Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

..viongozi wetu pia wamelelewa vibaya kiuongozi.

..mfumo umewadekeza sana kwa kuonea wananchi bila kuwajibika au consequences zozote.

..kwa mfano kiongozi anaweza kutoa uamuzi nyumba za wananchi zivunjwe na kusitokee athari zozote kwake. Na wananchi hawana mahali pa kwenda kulalamika kwasababu viongozi wetu wana-control kila kitu ikiwemo mahakama.

..sasa tabia hizohizo wanakwenda nazo ktk kufanya maamuzi dhidi ya wawekezaji. lakini hawa wawekezaji hawana tabia za kinyonge-nyonge kama Watanzania wa kawaida. Pia wawekezaji wana option ya kwenda kutafuta haki zao nje ya nchi ambako viongozi hawana control au mamlaka.

You are assuming kuwa wanaotengeneza hiyo mikataba wana ujuzi wa hayo mambo which is not correct!! Tunapeleka watu kwenda kutayarisha mikataba na kuletewa kusainiwa mikataba iliyoandikwa katika lugha tusiyoielewa. Kuna mikataba imetiwa saini hapa ikiwa katika lugha ya MANDARIN! Unafikiri kweli hiyo mikataba itakuwa kwa faida yetu au ya Wachina?
Ile mikataba mingine ya madini iliyosainiwa huko nyuma watu tuliowakabidhi ile Kazi hawakuwa waaminifu na kwavile they were left not to account for their shortcomings kwa mfano kwenye MAKINIKIA basi wanaendeleza game lao!!
 
"Kutafuta madini"
Kama hapati madini hana dai lolote juu ya ardhi hiyo, au siyo?
Ndio maana yake umeomba eneo kwa sababu ya kuchimba madini; that is the main condition ya contract to be specific it’s a ‘unilateral contract’ wewe uliyoomba hiyo kazi unawajibika na performance ya kutafuta na kuchimba madini.

Uifanyi hiyo kazi, aupo site miaka kibao na eneo limebaki kama pori.

Wewe ndio raisi wa Tanzania huyo mwekezaji ambae hana hela ungemwachia tu; wakati obvious conditional breach.
 
Mnafiki tu huyu na kapata ubunge wa michongo ambao haupati Tena na hajatufanyia lolote. Tumevunjiwa nyumba zetu hata siku moja hajapaza zauti angalau tupewe kifuta machozi.
Mwendazake alimbeba Sana halafu kumbe hata shukrani Hana.
Uwaziri ulimshinda, ukaribu mkuu ndio kabisa.

Hawa Ndio Maprof. Mchongo wanaojali matumbo yao kwanza. Huyu si alinunuliwa na Jiwe akaenda ccm ; Halafu Jiwe akamuhonga kuwa Katibu mkuu Halafu uBunge na Waziri? Watu kama Hawa CHAWA ni wa kukaa nao mbali sana!
 
Nakiri sikujieleza vizuri na kueleweka nilichoandika hapo.

Ukiacha mstari wa kwanza ambao ni nje ya mada hii, maneno mengine yote nilikuwa ninakubaliana na hoja yako ulivyoieleza hapo.

Huo mstari wa kwanza unahusu uelewa wangu kwako kuhusu mambo mbalimbali tuliyowahi kukutana na kuyajadili humu JF, mengine tukikubaliana, na mengine tukipishana mitizamo. Hili ni jambo la kawaida.

Kuhusu hizi kesi, ni kama umenistua akili kuanza kujiuliza juu ya nini ambacho huwa tunashtakiwa juu yake na mara nyingi kushindwa kujitetea. Sijui kama kuna mwekezaji yeyote aliyekuwa tayari kawekeza na mgodi wake ukanyang'anywa na serikali na yeye kuamua kwenda mahakamani kujitetea juu ya hilo.

Kwa uelewa wangu sasa, baada ya kukusoma ni kuwa hawa watu wanaotushtaki hawana madini yoyote ambayo walishayagundua, bali ni watu (Kampuni) zilizopewa eneo kutafuta madini. Ambacho bado pia sikijui, ni kama wanapopewa maeneo hayo wanayotakiwa kupewa madini kuna makubaliano yanayoifunga serikali kutoyadai tena maeneo hayo ikiyahitaji. Je hii mikataba masharti yake yapoje?
Hawa watu hupewa umiliki wa eneo husika; kwa muda gani? Ni gharama zipi hutakiwa kuzikamilisha wakati wakitafuta madini hayo. Ninaelewa pia baadhi ya maeneo hayo ni makazi ya wananchi ambao huendelea na shughuli zao kama kawaida.
Sasa huyu mwekezaji anayo haki gani juu ya eneo kama hilo!
Uwekezaji Tanzania land lease ni 33 years tenure. Hiko ndio wanachodai hawa matapeli kufutiwa matumizi ya umiliki kabla ya muda na bila ya kulipwa fidia.

Mkataba pia una mambo mengi crucial ni kitu kinaitwa ‘consideration’ hiyo ni thamani mnayobadilishana.

Nakupa shamba, uliendeleze na ulitumie. Wewe kwa sababu una lease ya 33 years unaamuwa kulitekeleza nikilichukua ushtaki.

Umesahau consideration ilikuwa ulime uuze unilipe kodi ndio sababu ya kukupa ardhi. Hiyo ni conditional breach ya mkataba sio tu nauvunja huko kwa wazungu wewe ndio unashitakiwa for loss of income na serikali umewapotezea kodi zao, wangempa mtu mwingine hilo shamba angelitumia vilivyo na kuwapa faida.

Conditional/repudiate ni breach inavunja mkataba wowote, it’s a serious issue in a contract.
 
Mimi Tena kivipi wakati kasema mwanaCCM mwenzako Tena bungeni kama angedanganya wangesema afute kauli kwenye Hansard isiwepo.

Nyie mlisema hatuwezi shtakiwa tunatishwa tu na Lissu. Leo Tena mnahamisha magoli kwamba kesi zipo ila maamuzi Bado?

Serikali ipi inajua mkuu? You're understating the incompetence ya watendaji wa serikalini. Mfano sheria ya permanent sovereignity ilitaka settlement zozote zifanyike katika mahakama za ndani. Kwani hawakujua hicho kitu hakifai? Mwaka mmoja baadae ndio wakafanya ammendements Ili kesi ziendelee kusikilizwa huko ICSID, ICC and so on. Ni hao hao serikali walidai Acacia imekwepa Kodi ya trillion 300 Leo hii wanakiri haikuwa kweli ilihali walipewa vyeti kabisa kama mashujaa kwa kuandaa ripoti. So don't understimate upuuzi wa hao watendaji
Waliotunga hiyo sheria walikuwa awajabobea katika maswala ya international business law.

Hakuna nchi inayotaka kuvutia wawekezaji halafu iseme maamuzi ya kesi yatafanyika Tanzania.

As a free country unaweza weka hiyo sheria; ila hakuna mtu mwenye lengo la kuwekeza kwa muda mrefu atakuja kwa sababu nyingi amongst them washajifunza serikali za third world hazitabiriki ndio msingi wa stabilisation clause pia.

Sasa ukiweka sheria pretty much uitaji FDI na ndio sababu ya wao kubadili hiyo sheria.
 
Mlimtukana Lissu leo mmeanza kushtakiwa na bado.
Unafikiri anaeshtakiwa ni JPM au SAMIA? JITAFAKARI.
Ni kibaraka tu kama vibaraka wengine, kama ana uchungu na uzalendo wa Taifa angeungana na huyo aliethubutu kutetea cha kwetu.
Yupi bora, anaetetea maslahi ya taifa kwa nguvu au anaeacha taifa liteketee kwa kuogopa atashtakiwa?
 
Mkuu 'Rasbamba; hebu tulizana kidogo utueleze utaratibu wenyewe hasa upoje katika kupewa ardhi huko wanakopewa hao watafuta madini.
Hii ardhi huwa wanapewa hati miliki ya eneo husika, kama kwa mfano ugawaji wa viwanja unavyofanyika?

