Prof. Kitila: Tanzania haitayumbishwa kwa sababu ya mabeberu kutunyima misaada, labda watafute vikwazo vingine

WAAMBIE watu Kwanini mmenyimwa misaada na hao mnaowaita MABEBERU??

Kwanini mnapopewa pesa hamsemi MABEBERU wametuchangia kiasi hiki?? Wanapowanyima mnabadili jina eti MABEBERU!πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
Kwani kupewa lazima?
 
Halafu wanakwambia nchi inapiga hatua.

Yani watu wamechoka akili mpaka wanatia huruma.

Yani Blenda na mashine za kufyatulia tofali kwao ni kiwanda.

Hawa watu ni wa kuwaonea huruma tu.
Wewe unaona inapiga nini?
 
Ni ujinga tu unaotusumbua. Hata kama una uchumi mzuri kiasi gani lakini huna utaalamu wa kutengeneza/kuunda chochote kile ndani ya Nchi yako kwa kutumia wataalamu wako, ujue huo wote bado ni ujinga tu.
Una uhakika hatuna utaalamu wa kuunda kitu ndani ya Nchi au unaropoka?
 
Kwa hiyo maana ya hiyo "labda watafute vikwazo vingine" ndiyo kitu pekee kitakachowayumbisha? Na je wakishatafuta hivyo vikwazo vingine mkayumbishwa mtawapigia magoti au mtapambano nao vita vya kiuchumi head-on?
 
Kwa hiyo maana ya hiyo "labda watafute vikwazo vingine" ndiyo kitu pekee kitakachowayumbisha? Na je wakishatafuta hivyo vikwazo vingine mkayumbishwa mtawapigia magoti au mtapambano nao vita vya kiuchumi head-on?
Hiyo kauli ya "labda watafute vikwazo vingine" nimeichukulia kwa uzito sana, Tanzania imefika level hizo kweli?
 
..sababu za kuwekewa vikwazo ni hoja nzito kuliko athari za vikwazo hivyo kwa Ccm.

..vikwazo vimekuja kwasababu ya Ccm kujihusisha na utekaji, utesaji, na mauaji, ya wakosoaji na wanaharakati.

..kiongozi asiyekuwa na utu, na uzalendo kwa Tanzania, ndiye anayeweza kuona ni sawa nchi yetu kuwekewa vikwazo kwa tuhuma za kukiuka haki za watu, na mauaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…