti anataka asikie neno MIGA hata zuzu huyu hajui maana ya MIGA.
Mi nilidhani kijani wote.
 
Ni muhimu kwanza kutambua kesi hizo 7 ni za madai gani? Kama mtakumbuka ndege yetu ilizuiwa Canada na South kwa madai ya mwaka 1974. Je, hilo lilikuwa kosa la nani?
Kwa sasa watajitokeza wengi kuongea lugha anayoipenda mama ili wapate nafasi ikiwemo kutetea majimbo yao.
 
..kuna makampuni yalishitaki wakati Magu yuko hai.

..umesahau suala hilo liliibukia Bungeni Prof.Kabudi akatoa majibu ya kejeli na kizandiki kwa wabunge wa upinzani

..walifungua kesi wakati yupo hai.

..umesahau ndege zilikamatwa mara ngapi wakati Magu akiwa madarakani?

..umesahau kwamba acacia walifungua kesi wakati Magu akijadiliana na barrick?
Ilikuwa lazima Magufuli kwa nchi za Magharibi kumkwamisha kwa njia zozote aidha kwa vikwazo ama sababu nyingine yeyote haswa baada ya kuwakwamisha Barricks na wawekezaji wengine katika Madini. Magufuli alikuwa MWIBA kwao na bahati nzuri kwao JPM alikuwa na maadui ndani ya nchi.

Hawakuwa na njia bora zaidi ya kumkwamisha isipokuwa hiyo ama kumuondoa kabisa madarakani kwa sababu walijua kuna uwezekano mkubwa akatawala miaka mitano mingine.

Kama walivyoondolewa kina Lumumba, Nkurumah, Sankara, Ghadaff, Magufuli pia ilikuwa LAZIMA..
 
Heshima kwako JokaKuu . Huyu jamaa ni wale wale tu. Haya alitakiwa ayaseme wakati yanafanyika na siyo kusubiri baada ya kuona Magufuli and co hawapo kwenye ulaji ndiyo aseme. Nina uhakika hata Magufuli angekuwepo mpaka sasa asingesema haya. Jamaa nimeshamdharau sana huyu na hana tofauti na hao anaowasema.
Cc Kalamu pita hapa, hoja hii hii nilisema juu ya Mpina.
 
Ilikuwa lazima Magufuli kwa nchi za Magharibi kumkwamisha kwa njia zozote aidha kwa vikwazo ama sababu nyingine yeyote haswa baada ya kuwakwamisha Barricks na wawekezaji wengine katika Madini. Magufuli alikuwa MWIBA kwao na bahati nzuri kwao JPM alikuwa na maadui ndani ya nchi.
Hawakuwa na njia bora zaidi ya kumkwamisha isipokuwa hiyo ama kumuondoa kabisa madarakani kwa sababu walijua kuna uwezekano mkubwa akatawala miaka mitano mingine.

Kama walivyoondolewa kina Lumumba, Nkurumah, Sankara, Ghadaff, Magufuli pia ilikuwa LAZIMA..
Conspiracy theorist!! Kila lawama kwa mabeberu wakati sisi wenyewe majizi humu humu. Hivi wizi aliyosema CAG Kuna mzungu kahusika? Why Kila failure yetu lawama kwa mzungu as if sisi wenyewe ni competent au waaminifu? Kwanini unaamini JPM auwawe na mabeberu Ilihali mafisadi yamejaa humu humu nchini?

Tuache hii inferiority complex and face the reality kuwa mchawi wa mtu mweusi ni mweusi mwenyewe
 
Ni muhimu kwanza kutambua kesi hizo 7 ni za madai gani? Kama mtakumbuka ndege yetu ilizuiwa Canada na South kwa madai ya mwaka 1974. Je, hilo lilikuwa kosa la nani?
Kitila anasema kesi 3 kati ya 7 ni issue za madini ikiwemo kufutiwa leseni kwa kampuni kadhaa za uchimbaji baada ya ammendements za sheria mwaka 2017 na regulations mpya za 2018.
 
