PostGE2025 Prof. Kitila: Serikali yatangaza mikakati 8 ya kupanua ajira kwa vijana

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo ametangaza mikakati mahsusi nane ya Serikali katika kuvutia uwekezaji na kupanua fursa za ajira kwa vijana nchini.

Mikakati hiyo imetangazwa leo, Novemba 28, 2025 mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Watoa Huduma na Kongamano la Uwekezaji lililoratibiwa TISEZA.

1764328025437.webp

Katika hotuba yake, Waziri amesema Serikali imejipanga kuongeza ushiriki wa vijana katika sekta ya uwekezaji kwa kuweka mifumo, miundombinu na programu maalum zitakazowawezesha kuanzisha na kukuza uwekezaji wao wenyewe.

Miongoni mwa mikakati hiyo nane ni serikali kuanzisha Kituo Maalum cha Kuhudumia na Kuwezesha Wawekezaji Vijana (Youth Investors Resource Centre). Kituo hicho kitatoa mafunzo, usaidizi wa uwezeshaji na huduma mbalimbali kwa vijana wanaotaka kuwekeza. Kitakuwa Mabibo, Dar es Salaam, huku kukiwa na uwakilishi katika ofisi za TISEZA za mikoa na kanda. Waziri amesema anatarajia kukizindua kituo hicho kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Aidha Prof. Kitila amesema Serikali inaanzisha programu maalum ya kuwezesha vijana kubuni na kuanzisha uwekezaji wa viwanda katika maeneo mbalimbali nchini. Katika mpango huo, maeneo maalum yametengwa kwa ajili ya vijana waliomaliza vyuo vikuu na vyuo vya ufundi ili waweze kuwekeza.

“Tunatenga maeneo yafuatayo maalum kwa uwekezaji utakaofanywa na vijana Dodoma (Nala, Ekari 100), Pwani (Kwala, Ekari 20), Mara (Bunda, Ekari 100), Ruvuma (Songea, Ekari 100) na Bagamoyo (Pwani, Ekari 20). Programu hii pia nitaizindua Pamoja na Kituo Cha Kuwezesha Vijana kabla ya mwisho wa mwaka huu”, ameeleza Prof. Kitila.

Programu hii itahusisha mafunzo, upatikanaji wa ardhi, uunganishwaji na wauzaji wa mitambo na malighafi, pamoja na kuunganisha vijana na benki zinazoshirikiana na TISEZA zikiwemo Azania Bank, TCB na CRDB.

Mkakati mwingine wa serikali ni kusogeza huduma za TISEZA katika kila mkoa ifikapo mwaka 2028 ambapo kila mkoa utakuwa na kituo maalum cha kutangaza na kuwezesha uwekezaji, hatua ambao itatekelezwa kwa ushirikiano na TAMISEMI.
 
Vijana hata wanazitaka hizo ajira basii?😀

Hivi hawa thinking capability yao imepungua kiasi hiko.

Hauwezi kutibu malaria kwa kunywa dawa za minyoo.

Hebu wamsikilize huyu mama hapa chini:

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo ametangaza mikakati mahsusi nane ya Serikali katika kuvutia uwekezaji na kupanua fursa za ajira kwa vijana nchini.

Mikakati hiyo imetangazwa leo, Novemba 28, 2025 mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Watoa Huduma na Kongamano la Uwekezaji lililoratibiwa TISEZA.

View attachment 3508831

Katika hotuba yake, Waziri amesema Serikali imejipanga kuongeza ushiriki wa vijana katika sekta ya uwekezaji kwa kuweka mifumo, miundombinu na programu maalum zitakazowawezesha kuanzisha na kukuza uwekezaji wao wenyewe.

Miongoni mwa mikakati hiyo nane ni serikali kuanzisha Kituo Maalum cha Kuhudumia na Kuwezesha Wawekezaji Vijana (Youth Investors Resource Centre). Kituo hicho kitatoa mafunzo, usaidizi wa uwezeshaji na huduma mbalimbali kwa vijana wanaotaka kuwekeza. Kitakuwa Mabibo, Dar es Salaam, huku kukiwa na uwakilishi katika ofisi za TISEZA za mikoa na kanda. Waziri amesema anatarajia kukizindua kituo hicho kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Aidha Prof. Kitila amesema Serikali inaanzisha programu maalum ya kuwezesha vijana kubuni na kuanzisha uwekezaji wa viwanda katika maeneo mbalimbali nchini. Katika mpango huo, maeneo maalum yametengwa kwa ajili ya vijana waliomaliza vyuo vikuu na vyuo vya ufundi ili waweze kuwekeza.

“Tunatenga maeneo yafuatayo maalum kwa uwekezaji utakaofanywa na vijana Dodoma (Nala, Ekari 100), Pwani (Kwala, Ekari 20), Mara (Bunda, Ekari 100), Ruvuma (Songea, Ekari 100) na Bagamoyo (Pwani, Ekari 20). Programu hii pia nitaizindua Pamoja na Kituo Cha Kuwezesha Vijana kabla ya mwisho wa mwaka huu”, ameeleza Prof. Kitila.

Programu hii itahusisha mafunzo, upatikanaji wa ardhi, uunganishwaji na wauzaji wa mitambo na malighafi, pamoja na kuunganisha vijana na benki zinazoshirikiana na TISEZA zikiwemo Azania Bank, TCB na CRDB.

Mkakati mwingine wa serikali ni kusogeza huduma za TISEZA katika kila mkoa ifikapo mwaka 2028 ambapo kila mkoa utakuwa na kituo maalum cha kutangaza na kuwezesha uwekezaji, hatua ambao itatekelezwa kwa ushirikiano na TAMISEMI.
Aha haha mbona kwenye irani haikuwepo?
 
Hatutaki kuhutibiwa tunataka kusikilizwa
Genius Man, kusikilizwa kunahitaji mtu azungumze kwa kuweka maneno mahali pake. Sidhani kama kuna mtu mwenye akili asiyefahamu jinsi dunia ya sasa inavyoendeshwa—ni ‘corporates’ ndizo zinazoamua mengi na ndizo zinazofanya kazi kubwa.
Kwa nini basi tuwageuze ndugu zetu, watoto wetu na rafiki zetu kuwa kama vifaa vya kufikia malengo yetu?
Bila shaka sote tutakufa, lakini angalau tujitahidi tusije tukawa sisi ndiyo sababu ya kifo cha mwingine.
Kama ilivyo, nazi haiwezi kushindana na jiwe; vikigongana, nazi ndiyo itakayopasuka.
 
wanaosababisha vifo ni polisi sio sisi sijui unatumia nini kufikiri yani mimi niwa hamasishe watu kupinga utekaji na mauwaji alafu niambiwe nauwa ?

Hili suala la kupinga mifumo ya kipumbavu ni wosia wa nyerere mwenyewe sio mimi vijana wanatakiwa wawe waasi dhidi ya wajinga.
 
Hatua walau. Lakini hiyo mipango itawasaidia tu vijana wenye connections na wasomi. Vipi majority walio wengi?
 
wanaosababisha vifo ni polisi sio sisi sijui unatumia nini kufikiri yani mimi niwa hamasishe watu kupinga utekaji na mauwaji alafu niambiwe nauwa ?

Hili suala la kupinga mifumo ya kipumbavu ni wosia wa nyerere mwenyewe sio mimi vijana wanatakiwa wawe waasi dhidi ya wajinga.
Kuhamasisha kwa kupinga bila kuunguza moto mali za watu na kufanya uharibifu mbona hiyo ipo poa, watu wengi wangeunga mkono juhudi zenu, lakini kitendo cha kuleta taharuki za uvunjifu wa amani kwa kuchoma moto vitu mbalimbali amabvyo kama wale vijana wangeachiwa nadhani nchi hadi leo watu wangekuwa majumbani mwao na wengi wangepoteza uhai kwa kukosa mahitaji muhimu.

Hao wazee wetu wakina Nyerere wangekuwa na akili kama za vijana wetu basi wasingetajwa jinsi wanavyotajwa, pamoja walikuwa vijana lakini walikuwa na busara, hekima na maarifa.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo ametangaza mikakati mahsusi nane ya Serikali katika kuvutia uwekezaji na kupanua fursa za ajira kwa vijana nchini.

Mikakati hiyo imetangazwa leo, Novemba 28, 2025 mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Watoa Huduma na Kongamano la Uwekezaji lililoratibiwa TISEZA.

View attachment 3508831

Katika hotuba yake, Waziri amesema Serikali imejipanga kuongeza ushiriki wa vijana katika sekta ya uwekezaji kwa kuweka mifumo, miundombinu na programu maalum zitakazowawezesha kuanzisha na kukuza uwekezaji wao wenyewe.

Miongoni mwa mikakati hiyo nane ni serikali kuanzisha Kituo Maalum cha Kuhudumia na Kuwezesha Wawekezaji Vijana (Youth Investors Resource Centre). Kituo hicho kitatoa mafunzo, usaidizi wa uwezeshaji na huduma mbalimbali kwa vijana wanaotaka kuwekeza. Kitakuwa Mabibo, Dar es Salaam, huku kukiwa na uwakilishi katika ofisi za TISEZA za mikoa na kanda. Waziri amesema anatarajia kukizindua kituo hicho kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Aidha Prof. Kitila amesema Serikali inaanzisha programu maalum ya kuwezesha vijana kubuni na kuanzisha uwekezaji wa viwanda katika maeneo mbalimbali nchini. Katika mpango huo, maeneo maalum yametengwa kwa ajili ya vijana waliomaliza vyuo vikuu na vyuo vya ufundi ili waweze kuwekeza.

“Tunatenga maeneo yafuatayo maalum kwa uwekezaji utakaofanywa na vijana Dodoma (Nala, Ekari 100), Pwani (Kwala, Ekari 20), Mara (Bunda, Ekari 100), Ruvuma (Songea, Ekari 100) na Bagamoyo (Pwani, Ekari 20). Programu hii pia nitaizindua Pamoja na Kituo Cha Kuwezesha Vijana kabla ya mwisho wa mwaka huu”, ameeleza Prof. Kitila.

Programu hii itahusisha mafunzo, upatikanaji wa ardhi, uunganishwaji na wauzaji wa mitambo na malighafi, pamoja na kuunganisha vijana na benki zinazoshirikiana na TISEZA zikiwemo Azania Bank, TCB na CRDB.

Mkakati mwingine wa serikali ni kusogeza huduma za TISEZA katika kila mkoa ifikapo mwaka 2028 ambapo kila mkoa utakuwa na kituo maalum cha kutangaza na kuwezesha uwekezaji, hatua ambao itatekelezwa kwa ushirikiano na TAMISEMI.
Yamepaniki shenzy🚮🚮
 
Kuhamasisha kwa kupinga bila kuunguza moto mali za watu na kufanya uharibifu mbona hiyo ipo poa, watu wengi wangeunga mkono juhudi zenu, lakini kitendo cha kuleta taharuki za uvunjifu wa amani kwa kuchoma moto vitu mbalimbali amabvyo kama wale vijana wangeachiwa nadhani nchi hadi leo watu wangekuwa majumbani mwao na wengi wangepoteza uhai kwa kukosa mahitaji muhimu.

Hao wazee wetu wakina Nyerere wangekuwa na akili kama za vijana wetu basi wasingetajwa jinsi wanavyotajwa, pamoja walikuwa vijana lakini walikuwa na busara, hekima na maarifa.
Umetoka kuniambia mimi kuhamasisha mabadiliko heti nauwa vijana sasa umeamia kwenye uharibifu wa vitu. vipi uharibifu wa uchaguzi wa kuiba kura uliofanywa na serikali haramu ? huu ndio hatari zaidi kwa sababu huna akili huwezi kuelewa.

Usihoji uharibifu wa vitu wakati watu wamejisimika madarakani kwa kuiba haki za raia
 
Waziri amesema Serikali imejipanga kuongeza ushiriki wa vijana katika sekta ya uwekezaji kwa kuweka mifumo, miundombinu na programu maalum zitakazowawezesha kuanzisha na kukuza uwekezaji wao wenyewe.
Sometimes sitaki kuwasikiliza maprofesa km hawa..
 
Back
Top Bottom