Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Nakiri sikujieleza vizuri na kueleweka nilichoandika hapo.

Ukiacha mstari wa kwanza ambao ni nje ya mada hii, maneno mengine yote nilikuwa ninakubaliana na hoja yako ulivyoieleza hapo.

Huo mstari wa kwanza unahusu uelewa wangu kwako kuhusu mambo mbalimbali tuliyowahi kukutana na kuyajadili humu JF, mengine tukikubaliana, na mengine tukipishana mitizamo. Hili ni jambo la kawaida.

Kuhusu hizi kesi, ni kama umenistua akili kuanza kujiuliza juu ya nini ambacho huwa tunashtakiwa juu yake na mara nyingi kushindwa kujitetea. Sijui kama kuna mwekezaji yeyote aliyekuwa tayari kawekeza na mgodi wake ukanyang'anywa na serikali na yeye kuamua kwenda mahakamani kujitetea juu ya hilo.

Kwa uelewa wangu sasa, baada ya kukusoma ni kuwa hawa watu wanaotushtaki hawana madini yoyote ambayo walishayagundua, bali ni watu (Kampuni) zilizopewa eneo kutafuta madini. Ambacho bado pia sikijui, ni kama wanapopewa maeneo hayo wanayotakiwa kupewa madini kuna makubaliano yanayoifunga serikali kutoyadai tena maeneo hayo ikiyahitaji. Je hii mikataba masharti yake yapoje?
Hawa watu hupewa umiliki wa eneo husika; kwa muda gani? Ni gharama zipi hutakiwa kuzikamilisha wakati wakitafuta madini hayo. Ninaelewa pia baadhi ya maeneo hayo ni makazi ya wananchi ambao huendelea na shughuli zao kama kawaida.
Sasa huyu mwekezaji anayo haki gani juu ya eneo kama hilo!
Mikataba inafanana na ile wa yule jamaa wwkala ww ndege aliyetaka kutupiga 100b na raisi wa nchi akasishi kusema mtupishe mambo yakaisha kirahisi hivyo
 
Kwa hiyo anawasema kima Kabudi,ossolo na genge lake?
 
ukweli usiopingika ni kwamba, Waalimu wa vyuo walio wengi hawajui practice ya kazi huko maofisi ya serikali, wao wanajua kufundisha basics tu na ni theories kwa wanafunzi. kwa maana hiyo, uwezo wa mwalimu wa chuo hata kama ni profesa ni sawa na uwezo alionao mwajiriwa fresh from school anayehitaji afanye kazi kwanza kujua mhimili wa ajira yake na namna mambo yanavyofanyika. kwenye suala la sheria, huwezi kumlinganisha kabudi na mtu mzoefu wa sheria kwenye ofisi ya Attorney General au hata wizara ya katiba. hao ndio walitakiwa wapewe nyadhifa za kabudi na wengine waliokuwa wamemzunguka mwendazake. shida mwendazake alikariri kuwa mtu mwenye akili ni mwenye PHD au professa. kumbe hao kile mmoja amespecialise kwenye eneo fulani tu kwenye utendaji kazi wale watu kwenye wizara na vitengo vya serikali waliofanya kazi walau miaka 10 ndio wangemsaidia kuliko hao. alipotoshwa sana, sote tunakumbuka suala la makinikia na barrick; kama kuna miaka watanzania hatutakiwi kuja kuirudia kiutendaji ni miaka ya awamu ya mwendazake.
 
Ili tuendelee, tunatakiwa kuwa serious na maslahi ya nchi kama zilivyo nchi za ulaya. ulaya cheza na vitu vyoote lakini sio pesa ya umma, utakwisha. hapa kwetu mtu anacheza na pesa ya umma na bado yupo kazini, tunataka kumfurahisha nani? mbona kama ni wapiga kura ukifukuza hawa wezi na wararushwa ndio utapata wapiga kura wengi raia huko mtaani wataona unafanya mambo ya maana? tusilegeze sana kamba ama la labda ni kwasababu na sisi tunakula.
 
Muungeni mkono lissu awasaidia sana sisi wengine hatupo tanzania tulifukuzwa kwa sababu ya kuelimisha na kusema ukweli .
Kwa nini unamahaba na mwanaume mwenzio hivyo .Lisu anarikodi gani ya hayo mambo
 
..wasomi walimuendekeza Magufuli na kumwambia mambo anayopenda kusikia, badala ya kumwambia ukweli na uhalisia.

..matokeo ya ushauri huo wa " kishujaa" serikali imeburuzwa mahakamani mara kadhaa, imeshindwa kesi, na kulazimika kuingia hasara ya kuwalipa wawekezaji fidia.
Mikataba aliyosain mkapa na kikwete alishauriwa na nani
 
Mkuu nina imani kuwa Wewe na Magufuli picha zilikuwa haziendi kabisa na bila shaka una sababu zako binafsi kuliko Uhalisia.

Niseme tu kwamba sisi watu ni wepesi sana kulaumu matokeo wakati hawajui wala.hatutaki kujua chanzo kilicho sababisha matokeo hayo, iwe hata mpira wa miguu. Kazi ya manazi au mashabiki ni kulaumu ama kushangilia matokeo lakini sii maandalizi na utekelezaji wake.

Ni hivi mkuu, tatizo kubwa tulonalo Tanzania ni la KIMFUMO. Na tatizo linaanzia kutokuwa na Azimio la Kitaifa kama wakati wa Mwalimu. Azimio la Zanzibar lipo kimaandishi tu lakini halitumiki kiutawala haswa kwenye UWEKEZAJI. Kila rais anayeingia madarakani anakuja na mfumo wake hakuna restrictions za.kudumu.

Haya Makampuni ya nje yanakuja kuwekeza kutokana na sheria zetu butu. Huenda kusajikiwa (register) kwa address tu na wakapewa liseni. Ambayo huenda kutafuta Ama kufanya utafiti wa biahara hiyo. Hizi liseni zinapatikana kirahisi sana tena hata kwa njia za nyuma lakini halali (registered). Fedha yako tu.

Wapo matapeli na wapo Wawekezaji wa kweli ambao wote nia na dhanira yao ni KUCHUMA kilichopo kutokana na mfumo mbovu. Mfano mdogo chukulia Chalinze Cement ni kampuni ilosajiliwa lakini hawana kiwanda wala ofisi lkn wana liseni halali kabisa hivi sasa ni mjadala Bungeni

Kwa hiyo, mfumo wetu tunasajili Makampuni ya nje kibao tena kwa misifa lakini haya makampuni mengine ni hewa hawakuja kuwekeza hawana hata mitambo ya utafiti wala ni ya biashara ila kuna mchongo fulani.

Sasa inapokuja gundulika baadae tumeingizwa chooo cha kike kutokana na udanganyifu wa Shirika tunawanyang'anya liseni zao ama tunafuta mikataba yao. Kumbuka mkuu tofauti na Leo na wakati ule tunatawaliwa ni ndogo sana. Tulitawaliwa baada ya sisi kuwakaribisha Wageni hao kwa nia njema kabisa, lakini dhamira yao ni ile ile KUJA KUCHUMA nchi zetu na mafao wapeleke Makwao. Tofauti ni kwamba leo tunasema wanatulipa kodi lkn madini na faida yote ni mali yao. Na zinaenda nje.

Sasa anapotokea Kiongozi ambaye hataki kabisa rasilimali zetu ziwafaidhishe wageni badala ya sisi wenyewe kuwa hapo ndipo ngoma inapoanzia. Kumbuka Azimio la Zanzibar bado lilikuwa na azimio ya kummilikisha Mwananchi uwekezaji wowote japo kwa ubia usiopungua asilinia 51.

Tuliondoa sheeia hizo tukarahisisha sheria ili.kuvutia Wawekezaji na bahati mbaya sana sii wote walokuja kwa nia jema. Tumeona Mahoteli wakibadilisha majina kila baada ya miaka mitano ya nafuu ya kodi. Sii huko tu imefikia mpaka kwenye miradi mikubwa kuzidi kutqka nafuu ya kodi ilihali sisi hatuna share kabisa!

Binafsi nipo na Magu katika hili, naamini kabisa Wachimbaji wadogo wa madini Tanzania au Qlwakulima wetu, wavuvi wetu, Wafugaji wetu wana impact kubwa katika mendeleo ya Taufa hili kuliko haya makampuni ya nje. Sioni sababu kabisa ya kuvutia Wawekezaji wa nje ikiwa sii maswala ya uwekezaji kiwanda cha Tech! Kama cha magari, kumputa, simu au hata kusadiaha na kukata madini hapa hapa nchini.
j
Hivyo, kwa jinsi tunavyosajili makampuni ya nje kuja kuwekeza nchini ndivyo tunavyo jiweka katika hali mbaya zaidi ya kushtakiwa huko mbeleni. MIKATABA MIBOVU ndio xhanzo cha kesi hizi na sii maamuzi yetu kuvunja mikataba hiyo!

Naamini hakuna KILIMO kinachomshinda Mtanzania mpaka tulete mwekezaji kutoka nje - HAKUNA. Wala hakuna Madini tunayoweza kushindwa kuwekeza sisi wenyewe isipokuwa kwa hofu ya kuogopa kivuli chetu wenyewe.

Hii mikataba holela tunayoingia na Mashirika ya nje kwa kuondoa masharti ili kuwavutia ndio chanzo cha kesi za kesho! Unamvutia mwekezaji anayekuja kukuibia ati ajira? Kwani Mkoloni alikuwa hatupi ajira? Kwa nini tulitaka kumuondoa ikiwa wazee wetu waliajiriwa na Mkoloni?..
Hiyo chalinze cement limited ni kielelezo cha serikali yetu isivyo makin failed state. Kama sio huu mparanganyiko wa twiga cement na twiga cement .hiyo chalinze cement Ltd ingekuwa ipo na inafanya kazi .na aina hii ya makampuni hasa kipindi hiki cha samia ndo yanaongezeka kama wawekazaji .na waziri anasimama anasema wawekeAji wameongezaka .poor Tanzania
 
Na kuhusu report ya Magufuli. Mkuu kamchezo kamechezwa baada ya kifo chake. Kila.kitu tunaambiwa sii kweli ilihali rais alitangaza wazi wazi mbele ya Watanzania walichokubaliana. Leo mnabadilishiwa maneno na kuambiwa haikuwa hivyo. Kila mtu mwoga kusema ukweli. Sioni ajabu UNAFIKI wa.Watanzania maana ni moja ya mila zetu. Hii ni sawa na Familia moja baada ya kufa mzazi wao wanadai ile wosia (WILL) haikuwa halali...
True watanzania wanafiki sana wapo hadi leo kila kitu wwnafsnya kumkomoa marehemu
 
Wapi hizo kesi zinasema wamenyang'anywa kwa sababu ya kutoendeleza migodi?

Umeambiwa wamefutiwa leseni sababu hawakucomply na regulations mpya za 2018.

Kingine issue sio JPM, mbona na yeye aliweka kifungu cha kwamba mashtaka yote yasikilizwe na mahakama za ndani ila mabeberu walipokataa ikabidi wafute hicho kipengele.
Nani kakuambia
 
Mikataba inafanana na ile wa yule jamaa wwkala ww ndege aliyetaka kutupiga 100b na raisi wa nchi akasishi kusema mtupishe mambo yakaisha kirahisi hivyo
Huyu anao mtindo wake wa kuwahujumu waTanzania, mtindo unaoudhi kwelikweli. Anatoa vimanenoneno tu visivyokuwa na maana yoyote mradi asikike, huku hafanyi kitu.
 
Uanjua sheria ya ardhi lakini tena kwa mujibu wa katiba huyo mwekezaji alikuwa anamwekeza nini mpaka ardhi ikachukualiwa .mbona sheria ipo wazi tu kama haujaendeleza ardhi .inachukuliwa .
Ni kweli... Sasa wanasheria wetu mbona wameshindwa kesi?

Unakuta unampa mwekezaji ardhi na mnapeana mikataba... Lakini kipengele cha kutokuendelezwa hakiwekwi makusudi...
Mkienda arbitration za kimataifa tunapigwa
 
Bana wee kaondoka na covid au moyo? Tanzania walochanja ni mil. 3 kati ya mil.60 unataka kunambia hao wengine woote wasiochanja walikuwa wajinga? Mbona wapo wanadunda mtaani wazimaaa!

Kwanza walochanja kila siku wagonjwa! Tena nasikia wanawake ndio kabisa hata hedhi hazina mpango zinapotea. Mimba za kuhesabu..
Hii akaunti ipo hacked mkuu? Mbona sio mkandara yule wa 2013? Kwamba una data za wote waliochanja kuwa hawaoni hedhi? Mimi wadogo zangu wawili wamechanja pamoja na mzee wangu huko bushi ila sijaona aliye na tatizo lolote mwaka wa tatu Sasa. Hizi mis information unazitoa wapi?

Kingine hii tabia ya "watu wanadunda" mnaitoa wapi? Mtu kutokujua status yake kiafya haimaanishi ni mzima. Mfano mtu ana ukimwi ila hafahamu ila sababu anadunda tu na hatumii ARV basi ni shujaa? Kwa mentality hii utakuta watu wanatembea na magonjwa ya kutisha alafu mwisho wa siku wakifa kwa ghafla tunaanza sema ni hujuma za wazungu!!

