Mkuu nina imani kuwa Wewe na Magufuli picha zilikuwa haziendi kabisa na bila shaka una sababu zako binafsi kuliko Uhalisia.
Niseme tu kwamba sisi watu ni wepesi sana kulaumu matokeo wakati hawajui wala.hatutaki kujua chanzo kilicho sababisha matokeo hayo, iwe hata mpira wa miguu. Kazi ya manazi au mashabiki ni kulaumu ama kushangilia matokeo lakini sii maandalizi na utekelezaji wake.
Ni hivi mkuu, tatizo kubwa tulonalo Tanzania ni la KIMFUMO. Na tatizo linaanzia kutokuwa na Azimio la Kitaifa kama wakati wa Mwalimu. Azimio la Zanzibar lipo kimaandishi tu lakini halitumiki kiutawala haswa kwenye UWEKEZAJI. Kila rais anayeingia madarakani anakuja na mfumo wake hakuna restrictions za.kudumu.
Haya Makampuni ya nje yanakuja kuwekeza kutokana na sheria zetu butu. Huenda kusajikiwa (register) kwa address tu na wakapewa liseni. Ambayo huenda kutafuta Ama kufanya utafiti wa biahara hiyo. Hizi liseni zinapatikana kirahisi sana tena hata kwa njia za nyuma lakini halali (registered). Fedha yako tu.
Wapo matapeli na wapo Wawekezaji wa kweli ambao wote nia na dhanira yao ni KUCHUMA kilichopo kutokana na mfumo mbovu. Mfano mdogo chukulia Chalinze Cement ni kampuni ilosajiliwa lakini hawana kiwanda wala ofisi lkn wana liseni halali kabisa hivi sasa ni mjadala Bungeni
Kwa hiyo, mfumo wetu tunasajili Makampuni ya nje kibao tena kwa misifa lakini haya makampuni mengine ni hewa hawakuja kuwekeza hawana hata mitambo ya utafiti wala ni ya biashara ila kuna mchongo fulani.
Sasa inapokuja gundulika baadae tumeingizwa chooo cha kike kutokana na udanganyifu wa Shirika tunawanyang'anya liseni zao ama tunafuta mikataba yao. Kumbuka mkuu tofauti na Leo na wakati ule tunatawaliwa ni ndogo sana. Tulitawaliwa baada ya sisi kuwakaribisha Wageni hao kwa nia njema kabisa, lakini dhamira yao ni ile ile KUJA KUCHUMA nchi zetu na mafao wapeleke Makwao. Tofauti ni kwamba leo tunasema wanatulipa kodi lkn madini na faida yote ni mali yao. Na zinaenda nje.
Sasa anapotokea Kiongozi ambaye hataki kabisa rasilimali zetu ziwafaidhishe wageni badala ya sisi wenyewe kuwa hapo ndipo ngoma inapoanzia. Kumbuka Azimio la Zanzibar bado lilikuwa na azimio ya kummilikisha Mwananchi uwekezaji wowote japo kwa ubia usiopungua asilinia 51.
Tuliondoa sheeia hizo tukarahisisha sheria ili.kuvutia Wawekezaji na bahati mbaya sana sii wote walokuja kwa nia jema. Tumeona Mahoteli wakibadilisha majina kila baada ya miaka mitano ya nafuu ya kodi. Sii huko tu imefikia mpaka kwenye miradi mikubwa kuzidi kutqka nafuu ya kodi ilihali sisi hatuna share kabisa!
Binafsi nipo na Magu katika hili, naamini kabisa Wachimbaji wadogo wa madini Tanzania au Qlwakulima wetu, wavuvi wetu, Wafugaji wetu wana impact kubwa katika mendeleo ya Taufa hili kuliko haya makampuni ya nje. Sioni sababu kabisa ya kuvutia Wawekezaji wa nje ikiwa sii maswala ya uwekezaji kiwanda cha Tech! Kama cha magari, kumputa, simu au hata kusadiaha na kukata madini hapa hapa nchini.
j
Hivyo, kwa jinsi tunavyosajili makampuni ya nje kuja kuwekeza nchini ndivyo tunavyo jiweka katika hali mbaya zaidi ya kushtakiwa huko mbeleni. MIKATABA MIBOVU ndio xhanzo cha kesi hizi na sii maamuzi yetu kuvunja mikataba hiyo!
Naamini hakuna KILIMO kinachomshinda Mtanzania mpaka tulete mwekezaji kutoka nje - HAKUNA. Wala hakuna Madini tunayoweza kushindwa kuwekeza sisi wenyewe isipokuwa kwa hofu ya kuogopa kivuli chetu wenyewe.
Hii mikataba holela tunayoingia na Mashirika ya nje kwa kuondoa masharti ili kuwavutia ndio chanzo cha kesi za kesho! Unamvutia mwekezaji anayekuja kukuibia ati ajira? Kwani Mkoloni alikuwa hatupi ajira? Kwa nini tulitaka kumuondoa ikiwa wazee wetu waliajiriwa na Mkoloni?..