Wewe unaongelea hisia badala ya kuongelea ukweli.
Haya ni makampuni ambayo yalikuwa na leseni za kufanya utafiti.
Utafiti ni gharama kubwa na ni risk kubwa, ndiyo maana hakuna Serikali hata moja Duniani ambayo hufanya utafiti wa madini, mafuta au gas. Ni makampuni yenye mitaji yao ndiyo hufanya kazi hiyo. Uwezekano wa kupoteza pesa kwenye utafiti ni zaidi ya 90%.
Fikiria kampuni kama ya Petra ilikuja Tanzania ilifanya utafiti wa mafuta kwa gharama ya dola milioni 760, mafuta hawakupata, wakaondoka zao. Sasa hapo wewe umenyonywa kitu gani? Au unafikiri Tanzania ina uwezo wa kutenga japo dola bilioni 10 tu kufanya utafiti wa madini, mafuta na gas?
Makampuni ya nje au ya ndani hufanya utafiti kwa kuomba tu leseni, hakuna mkataba wowote, kinachoangaliwa ni sheria tu ya madini inasemaje kwa mtu anayetaka kufanya utafiti wa madini. Akiyapata madini, anataka kuanza uchimbaji, kama mradi utakuwa na mtaji wa zaidi ya dola milioni 100 ndiyo atasaini mkataba na Serikali, na atapewa leseni ya SML. Kama uwekezaji wako ni chini ya dola milioni 100 ataomba ML, na hakuna mkataba na Serikali, utaongozwa tu na sheria ya madini. Na hiyo haijalishi wewe ni Mtanzania au mgeni. Kama umefanya utafiti, lakini huwezi kuanza ujenzi wa mgodi mara moja, ili eneo ulilolifanyia utafiti liendelee kuwa lako wakati unajiandaa kuomba SML au ML, ukitaka utaomba Retention License. Na Retention License muda wake ni miaka mitatu tu, na hairuhusiwi kurudia kuiomba tena. Sasa hawa wawekezaji waliomba retention licenses, tukawapa, halafu baada ya miaka miwili, eti Serikali imefuta Retention License kuwa miongoni mwa leseni zinazotolewa na Serikali, na hivyo wote waliokuwa na retention licenses, wamepoteza haki zao zote! Kweli mtu mwenye akili timamu anaweza kufanya hivyo? Ulikuwa ni ukichaa wenye madhara makubwa kwa Taifa.