Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Wewe unaongelea hisia badala ya kuongelea ukweli.

Haya ni makampuni ambayo yalikuwa na leseni za kufanya utafiti.

Utafiti ni gharama kubwa na ni risk kubwa, ndiyo maana hakuna Serikali hata moja Duniani ambayo hufanya utafiti wa madini, mafuta au gas. Ni makampuni yenye mitaji yao ndiyo hufanya kazi hiyo. Uwezekano wa kupoteza pesa kwenye utafiti ni zaidi ya 90%.

Fikiria kampuni kama ya Petra ilikuja Tanzania ilifanya utafiti wa mafuta kwa gharama ya dola milioni 760, mafuta hawakupata, wakaondoka zao. Sasa hapo wewe umenyonywa kitu gani? Au unafikiri Tanzania ina uwezo wa kutenga japo dola bilioni 10 tu kufanya utafiti wa madini, mafuta na gas?

Makampuni ya nje au ya ndani hufanya utafiti kwa kuomba tu leseni, hakuna mkataba wowote, kinachoangaliwa ni sheria tu ya madini inasemaje kwa mtu anayetaka kufanya utafiti wa madini. Akiyapata madini, anataka kuanza uchimbaji, kama mradi utakuwa na mtaji wa zaidi ya dola milioni 100 ndiyo atasaini mkataba na Serikali, na atapewa leseni ya SML. Kama uwekezaji wako ni chini ya dola milioni 100 ataomba ML, na hakuna mkataba na Serikali, utaongozwa tu na sheria ya madini. Na hiyo haijalishi wewe ni Mtanzania au mgeni. Kama umefanya utafiti, lakini huwezi kuanza ujenzi wa mgodi mara moja, ili eneo ulilolifanyia utafiti liendelee kuwa lako wakati unajiandaa kuomba SML au ML, ukitaka utaomba Retention License. Na Retention License muda wake ni miaka mitatu tu, na hairuhusiwi kurudia kuiomba tena. Sasa hawa wawekezaji waliomba retention licenses, tukawapa, halafu baada ya miaka miwili, eti Serikali imefuta Retention License kuwa miongoni mwa leseni zinazotolewa na Serikali, na hivyo wote waliokuwa na retention licenses, wamepoteza haki zao zote! Kweli mtu mwenye akili timamu anaweza kufanya hivyo? Ulikuwa ni ukichaa wenye madhara makubwa kwa Taifa.
Hizo dolla mllion 760 uliziona au umesikia ww makapuku na wew ukapayuka , kama kasuku wa shamba porin .wawekazaji Katu huwa hawasemi ukweli has kww nchi ya Dunia ya tatu ambopo swala la uwazi ni F .kampuni inatumia 80m usd inarekodi kwenye vitabu 800m usd
 
Duh!

Mkuu 'Mkandara', hata nawe unaamini Magufuli aliondolewa?

Magufuli angekuwa anadunda hadi leo isingekuwa kiburi chake cha ujinga kuidharau COVID-19.

Ni tabia hizo hizo za dharau na kutotaka kufuata taratibu ndizo pia zilizovuruga mambo mazuri aliyonuia kuyafanyia nchi, kama haya ya madini.

Kwa mfano, angeachana na majivuno ya kujiona yeye hakuna wa kumpiga, akamwita Lissu na wengine na kuwasikiliza wanasema nini kuhusu swala hilo la mikataba, pasingekuwepo na tafrani zote zilizotokea na akina Lissu wasingefika huko walikofika.

Weaknesses za Magufuli zilikuwa katika tabia zake mbovu.
Lisu unanpenda hee huyu ndo mwanasheria pekee anarikodi gan kwenye haya mambo au ndo Lesbia mwenzenu maana hamuachi kumtaja taja kila kona
 
..Prof.Kitila anadai Tanzania imeshtakiwa na makampuni ya madini, na mashauri hayo yanapelekea serikali kuingia hasara.

..Prof anadai Wasomi walitoa ushauri ili kuwafurahisha viongozi badala ya kuwaambia ukweli kuhusu madhara ya kuvunja mikataba ya kimataifa.

[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
..zimekamatwa ndege tatu.

..bombadier iliyokamatwa Canada kwa kesi ya mkandarasi aliyevunjiwa mkataba na Magu wakati akiwa waziri wa ujenzi.

..airbus iliyokamatwa Afrika Kusini kutokana na kesi ya mzungu aliyenyang'anywa mali zake wakati wa utawala wa Nyerere.

..Boeing inayoshikiliwa Uholanzi. Madai ya kesi hii siyafahamu.
Si bora ungesema zote hauzifahamu kuliko kudanganya ungepungukiwa Na nini kiongozi
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Ukimsikia kwa makini Prof Kitila kazungumzia toka mfumo wa zamani, kuja kati miaka ya 90 na saaa hivi tuko wapi na tunatakiwa tufanye nini. Hizi kesi 3 za madini kati ya kesi 7 zipo mahakamani.