Katika utaratibu huo mwekezaji hupewa masharti gani ya kuyatimiza.

Inaelekea kuwa na ufahamu juu ya swala hili, hebu tufafanulie vizuri ili tujue makubaliano yahusuyo uwekezaji wa namna hiyo.

Jibu lako hapo juu ulilompa 'Mayor', kidogo halijitoshelezi, nadhani ulchukulia tu kwamba wasomaji watakuwa wanajua unachozungumzia. Fafanua kidogo sote tupate uelewa.
Kalamu , kesi nyingi ambazo mali za Tanzanian kama ndege zimeshiliwa zinatokea na ardhi. Uwekezaji wa Madini unawekezwa kwenye ardhi kwa hiyo kitu cha kwanza katika uwekezaji huo lazima uwe na ardhi. Mimi nikipoteza mda wangu hapa kufafanua bado wengi vichwa ngumu watabisha kwa hiyo wewe jielimishe mwenyewe nenda kwenye mtatandao utasoma kama au muulize huyo waziri atoe ufafanuzi walibadilisha sheria zipi na ilikuwaje wakaanza kutokuelewana na na hao wawekezaji wa madini kwani kuna kesi tatu za madini na karibu zitakwisha kwa hiyo majibu yatakuja karibuni. Wawekezaji wa madini wana MIGA insurance ambayo ni gali sana ukimfutia mkataba na yeye ana MIGA utapambana nae na aliempa bima kwa hiyo wewe kushinda ni ndoto ya alinacha
 
Sina jibu kwa swali lako mkuu Rasbamba. Inawezekana ni kwa sababu sikulielewa vizuri swali lenyewe.
Jibu ni kwamba hatuna wasomi tuna wachumia matumbo yao na ndugu zako na marafiki wao kwa hiyo Watanzania waamke wajielewe watetee maisha yao na ya watoto wao la sivyo watadhulumiwa kila kukicha
 
Halafu huyu Mkumbo hivi anajitambua kweli? Aliwahi kusimulia jinsi alivyoingizwa UDSM kuwa mwalimu BILA qualifications. It is a shame. Kisa alipokuwa rais wa serikali ya wanafunzi pale UD aliwasaliti wenzie kwenye mgomo.

BILA AIBU yeye anadai eti kiongozi fulani pale UD alimgundua kuwa ni talented. Shame shame shame
Hahaha aliwasaliti wenzake kwenye mgomo wa mwaka 1994 akapelekwa Nairobi hahahaha
 
Hahaha aliwasaliti wenzake kwenye mgomo wa mwaka 1994 akapelekwa Nairobi hahahaha
Kumbe wengi tunalifahamu hili. Halafu usaliti hata siku moja hauishi mara moja . Alikuwa msaliti CHADEMA kiongozi wake ZZK nako akafukuzwa. Kwa bahati mbaya sana wakati huu ni lazima awe chawa kweli kweli. Alipoingia siasa ina maana alijiuzulu kazi UDSM kufuata na sheria za nchi. Uchawa usipomsaidia akaendelea kuwepo kwenye siasa au utumishi wa kuteuliwa kamwe hawezi kurudi UDSM kwa sababu lazima aombe kazi upya. Na akiomba wataangalia vyeti vyake vyote kuanzia degree ya kwanza. Sasa GPA ya degree ya kwanza haikutosha kuajiriwa kama TA ila ikasemekana ni talent aliyefaidi kwenye usaliti akaamuru aajiriwe, leo hii hiyo kitu haiwezekani. Hata CAG akikuta upuuzi kama huo atapiga query kubwa. Lazima aongeze uchawa mara elfu na elfu.
 
Jibu ni kwamba hatuna wasomi tuna wachumia matumbo yao na ndugu zako na marafiki wao kwa hiyo Watanzania waamke wajielewe watetee maisha yao na ya watoto wao la sivyo watadhulumiwa kila kukicha
Kwenye hili ninakubaliana nawe moja kwa moja.
Ili "waTanzania waamke, wajielewe watetetee maisha yao na ya watoto wao...", ni lazima kwanza pawepo na watu wenye uelewa huo ambao wataongoza juhudi hizo.

Mimi naamini waTanzania wanajielewa na wanatambua haya yote yanayofanyika chini ya hawa viongozi tulionao sasa; waTanzania wanachokikosa, tena sana ni uongozi wa kuunganisha na kusimamia juhudi za kukataa haya yanayofanyika sasa hivi.
 
Muungeni mkono lissu awasaidia sana sisi wengine hatupo tanzania tulifukuzwa kwa sababu ya kuelimisha na kusema ukweli .
 
Mnafiki tu huyu na kapata ubunge wa michongo ambao haupati Tena na hajatufanyia lolote. Tumevunjiwa nyumba zetu hata siku moja hajapaza zauti angalau tupewe kifuta machozi.
Mwendazake alimbeba Sana halafu kumbe hata shukrani Hana.
Uwaziri ulimshinda, ukaribu mkuu ndio kabisa.
Sijui akili umezipata lini maana ungekuwa nazo toka mwanzo usingejenga karibu na barabara utadhani maisha ni enzi zile kutuma barua kwa njia ya mabasi- IRUSHE TU TUTAIONA
 
Prof. Kitila Mkumbo anadai Tanzania imeshtakiwa na makampuni ya madini, na mashauri hayo yanapelekea serikali kuingia hasara.

Prof anadai Wasomi walitoa ushauri ili kuwafurahisha viongozi badala ya kuwaambia ukweli kuhusu madhara ya kuvunja mikataba ya kimataifa.

Kitila Mkumbo,anawakilisha Ma Prof wa hovyo kabisa kutokea Tanzania.Kitila Mkumbo ni Prof mnafiki ,muongo na asiyesitahili kupewa nafasi ya uongoz kwa kuwa sio mkweli.Nilikutana ,na ndugu huyu kwa Mara ya kwanza Mwaka 1992 mwezi wa nane,akiwa na wenzake wakitokea Singida ,shule moja ya sekondari iliitwa Mwenge.Ndugu huyu ,alifika Pugu high school kusomea PCB.Lakin alifika pale akiwa na division three.Kwa hiyo hakuwa na uwezo mkubwa.Ndugu huyu alimaliza Pugu high school ,Mwaka 1994 na kupata division three Tena.Lakin alitumia mbinu anazozijua akajiunga ,UDSM.Pale UDSM ,hakupata GPA ya maana lakin ,akabakishwa kuwa lecturer ,wakati wenye GPA za maana wakiondoka chuoni.Nimejaribu kuweka historia yake ,ili mjue kuwa huyu hana uwezo mkubwa wa akili ,Ila ni mtu wa kuforge ,kujipendekeza na pia kutumia opportunity kusonga mbele.Kutumia opportunity Nina maana ni mtu anayeweza kubadilika ghafla kwa ajili ya maslahi tu.Kwa Sasa anajaribu kubadilika na kumponda JPM ili apewe nafasi hata ya uwaziri.Lakin kumbuka JPM alimtoa jalalani na kumpa ukatibu mkuu na pia uwaziri.Lakin anaona kuwa JPM ameshafariki ,kwa hiyo ni kumkandia tu.Hatuwezi kuendelea tukiwa na maprofesa wa hovyo Kama Kitila.
 
Kwa hiyo hija iliyopo hapa ni kwamba waliotushtaki wako sahihi na sisi ndiyo wenye makosa.

Zaidi ni kuwa wasomi waliowahi kuwashauri viongozi hawana makosa isipokuwa wenye makosa ni viongozi ambao waliwahi kuchukua hatua baada ya ushauri, hatua zilizopelekea tukashtakiwa; hao ndiyo wenye makosa

Kati ya wasomi wetu tulionao ambao mara nyingi huwa wananipa wakati mgumu sana kuelewa hoja zao, ni huyu Mbunge wangu
 
Sijui akili umezipata lini maana ungekuwa nazo toka mwanzo usingejenga karibu na barabara utadhani maisha ni enzi zile kutuma barua kwa njia ya mabasi- IRUSHE TU TUTAIONA
Utakua ndio wewe Prof. Uliyenunuliwa na mwendazake kwa Bei ya jioni ili kutoka upinzani?
How can a full prof. Be bought like a sack of beans? I pity you.
 
Kwa hiyo hija iliyopo hapa ni kwamba waliotushtaki wako sahihi na sisi ndiyo wenye makosa.

Zaidi ni kuwa wasomi waliowahi kuwashauri viongozi hawana makosa isipokuwa wenye makosa ni viongozi ambao waliwahi kuchukua hatua baada ya ushauri, hatua zilizopelekea tukashtakiwa; hao ndiyo wenye makosa

Kati ya wasomi wetu tulionao ambao mara nyingi huwa wananipa wakati mgumu sana kuelewa hoja zao, ni huyu Mbunge wangu

..wasomi walimuendekeza Magufuli na kumwambia mambo anayopenda kusikia, badala ya kumwambia ukweli na uhalisia.

..matokeo ya ushauri huo wa " kishujaa" serikali imeburuzwa mahakamani mara kadhaa, imeshindwa kesi, na kulazimika kuingia hasara ya kuwalipa wawekezaji fidia.
 
Kitila Mkumbo,anawakilisha Ma Prof wa hovyo kabisa kutokea Tanzania.Kitila Mkumbo ni Prof mnafiki ,muongo na asiyesitahili kupewa nafasi ya uongoz kwa kuwa sio mkweli.Nilikutana ,na ndugu huyu kwa Mara ya kwanza Mwaka 1992 mwezi wa nane,akiwa na wenzake wakitokea Singida ,shule moja ya sekondari iliitwa Mwenge.Ndugu huyu ,alifika Pugu high school kusomea PCB.Lakin alifika pale akiwa na division three.Kwa hiyo hakuwa na uwezo mkubwa.Ndugu huyu alimaliza Pugu high school ,Mwaka 1994 na kupata division three Tena.Lakin alitumia mbinu anazozijua akajiunga ,UDSM.Pale UDSM ,hakupata GPA ya maana lakin ,akabakishwa kuwa lecturer ,wakati wenye GPA za maana wakiondoka chuoni.Nimejaribu kuweka historia yake ,ili mjue kuwa huyu hana uwezo mkubwa wa akili ,Ila ni mtu wa kuforge ,kujipendekeza na pia kutumia opportunity kusonga mbele.Kutumia opportunity Nina maana ni mtu anayeweza kubadilika ghafla kwa ajili ya maslahi tu.Kwa Sasa anajaribu kubadilika na kumponda JPM ili apewe nafasi hata ya uwaziri.Lakin kumbuka JPM alimtoa jalalani na kumpa ukatibu mkuu na pia uwaziri.Lakin anaona kuwa JPM ameshafariki ,kwa hiyo ni kumkandia tu.Hatuwezi kuendelea tukiwa na maprofesa wa hovyo Kama Kitila.

..tunakosea kumchambua Kitila Mkumbo binafsi.

..njia sahihi ni kuchambua hoja aliyoitoa.
 
Muungeni mkono lissu awasaidia sana sisi wengine hatupo tanzania tulifukuzwa kwa sababu ya kuelimisha na kusema ukweli .
Hapa unanifanya nisiamini chochote unachokiandika humu.
Hiyo uliyotaja siyo sababu ya msingi, na ujue kwamba siyo peke yako una hali hiyo.

Popote ulipo, kama unajali hali za waTanzania, hiyo siyo sababu ya kukuzuia. In 'fact', hiyo ndiyo ingekuwa sababu muhimu sana ya wewe kushiriki katika juhudi hizo.

Kuhusu Lissu, ni wakati wake sasa kujitambulisha anaposimamia yeye kama yeye, bila ya kufungwa mnyororo na chama chake, au kutoonekana kutokuwa na shukrani kwa waliosaidia kuokoa uhai wake. Kuipigania Tanzania kuna thawabu kubwa zaidi kushinda kitu kingine chochote, ikiwa ni pamoja na maisha na uhai wa mhusika.
 
Back
Top Bottom