Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.
Inaonesha hqtq utaratibu wa kujiudhuru huujui,,lipumba hakutimiza vigezo vya kisheria vya kujiudhuru
Tufanye unachosema ni sahihi je Kwa miezi kumi ambapo hakuwa anafanya kazi alitegemea nani alikuwa anamfanyia kazi zake.

Ofisini kwenu unaweza kaa nyumbani miezi kumi alafu ukarudi ukaendelea na kazi zako kama kawaida?

Huyu Prof.[HASHTAG]#Lipumba[/HASHTAG] atakuwa na matatizo nani amempa hayo mamlaka na yeye kama nani? Naona anajitekenya na kucheka mwenyewe.

Mimi sasa hivi simushangai prof Lipumba kwani ninajua amechanganyikiwa,ninaye mshangaa ni huyu mtu anayejiita jaij mtungi kuhalalisha shudu kuwa mbegu.
Nenda mbali na kumshangaa huyo jajijechaccm no.2. CUF iko ktk wakati mgumu sana. Soon inapasuliwa kwa nguvu za dola itakayotumiwa na ccm.

Hivi tofauti ya wafuasi na mashabiki ni nini?

Wafuasi ni wale ambao mko nao pamoja
mfano wanachama wenzio wanakufuata...

mashabiki ni wale wanaokuunga mkono lakini sio wanachama....hawako kwenye chama

Hatua hii kaichukua kwa madai ya kwamba anakisuka chama upya. Professor Lipumba kachukua hatua hii mara baada ya jana kurudi katika kiti chake ikiwa ni maamuzi ya msajili wa vyama vya siasa, ambaye kisheria ndio mlezi wa vyama vyote vya siasa!...

Katika kauli yake, kasema hii ni hatua ya kawaida katika kusuka chama ili kiendane na wakati na kujipanga kwa uchaguzi wa meya Kinondoni na Ubungo, na uchaguzi mkuu wa 2020...

Pia, Prof. Lipumba kawaonya wabunge wa CUF kuacha kurukia mambo na kasema watii katiba, sheria, na kanuni za chama hicho vinginevyo watapoteza nafasi zao

Hayo yakiwa yanaendelea kwa upande mwingine viongozi wa mpito wakiongozwa na Mtatiro na Maalim Seif wameitisha baraza kuu itakayofanyika siku ya Jumanne Zanzibar ili kutoa kauli ya pamoja ya kupinga maamuzi ya Jaji Mtungi

Tik tak tik tak tik tak!! Nikiona hivi naikumba NCCR - Mageuzi ya 1995 baada ya uchaguzi! Ngoma ndio kwanza mbichi kabisa.

Hivi maandamano yanaruhusiwa?

Kuna wakati napata shida uelewa wa jinsi jeshi linavyofanya Kazi. Wanasema ukisimamishwa na traffic marufuku kushuka kwenye Gari lakini....haitekelezwi. Wanasema hakuna maandamano......angalia hayo ya lipumba

Wanasema waangalizi wa a man I lakini office za chama zinavunjwa bila kibali cha mahakama.....wanaangalia.

Mkuu The Boss, nimekuelewa kadri ya uelewa wangu, na bado ninakudai utuwekee hapa hayo 'madai' ya wafuasi wa Lipumba dhidi ya Seif na Mtatiro...

Madai yao makuu wafuasi wa bara ni chama kujali siasa za Zanzibar zaidi
kutojali yanayotokea huku bara
hadi ruzuku na rasilimali kutumikia Zanzibar zaidi......
ni kama wabara wanaburuzwa...Seif kuwa kama ndo mwenye sauti ya mwisho kuliko yoyoye...
na sasa Mtatiro ni kama anatumika kuwa kibaraka....

Niliwahi kuuliza humu CUF Lipumba yuko peke yakeau ana wafuasi?

naona kumbe kina Mtatiro hawajui wanachofanya

Halafu Mtatiro nae kahamia Zanzibar?
Prof ana wafuasi wengi sana, kuanzia kwa mkulu wa nchi mstaafu adi wa Ngosha, apo achana na majaji, mapolisi na msajili

Hii ni sababu mojawapo ya kwa niji Mbowe ataendelea kuheshimika sana. Kwa sababu ni kiongozi mwenye msimamo lakini pia mwenye uwezo wa kuiona hatari kabla haijatokea.
NCCR waliangamia kwa mbinu chafu kama hizi zinazoendelea sasa za kuiangamaiza CUF.

Mbinu kama hizi wakati wote hazijaweza kumshinda Mbowe. Mbowe huziona kabla hazijatokea, na huchukua hatua kabla ya madhara kutokea. Kama siyo uimara wa Mbowe na wenzake ngazi za juu, huenda CHADEMA ingekuwa imeparanganyika zamani sana.

CHADEMA waendelee kuchukua tahadhari kubwa maana nao hawapo salama kwa mbinu kama hizi zinazotumika kwa CUF. NI rahisi sana chama kuvurugika kama mshindani wako anaweza kupenya mpaka kushika nafasi ya juu kabisa katika chama. Walitaka wafanye hivyo kwa CHADEMA lakini walishindwa, wakaishia tu na maneno kuwa ndani ya CHADEMA kuna udikteta, Mbowe ni dikteta, Mbowe ni mwenyekiti wa maisha, n.k. lakini yote hayo ni kwa sababu Mbowe hapenyeki.

VP uchaguzi wa cuf lini? au ndo alipouvuruga profesa ndo bac tena! Swali la kizushi!,hv katiba ya cuf ni lazima mwenyekiti awe mnyamwezi au msukuma? Nikichukulia wenye viti wote waliowahi kushika nafasi hiyo james mapalala, nsobi mageni(baba mzazi wa mbunge wa zamani Leticia Nyerere
marehemu na profesa ngangari).

Nahisi umeya wa Ubungo na Kinondoni kuludi CCM. Mission complete chezea ccm wewe mahesabu ya mbali kabisa mkishtuka tayali zamaani wamemaliza michezo
Kwa mwendo huu hatutakuja kuiondoa CCM Lipumba anashiriki kikamilifu kuwagawa wanachama ili CCM itereze bila kikwazo,namchukia sana huyo kibaraka

Kuna mdudu tayari ndani ya Cuf....tusubiri tuone mmeng'enyo wake. Hakika kwa mtindo huu hakiwezi kuwa imara tena kama chama pinzani zaidi ya kuudhoofisha upinzani...Huyu siyo Lipumba yule tena.!

Prof hakikisha unamzamisha kwenye maji marefuu mtatilo kama ulivyomlea ndivyo unavotakiwa kumzamisha kwenye maji marefu ili akitoka ajue wew ni msomi wa uchumi

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom