PostGE2025 Prof. Kitila: Serikali yatangaza mikakati 8 ya kupanua ajira kwa vijana

PostGE2025 Prof. Kitila: Serikali yatangaza mikakati 8 ya kupanua ajira kwa vijana

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kuhamasisha kwa kupinga bila kuunguza moto mali za watu na kufanya uharibifu mbona hiyo ipo poa, watu wengi wangeunga mkono juhudi zenu, lakini kitendo cha kuleta taharuki za uvunjifu wa amani kwa kuchoma moto vitu mbalimbali amabvyo kama wale vijana wangeachiwa nadhani nchi hadi leo watu wangekuwa majumbani mwao na wengi wangepoteza uhai kwa kukosa mahitaji muhimu.

Hao wazee wetu wakina Nyerere wangekuwa na akili kama za vijana wetu basi wasingetajwa jinsi wanavyotajwa, pamoja walikuwa vijana lakini walikuwa na busara, hekima na maarifa.
D9.. kakumbatiane mama yako km kifaranga cha kuku..
 
Acheni ujinga watanzania, ccm wako madarakani tangu uhuru, leo ndio wawe na mkakati wa ajira kwa vijana, mnafanywa mipumbavu nanyi mnawasikiliza?

Vijana jitokezeni D9 tuongee lugha wanayo isikia na kuielewa kwa sauti kubwa.
 
Kuna zile zilitangazwa kabla ya uchaguzi, deadline ikaja mtandao umezimwa.
 
Huu mpango wa prof unafanana na ule mpango wa Bashe wa BBT, huu mpango utafeli vilevile, wanatudanganya kutuelndeleza vijana kwa ahadi za kipumbavu na ubongo! Bullshit Programs from Bullshit Prof
 
D9.. kakumbatiane mama yako km kifaranga cha kuku..
Wafikirie ndugu zetu waliyotangulia mbele ya haki, huenda wewe ukaja tena kwenye JF na kuandika unachotaka kuandika lakini kuna wenzenu ambao ndiyo watakaotolewa kafara.
Kila mtu atakufa lakini tafadhali usiwe sababu ya mwingine afe kwa maslahi yako.
 
Wafikirie ndugu zetu waliyotangulia mbele ya haki, huenda wewe ukaja tena kwenye JF na kuandika unachotaka kuandika lakini kuna wenzenu ambao ndiyo watakaotolewa kafara.
Kila mtu atakufa lakini tafadhali usiwe sababu ya mwingine afe kwa maslahi yako.
December 9 ni siku ya Uhuru wa Tanganyika.
 
December 9 ni siku ya Uhuru wa Tanganyika.
Hakuna mtu asiyejua kuwa 9 December ni siku ya uhuru wa Tanganyika. Basi isiwe ndiyo siku itakayoandikwa kwenye kaburi lako au la mwingine mwenye kutaka kuandamana kama tarehe ya kufariki.
 
Kuhamasisha kwa kupinga bila kuunguza moto mali za watu na kufanya uharibifu mbona hiyo ipo poa,
Mkuu,
Labda wewe ni mgeni. Wameshafanya hivyo mara nyingi sana lakini wanaishia kutekwa na kuuawa na watawala.

Ukiona mtu anavunja mlango wake usifikiri ni mjinga, Inawezekana funguo imepotea au imeharibika au kitasa ni kibovu
 
Hakuna mtu asiyejua kuwa 9 December ni siku ya uhuru wa Tanganyika. Basi isiwe ndiyo siku itakayoandikwa kwenye kaburi lako au la mwingine mwenye kutaka kuandamana kama tarehe ya kufariki.
Na iwe hivyo watu washakunywa maji ya bendera ya Tanganyika hakuna kurudi nyuma.. D9
 
Mafisadi, watekaji, wauaji, wafiraji wa ccm
Hizo ni tuhuma na shutuma ambazo kama zikithibitika basi zitampeleka mwenye kutuhumiwa kifungoni, lakini wapo wapi hao watuhumiwa?
Mwamba kwenye hiyo video anatamka wazi wazi kuhusu uasi unafikiri hana cha kujibu kwenye hizo mahakama za sheria?
 
Hatua walau. Lakini hiyo mipango itawasaidia tu vijana wenye connections na wasomi. Vipi majority walio wengi?
Vijana wengi wa vijijini ndio wanaimbishwa amani na wanaitikia kama wajinga, acha hawa wa mjini walioamua kuandamana wapate fursa baada ya kumwaga damu.
 
Vijana wengi wa vijijini ndio wanaimbishwa amani na wanaitikia kama wajinga, acha hawa wa mjini walioamua kuandamana wapate fursa baada ya kumwaga damu.
Ndugu yangu, fursa gani tunayoweza kusema zipo baada ya maandamano? Au ni biashara za kuuza majeneza?
Kwanini watu hupenda kuzungumza mambo ambayo wao wenyewe hawana hata nia ya kuyatekeleza?

Hebu tujiulize kwa uaminifu: kweli mtu mzima unaweza kumpeleka mwanao, ndugu yako au rafiki yako kwenye maandamano ambayo mizizi yake ni uasi, na ambako kuna uwezekano halisi wa kufyatuliwa risasi na kupoteza uhai?
Je, tumefika hatua ya kuwa kwenye ajenda ya kupunguzana tu kwa sababu ‘tumezidi’?

Kwa nchi kama yetu, haya mambo yanaweza kufikiwa kwa mazungumzo, busara na njia za kistaarabu. Tusidanganyike na yaliyotokea Bangladesh, Nepal au Guinea-Bissau tukadhani kuwa mwelekeo huo unaweza kutokea nyumbani. Hapana—tujue mazingira yetu na historia yetu, na tulinde amani ambayo tunaitegemea sote.

Baada ya mapinduzi nini kitatokea? Ni ujaji wa sampuli mpya tu ya wanufaika wachache wakati wengi watakuwa kama tulivyokuwa.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo ametangaza mikakati mahsusi nane ya Serikali katika kuvutia uwekezaji na kupanua fursa za ajira kwa vijana nchini.

Mikakati hiyo imetangazwa leo, Novemba 28, 2025 mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Watoa Huduma na Kongamano la Uwekezaji lililoratibiwa TISEZA.

View attachment 3508831

Katika hotuba yake, Waziri amesema Serikali imejipanga kuongeza ushiriki wa vijana katika sekta ya uwekezaji kwa kuweka mifumo, miundombinu na programu maalum zitakazowawezesha kuanzisha na kukuza uwekezaji wao wenyewe.

Miongoni mwa mikakati hiyo nane ni serikali kuanzisha Kituo Maalum cha Kuhudumia na Kuwezesha Wawekezaji Vijana (Youth Investors Resource Centre). Kituo hicho kitatoa mafunzo, usaidizi wa uwezeshaji na huduma mbalimbali kwa vijana wanaotaka kuwekeza. Kitakuwa Mabibo, Dar es Salaam, huku kukiwa na uwakilishi katika ofisi za TISEZA za mikoa na kanda. Waziri amesema anatarajia kukizindua kituo hicho kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Aidha Prof. Kitila amesema Serikali inaanzisha programu maalum ya kuwezesha vijana kubuni na kuanzisha uwekezaji wa viwanda katika maeneo mbalimbali nchini. Katika mpango huo, maeneo maalum yametengwa kwa ajili ya vijana waliomaliza vyuo vikuu na vyuo vya ufundi ili waweze kuwekeza.

“Tunatenga maeneo yafuatayo maalum kwa uwekezaji utakaofanywa na vijana Dodoma (Nala, Ekari 100), Pwani (Kwala, Ekari 20), Mara (Bunda, Ekari 100), Ruvuma (Songea, Ekari 100) na Bagamoyo (Pwani, Ekari 20). Programu hii pia nitaizindua Pamoja na Kituo Cha Kuwezesha Vijana kabla ya mwisho wa mwaka huu”, ameeleza Prof. Kitila.

Programu hii itahusisha mafunzo, upatikanaji wa ardhi, uunganishwaji na wauzaji wa mitambo na malighafi, pamoja na kuunganisha vijana na benki zinazoshirikiana na TISEZA zikiwemo Azania Bank, TCB na CRDB.

Mkakati mwingine wa serikali ni kusogeza huduma za TISEZA katika kila mkoa ifikapo mwaka 2028 ambapo kila mkoa utakuwa na kituo maalum cha kutangaza na kuwezesha uwekezaji, hatua ambao itatekelezwa kwa ushirikiano na TAMISEMI.
Watu wa aina ya huyu Kikaragosi
 
Back
Top Bottom