Unafiki tu,unafiki tu wahuniiiii hawa
Lisu aluposimama katika ukweli walimdhihaki.

Ukweli ni kwamba kwenye kesi zote ambazo Serikali imeshtakiwa na makampuni ya kimataifa ya madini yaliyowekeza Tanzania, hakuna hata kesi moja ambayo Serikali ina uwezo wa kushinda. Ukiusema ukweli huu, wamafiki wanaamza kusema eti wewe siyo mzalendo! Kwao mtu mwongo ndiyo mzalendo.
 
Conspiracy theorist!! Kila lawama kwa mabeberu wakati sisi wenyewe majizi humu humu. Hivi wizi aliyosema CAG Kuna mzungu kahusika? Why Kila failure yetu lawama kwa mzungu as if sisi wenyewe ni competent au waaminifu? Kwanini unaamini JPM auwawe na mabeberu Ilihali mafisadi yamejaa humu humu nchini?

Tuache hii inferiority complex and face the reality kuwa mchawi wa mtu mweusi ni mweusi mwenyewe
Conspiracy theory ni ile unaambia rais amekufa kwa ugonjwa wa moyo au Covid. Mkuu tuna Uhuru wa habari na haki ya kuijeleza, kwa nini mnashindwa kuchanganya na za kwenu?

Ni kweli lawama zipo kwa Mzungu kwa sababu sisi ni kama mwanamke Malaya, siku zote ushawishi wa mwanamme ndio humfanya mwanamke akatembea nje ya ndoa, japo mmewe pia anaweza kuwa na mapungufu yake lakini hampi haki ya kutembea nja ya ndoa.

Serikali hii awamu ya sita, wanajua wazi kilichotokea na ndio maana sasa hivi ni KANYAGA TWENDA. Zinatumika kila mbinu kumfunika JPM wakati hakuna sababu ya maana.

Kama tumeamua kurudisha diplomasia na mabeberu sii waseme tu kuna haja gani ya kumzungunzia Magufuli. Hata wakati wa Nyerere, alipokufa bdio habari nyingi za kupinga Ujamaa lkn lipi jema tulofanya baada ya kumshutumu yeye?

Na iweje leo hii hotuba zake ndio zinashika mitazamo ya kila mwana siasa nchini! Je, Ule ubaya wake umeishia wapi?
 
Kabudi na mruma hao
Prof Mruma mnamwonea.

Kamati ya madini ya Mruma iliandika report ya kitaalam ambayo ilieleza wazi kuwa hakuna tunachoibiwa, na taarifa ya Acacia iliyopelekwa Serikalini kuhusiana kilichomo kwenye makinikia mi sahihi.

Baadaya report hiyo kupelekwa ikulu, watu wa TISS waliirudisha kwake na akaamriwa aibadilishe. Haiwezekani report iseme hatuibiwi wakati Rais amekwishawaambia wananchi kuwa tunaibiwa. Maskini Mruma hakuwa na namna, na maisha bado anayapenda. Akaibadilisha iendane na matakwa ya Rais.

Mpaka leo, Prof. Mruma anaeleza wazi kuwa anakereka sana akiikumbuka report ile, na kitendo cha baadhi ya watu kumwita profesa wa makinikia.

Na anasema kuwa aliiandika kwa namna ambayo kila mwenye uelewa wa masuala ya madini, aelewe kuwa amelazimishwa, yaani aliifanya report kuwa ya kienyeji sana ili wenye akili watambue kuwa amelazimisha. Aliisoma huku wakati wote akitetemeka.
 
Kuna Juha mmoja humu anajiita Eltwege aje asikie kijani mwenzie anavyokubaliana na Lissu, maana huwa anabwabwaja humu kuwa hawajashtakiwa, kwa uzuzu wake eti anataka asikie neno MIGA hata zuzu huyu hajui maana ya MIGA.
Etweke, Jilala, wewe unaamini ni watu wenye utimamu kichwani? Nadhani ni wa hivyo hivyo. Tuwakubali kwa sababu tu ya ubinadamu wao lakini hutarajii kusikia chochote cha maana toka kwao.
 
Back
Top Bottom