Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.
Nalikumbuka swali lako... na wakati watu tunaelezea uhalisia, wengine walitukejeli! Leo hii inashangaza kuona mtu asiye na wafuasi lakini bado ameweza kuingia HQ! Na tukiweka unafiki pembeni, hata hapa JF tunaowaona wapo sana upande wa akina Mtatiro ni watu wa CHADEMA ndio wengi kuliko CUF!
Hata wale wajana sio wa CUF utaona watakapo ishia.
 
Sio threat kwa ccm, ila the hpothesis so far, which is greatly turning into a fact, is that they are using this situation as a way ya kudhoofisha ukawa pia.Since CUF ni moja ya chama kikubwa kilichokuwa kinatengeneza ukawa, so wakifanikiwa kumback up Lipumba(through msajili wa vyama vya siasa na polisi as we have seen) akafanikisha agenda yake. Then cuf itakuwa imedhoofika vya kutosha which will inturn put huu muungano wa ukawa at risk.
Na Mie Nahofia Ilo
 
Kikao kilichoketi 28,August kilitangaza kumfukuza uanachama Lipumba.
Ile ilikuwa planned baada ya kuwa amejiuzulu na akaleta fujo kwenye kikao kisichomhusu. Wewe ujiuzulu kwa barua si kwa maneno halafu urudi use m/kiti wa kikao wapi na wapi ?
 
Hatua hii kaichukua kwa madai ya kwamba anakisuka chama upya. Professor Lipumba kachukua hatua hii mara baada ya jana kurudi katika kiti chake ikiwa ni maamuzi ya msajili wa vyama vya siasa, ambaye kisheria ndio mlezi wa vyama vyote vya siasa!...

Katika kauli yake, kasema hii ni hatua ya kawaida katika kusuka chama ili kiendane na wakati na kujipanga kwa uchaguzi wa meya Kinondoni na Ubungo, na uchaguzi mkuu wa 2020...

Pia, Prof. Lipumba kawaonya wabunge wa CUF kuacha kurukia mambo na kasema watii katiba, sheria, na kanuni za chama hicho vinginevyo watapoteza nafasi zao

Hayo yakiwa yanaendelea kwa upande mwingine viongozi wa mpito wakiongozwa na Mtatiro na Maalim Seif wameitisha baraza kuu itakayofanyika siku ya Jumanne Zanzibar ili kutoa kauli ya pamoja ya kupinga maamuzi ya Jaji Mtungi
Ujio wa Li-Pumba CUF unafurahiwa na Wana-Lumumba zaidi kuliko wana CUF wenyewe
 
Usipate shida sana mkuu. Ni suala la ZANZIBAR na uchaguzi uliovurugwa na Jecha. Hapa lengo ni kuifuta CUF kama ni chama cha siasa ili suala la uchaguzi Zanzibar liwe halina mashiko kwa Maalim Seif as his political party will be no longer existing!

Kitakachofata kutoka hapo ni Independent Zanzibar. Mark my words!
Huu ndio ukweli na watafanikiwa...ni hatari sana
 
Wakishaenda nini kitatokea? Au unataka wale wahuni na polisi wanaomlinda Lipumba wawaletee vurugu ndio ufurahi? Hivi Lipumba alivyoniuzulu CUF haikuwa na wafuasi ? Ndio maana nimekuambia kama ni wafuasi hata Diamond anao na wewe ni mmoja wa wafuasi wake!
Maneno mengi ya nini wakati nimeshaweka proposal mezani?
 
Safi sana Profesa Lipumba fyeka wote hapo, safisha chama chake
 
Ngunguri Vs Ngangari
1474803358893.png
1474803374803.png
1474803391223.png
 
Profesa anadai haki yake kwani kadhalilishwa sana na Sefu...

Hujiulizi kwanini vikao vinafanyikia Zanzibar na sio Bara?

Sefu atamjua tu Profesa maana hajui mziki wake. Mziki wa Profesa sio wa Dr Slaa ambaye aliiacha Chadema akaenda ughaibuni...Profesa ni Jino kwa Jino hasaaa yaani ni Ngangari kinomaaaa...
Kile kikao kilichofanyika Ubungo Plaza mpaka Lipumba na Kundi lake wakaingilia kuvuruga kikao ilikua Zanzibar ile??
 
Sefu kaona urais wa Zanzibar haupati tena...kaamua kukivuruga chama upande wa Bara...

Wana CUF wa Bara msikubali maamuzi wa Chama yakawa yanafanywa na Wazanzibari peke yao. Nyie mnayo haki na chama kinao wanachama pande zote mbili.

Hakuna mtu aliyejitolea kukijenga chama kwa hali na mali kama Profesa. Msimuache peke yake Profesa katika hili...pambaneni na ikishindikana basi gawaneni mbao...CUF Zanzibar iongozwe na Sefu na Mtatiro na CUF Bara iongozwe na Profesa na Magdalena Sekaya..
 
Mkuu kwanza Wabunge wote wa Bara wako na Lipumba. Mtatiro yuko pekee na alitumika kama chambo cha kuaminisha watu wa bara.

Ila huu mchezo una maana sana kisiasa. Vyama vyetu huwa vina amua vitu kama havina vikao vya maamuzi. Ni mwaka CUF walishindwa kutoa maamuzi ya Lipumba kujuuzuru. Sasa ndo wanaona kuna nini ndani.

Huwa tunafanya kazi kwa mazoea sana.
Niliwahi kuuliza humu CUF Lipumba yuko peke yakeau ana wafuasi?

naona kumbe kina Mtatiro hawajui wanachofanya


Halafu Mtatiro nae kahamia Zanzibar?
 
Lipumba anao wafuasi.....asidharauliwe.....ndio maana kina Mtatiro wanakimbilia Zanzibar.

Suluhisho:
Seif na Lipumba wajifungie waongee kiutu uzima wayamalize.....wao ukitazama kwa ndani hawana ugomvi.
 
Wasomi wetu wanatumika vibaya.kwa mtindo huu tutabaki kuwa watu wa zama za mawe.
 
Kile kikao kilichofanyika Ubungo Plaza mpaka Lipumba na Kundi lake wakaingilia kuvuruga kikao ilikua Zanzibar ile??
Tunazungumzia ya sasa na sio ya kale...kwanini vikao vyote sasahivi ni Zanzibar?.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom