..viongozi wetu pia wamelelewa vibaya kiuongozi.
..mfumo umewadekeza sana kwa kuonea wananchi bila kuwajibika au consequences zozote.
..kwa mfano kiongozi anaweza kutoa uamuzi nyumba za wananchi zivunjwe na kusitokee athari zozote kwake. Na wananchi hawana mahali pa kwenda kulalamika kwasababu viongozi wetu wana-control kila kitu ikiwemo mahakama.
..sasa tabia hizohizo wanakwenda nazo ktk kufanya maamuzi dhidi ya wawekezaji. lakini hawa wawekezaji hawana tabia za kinyonge-nyonge kama Watanzania wa kawaida. Pia wawekezaji wana option ya kwenda kutafuta haki zao nje ya nchi ambako viongozi hawana control au mamlaka.
You are assuming kuwa wanaotengeneza hiyo mikataba wana ujuzi wa hayo mambo which is not correct!! Tunapeleka watu kwenda kutayarisha mikataba na kuletewa kusainiwa mikataba iliyoandikwa katika lugha tusiyoielewa. Kuna mikataba imetiwa saini hapa ikiwa katika lugha ya MANDARIN! Unafikiri kweli hiyo mikataba itakuwa kwa faida yetu au ya Wachina?
Ile mikataba mingine ya madini iliyosainiwa huko nyuma watu tuliowakabidhi ile Kazi hawakuwa waaminifu na kwavile they were left not to account for their shortcomings kwa mfano kwenye MAKINIKIA basi wanaendeleza game lao!!