So low from a GT of your calibre
 
Hii akaunti ipo hacked mkuu? Mbona sio mkandara yule wa 2013? Kwamba una data za wote waliochanja kuwa hawaoni hedhi? Mimi wadogo zangu wawili wamechanja pamoja na mzee wangu huko bushi ila sijaona aliye na tatizo lolote mwaka wa tatu Sasa. Hizi mis information unazitoa wapi?

Kingine hii tabia ya "watu wanadunda" mnaitoa wapi? Mtu kutokujua status yake kiafya haimaanishi ni mzima. Mfano mtu ana ukimwi ila hafahamu ila sababu anadunda tu na hatumii ARV basi ni shujaa? Kwa mentality hii utakuta watu wanatembea na magonjwa ya kutisha alafu mwisho wa siku wakifa kwa ghafla tunaanza sema ni hujuma za wazungu!!

So low from a GT of your calibre
Hahahaha, yule yule umjuaye. Nitakujibu kwa wepesi kabisa. Nina mke na watoto watatu wa kike ambao wote wana marafiki wa kike. Malalamiko yao nayasikia na hakuna wa kuwasemea.

Ukimwi hauna chanjo, hizo ARV ni kuzuia tu kusambaa lakini mgonjwa wa Ukimwi anao na anaweza ambukiza. Covid hata kama umechoma kinga bado unaweza kuipata na ukafariki. Hoja yangu ni Kinga sio Covid -19 (SARS)

Kuhusu kudunda mkuu wangu sote tunajua Covid haina dawa wala haicheleweshi. Kama watu mil. 60 wapo hai leo hii baada ya miaka mitatu. Utasemaje? Kudra ya Mungu? Sijasema ugonjwa haupo ila nasema hivi siamini hizo kinga zao.

Kifupi, Chanjo za Covid zilikuwa biashara na wao wanajua maana mpaka leo hii zipo booster 5 yaani hata kama ulichanja zile 2 au 3 bado haupo salama. Na hii ya 5 pia bado wanasema sio guarantee. China wamepigana na Ugonjwa huu kwa kila mbinu mpaka wamerudi kwenye virutubishi vya kienyeji. Ina fact wao na Japan wametumia zaidi mimea ya asili kuzuia SARs maana Covid sio geni kwao.

Hao Wasomi wenyewe walichanganyikiwa wakalazimishwa kukubali. Marekani yenyewe kuna States nyingi tu watu hawakuchoma wala lazima kuvaa barakoa, Texas mojawapo! Je, uliambiwa na vyombo vya habari? Hiyo Marekani ni state ngapi hazikujifungia? Na kwa nini wao watu walisafiri toka state moja kwenda nyingine bila chanjo?

Nasema vitu kwa sababu navijua laa siwezi kuchukua maneno ya mtu au watu. Huwa nina mitazamo yangu kwa yale nilopitia, hata kama itawakwaza wengine lakini ninao Uhuru wa kujieleza - Ni haki yangu.
 
Kitila atokee aseme alimaanisha nini, zaidi ya hapo hizi Spinning ya neno "Shujaa" linachafua zaidi. Kwani naamini haikuwa dhamira yake na wala hakuwa anambeza Hayati Raisi.

Uje uwasaidie wenzetu na Lugha.
 
Hii kuna mapunga yanayo amini kauli hizi!, huyu kitila si ndiyo alirudisha kadi ya ACT na kulamba kopo asali uwaziri, ujue hawa wanasiasa wanatuchezea sana akili. Ingekuwa amri yangu ni kuwatandika bakora kiumbe yeyote anayejiita mwanasiasa. Nina hasira nao hawa viumbe ☹️☹️☹️
 
Kwa nin tusipambane na hao Waliongia mkataba wa kihuni kwanza
Una akili Sana Mkuu. Tulitakiwa kuanza nao. Lisu alimwambia magu walioingia mkataba wapo. Tuanze nao Kama kweli tupo na Nia ya dhati kukomesha walaji serikalini
 
..wasomi walimuendekeza Magufuli na kumwambia mambo anayopenda kusikia, badala ya kumwambia ukweli na uhalisia.

..matokeo ya ushauri huo wa " kishujaa" serikali imeburuzwa mahakamani mara kadhaa, imeshindwa kesi, na kulazimika kuingia hasara ya kuwalipa wawekezaji fidia.
Madili ya watu tu sawa tu kama vile ndege ilivyowahi kukamtwa South Africa
 
Back
Top Bottom