Prof. Kitila: Tanzania haitayumbishwa kwa sababu ya mabeberu kutunyima misaada, labda watafute vikwazo vingine

Prof. Kitila: Tanzania haitayumbishwa kwa sababu ya mabeberu kutunyima misaada, labda watafute vikwazo vingine

WAAMBIE watu Kwanini mmenyimwa misaada na hao mnaowaita MABEBERU??

Kwanini mnapopewa pesa hamsemi MABEBERU wametuchangia kiasi hiki?? Wanapowanyima mnabadili jina eti MABEBERU!😄😄😄
Kwani kupewa lazima?
 
Halafu wanakwambia nchi inapiga hatua.

Yani watu wamechoka akili mpaka wanatia huruma.

Yani Blenda na mashine za kufyatulia tofali kwao ni kiwanda.

Hawa watu ni wa kuwaonea huruma tu.
Wewe unaona inapiga nini?
 
Wala usishangae huyo chawa kukwambia Tanzania ina viwanda 28000.

Kwa ma CCM hata cherehani inahesabika ni kiwanda.
Chereni ni nini? Bado hujasema Hadi useme 👇
Screenshot_20260804-061311.jpg
 
Ni ujinga tu unaotusumbua. Hata kama una uchumi mzuri kiasi gani lakini huna utaalamu wa kutengeneza/kuunda chochote kile ndani ya Nchi yako kwa kutumia wataalamu wako, ujue huo wote bado ni ujinga tu.
Una uhakika hatuna utaalamu wa kuunda kitu ndani ya Nchi au unaropoka?
 
My Take
Nakubaliana na Prof.Kitila Mkumbo na kwamba nimewahi andika hapa jukwaani kuwa Mzungu yeyote hata asupotoa hata jero haiwezi yumbisha Tanzania Kwa sababu Bajeti yetu ya Zaidi ya Trilioni 62 inapata Msaada wa Mabeberu Kwa chini ya Trilioni Moja Kwa mwaka. Pia soma Ongezeko la bajeti ya serikali mwaka 2026/27 kutoka trilioni 55 hadi trilioni 62 ni ujumbe tosha kwamba Tanzania haitayumbishwa na mabeberu | JamiiForums Tanzania Ongezeko la bajeti ya serikali mwaka 2026/27 kutoka trilioni 55 hadi trilioni 62 ni ujumbe tosha kwamba Tanzania haitayumbishwa na mabeberu

Na kwamba Uchumi wa Tanzania wa karibu $100 B unaokua Kwa zaidi ya 5.5% Kila mwaka hautegemei misaada Wala hisani ya beberu yeyote.

In fact wanatakiwa waondoe kabisa Kwa sababu sehemu kubwa ya watu wapumbavu Huwa wanawaza misaada kana kwamba ni Haki Yao.

Mfano kina Morocco walimuahidi Marehemu Mwendazake kujenga uwanja lakini Leo hii tunajenga wenyewe viwanja vipya takribani 4 Bara na Visiwani bila Msaada wa beberu Wala kibaraka wao yeyote na mambo mengine yote yanaenda.Pia

Nchi itayumba kidogo ikikosa Mkopo na sio Msaada na Hilo la kukusa Mkopo halipo Kwa sababu tunaweza pata kokote kuanzia Iran Hadi South Africa.

Heko Prof.Kitila Kwa kuwapasha wao na vibaraka wao.

View: https://www.instagram.com/reel/Dbk8RbUibPT/?igsh=MTJtaThjYndwN2JmOA==

Kwa hiyo maana ya hiyo "labda watafute vikwazo vingine" ndiyo kitu pekee kitakachowayumbisha? Na je wakishatafuta hivyo vikwazo vingine mkayumbishwa mtawapigia magoti au mtapambano nao vita vya kiuchumi head-on?
 
Kwa hiyo maana ya hiyo "labda watafute vikwazo vingine" ndiyo kitu pekee kitakachowayumbisha? Na je wakishatafuta hivyo vikwazo vingine mkayumbishwa mtawapigia magoti au mtapambano nao vita vya kiuchumi head-on?
Hiyo kauli ya "labda watafute vikwazo vingine" nimeichukulia kwa uzito sana, Tanzania imefika level hizo kweli?
 
..sababu za kuwekewa vikwazo ni hoja nzito kuliko athari za vikwazo hivyo kwa Ccm.

..vikwazo vimekuja kwasababu ya Ccm kujihusisha na utekaji, utesaji, na mauaji, ya wakosoaji na wanaharakati.

..kiongozi asiyekuwa na utu, na uzalendo kwa Tanzania, ndiye anayeweza kuona ni sawa nchi yetu kuwekewa vikwazo kwa tuhuma za kukiuka haki za watu, na mauaji.
 
Back
Top Bottom