Tumefuta liseni za Uwekezaji kutokana na hitilafu za mitakaba yenyewe. Makosa yalifanyika kwenye mikataba na sii hatua tulochukua. Ushauri ulikuwa mbovu toka mwanzo wa mikataba hiyo.

Kesi zipo mahakamani bado, haina maana makosa yalifanyika ikiwa lengo ni sisi wenyewe tunataja tumiliki madini haya yalotajwa, tume.makini sana hapa.

Na kapendekeza turudi katika mfumo wa zamani kuhakikisha sisi wenyewe ndio tunamiliki madini hayo. Mbunge nd. Muhongo pia ameishauri serikali vivyo hivyo.


Hizi Kesi zitatuumiza lakini haziwezi kutuzuia kabisa kuacha njia yetu kwa sababu tutapoteza mabillioni ya Usd kwa kuogopa kesi kadhaa.

Angalizo hapa ni tujiandae maana kuna vita kubwa ya Madini inakuja, wataalam wetu wamshauri vema rais (tahadhali ya vita ya madini) wasimshauri ili kumfurahisha wakati sisi tutaumizwa kwa kuweka mikataba mibovu.

Mama mgeni katika mambo na hawa wataalam wa sheria ndio ngao na tegemeo letu, wamshauri vizuri sii kutaka kumfurahisha ili yasije tokea ya nyuma..

Kwa mtazamo wangu, inabidi mtu umsikilize kwa makini sana Prof. Kitila toka mwanzo ukifuatia record yake akiwa Chadema kuhusu msimamo wake juu ya madini (Liganga na Mchuchuma)

Maasalaam..
 
Mtanikumbuka

Wakati ushauri mbaya unatolewa yeye alikuwa ACT Wazalendo?
Huyo ni mnafiki Mwandamizi amesahau kuwa anaUbunge wa kupewa! Subiri ije 2025 hatathubutu hata kugimbea udiwani...labda mama Ampe tena!
Ninjeri wangetubu ...watuambie ukweli kuwa waliishinkinafiki na kizandiki mbele za JIWE ..badala yakujifanya wanakosoa .Hayo yalikosolewa na Wazalendo wengi lakini wao waliufyata !
 
Ni hivi ngoja nikuambie Africa tunafanywa nyumbu na watu weupe Kwa Sababu nimemshuhudia moina mara kadhaa analalamika serikali au wasomi wetu kushindwa kuchukua hatua za kuwalipisha wawekezaji Kwa ucheweleshaji miradi au kufanya kinyume cha mkataba.

mambo haya ni Kwa Sababu ya tunaamini kumpiga faini mwekezaji ni kumfukuza lakini wanatufanyia Mambo ya ovyo sana na unyanyasaji Kwa Sababu hatuna wataalamu.

Magufuli namtolea mfano hapa kwamba yeye kama mwanadamu alikuwa anaumia kuona watanzania tunafanywa kama wajinga japo mikataba tuliyoingia nayo hizo kampuni ni ya kinyonyaji.

Ni Sawa na umempangisha mpangaji kwenye nyumba unayoishi alafu amekulipa Kodi ya mwaka alafu anafanya matendo ambayo yanakuudhi Ila ukivunja mkataba unatakiwa umlipe fidia na ukimuacha anazidi kukuharibia familia anatembea na mkeo na watoto hivi utasubiri mkataba uishe au utafukuza kulinda hadhi yako.


Mikataba mingi ya madini Ni ya kinyonyaji na moja ya masharti ya unapomlazimisha au kumshawishi mwekezaji ni kwamba mikataba itakuwa ni Siri haiwekwi hadharani wala kujadiliwa .
Jambo ili serikalini hawataki kuliweka wazi lakini ndio ukweli kwamba wawekezaji wanatoa sharti kwamba kama unataka niwekeze Tanzania mikataba haitojadiliwa mpaka tutakaposainishana wakilenga kwamba kitendo cha kujadiliwa na WANANCHI kutaleta sintofahamu au kukataliwa .
Ubarikiwe.
 
Huo ni uchawa tu baada ya mama kusema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake, wengine ndo Hao wanaanza kununua kamba mpya waziongezee hapo wale wanavyotaka.....
Kwahiyo nawew waweza tafuta yako mkuu uone waweza kula vipi.. naona wapinzani walivyolambishwa asali na mama wanaona JPM ndo alifanya kosa na ndo mahubiri yao this is lack of cognitive skills... watanzania washabadilika hawataki tantarira za ajabu

Hoja yako ni nini hapa, au ukweli umekuumiza hadi hujui useme nini? Magufuli alikuwa na pupa za kijinga na haya ndio matokeo yake.
 
Ni hivi ngoja nikuambie Africa tunafanywa nyumbu na watu weupe Kwa Sababu nimemshuhudia moina mara kadhaa analalamika serikali au wasomi wetu kushindwa kuchukua hatua za kuwalipisha wawekezaji Kwa ucheweleshaji miradi au kufanya kinyume cha mkataba.

mambo haya ni Kwa Sababu ya tunaamini kumpiga faini mwekezaji ni kumfukuza lakini wanatufanyia Mambo ya ovyo sana na unyanyasaji Kwa Sababu hatuna wataalamu.

Magufuli namtolea mfano hapa kwamba yeye kama mwanadamu alikuwa anaumia kuona watanzania tunafanywa kama wajinga japo mikataba tuliyoingia nayo hizo kampuni ni ya kinyonyaji.

Ni Sawa na umempangisha mpangaji kwenye nyumba unayoishi alafu amekulipa Kodi ya mwaka alafu anafanya matendo ambayo yanakuudhi Ila ukivunja mkataba unatakiwa umlipe fidia na ukimuacha anazidi kukuharibia familia anatembea na mkeo na watoto hivi utasubiri mkataba uishe au utafukuza kulinda hadhi yako.


Mikataba mingi ya madini Ni ya kinyonyaji na moja ya masharti ya unapomlazimisha au kumshawishi mwekezaji ni kwamba mikataba itakuwa ni Siri haiwekwi hadharani wala kujadiliwa .
Jambo ili serikalini hawataki kuliweka wazi lakini ndio ukweli kwamba wawekezaji wanatoa sharti kwamba kama unataka niwekeze Tanzania mikataba haitojadiliwa mpaka tutakaposainishana wakilenga kwamba kitendo cha kujadiliwa na WANANCHI kutaleta sintofahamu au kukataliwa .

Yeye Magufuli aliweka mikataba wazi kwakuwa alikuwa na uchungu na mali za watanzania?
 
Hayo makampuni yalingoja mpaka mwamba aondoke ndio wafungue mashtaka ya kuvunja mikataba ya madini ??!! Wakati akiwa Hai aliyevunja mikataba walikuwa wanamuogopa kumshitaki ??!! Ukistaajabu ya Musa ……….. !! Michongo inakuja !!
Ndege si zilikamatwa wakati akiwa hai madarakani, au unajizima dat?
 
Wabaya wa Tanzania sio makampuni ni watanzania wenyewe,umshitaki mtu ambaye bado unamhitaji kuchota Mali kwake na kuneemeka!!!mwenye kichwa kibovu ndo anaweza kuamini. Wapo watanzania nyuma ya haya makampuni .
Kabisa..na inasikitisha kuona watu wanashangilia taasisi yenye maazimio mazuri kufeli... Nazidi kuamini ngozi nyeusi Ina matatizo
 
Jibu ulichouliza sio kujitungia swali na kujijibbu unavyotaka
Mkuu huyu huwa na madini, ila likija kwenye suala la Mwafrika kufanya maamuzi yake yeye huwa anakasirika na kuanza kutupa vijembe. Ukifuatilia uwasilishaji wake na mtiririko wa Uzi huu kama mada inavyoelezea unategemea kusikia au kuona majibu yanayokuwa na mtazamo wa Kuwa...Viongozi huwa wanalaghaiwa- lakini hilo sio iliyokuwa lengo lake- nasema kwa Uhakika! Anajua fika Mada yake inamgusa moja kwa moja Hayati Magufuli na anajua fika kuwa mashauri anayodai Kitila yana Ukweli ila yeye hataki huo ukweli kwani inaosha na kuondoa madoa wanayomwekea Hayati kwa lengo Kuu ambalo ni kumchafua na kuonyesha kila Jambo lililotokea kwenye Utawala wake alilifanya au kuagiza lifanyike, Lilikuwa halifai kwa Taifa au Kimataifa Kiufupi, wanadai hayati Rais J.P.M alihusika peke yake. Sasa utaona kuwa, kwa kipindi kifupi kumetokea vitu Vinvyoondoa madoa hayo na kuwafanya hawa wenzetu humu kuonekana ni wadanganyifu()mfano:kuhusu COVID 19, au hapa Kuwa Hayati alipata mashauri mabaya au kudanganywa. Haya mambo yanawachafua EGO zao na pale wanapopata mwanya wa kuendeleza uwongo(kumbuka hawa ni Spin Doctors) basi watafanya hivyo na ndio maana hawajibu kulingana na mada bali kile wanachotaka umma uone. Na ndio huko..."
kujitungia maswali na kuyajibu Wanavyotaka
Alimradi machafuzi yanaendelea.
 
Back
Top Bottom