Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.
Tunazungumzia ya sasa na sio ya kale...kwanini vikao vyote sasahivi ni Zanzibar?.
CUF bara haikubaliani na jinsi Seif anavyoiacha CUF isemewe na CDM ( lowassa).

Vijana wa ngangari washaijua janja hii ya nyani [emoji1] [emoji1]
 
Unaweza kuwa hunielewi
sisemi Lipumba hatumiki
au Lipumba anafaa....ninachosema ni kuwa ana wafuasi
na hao wafuasi wana 'madai' yao.....

Sio Seif au Mtatiro anaeonekana kujali hao wafuasi
wao wako tayari Lipumba aondoke na hao wafuasi....
ndo maana huu mgogoro unazidi kukua
Mkuu The Boss, nimekuelewa kadri ya uelewa wangu, na bado ninakudai utuwekee hapa hayo 'madai' ya wafuasi wa Lipumba dhidi ya Seif na Mtatiro...
 
Watu wengi wanapenda kufanya mambo kihisia tu
hawataki kutazama reality....Lipumba hata kama kanunuliwa na CCM..
akiweza kuwa na wafuasi tu basi ni tatizo
siasa ni watu na sio sheria...
Hivi tofauti ya wafuasi na mashabiki ni nini?
 
Kwani wewe unafikiri hili Li-Pumba lina akili. Kaandika barua ya kujiuzulu na kuikimbia ofisi. Kama aavyosema kuwa hajajibiwa barua yake, mbona alikuwa hhudhurii kazini? Barua yake haikuomba aruhusiwe kujiuzulu, alitamka kujiuzulu na ikfuatiwa na safari ya nje ya nchi ya kazi zake binafsi. Muajiri gani atakayekuruhusu kutokuwepo ofisni kwa miezi zaidi ya tisa halafu uamaue tu kurudi ofisini. Hata hizo sheria za kazi zinaruhusu? Huyo msajili wa Chama angepelekewa audited account ya matumizi ya chama na kuonesha expenses za Li-Pumba wakati ana haha mitaani angezikubali kwa vile on his own words kwamba Li-Pumba bado aliendelea kuwa mwenyekiti wa Chama? CUF kuitisha uchaguzi mpya wa kum replace haikuwa na maana kwamba resignation yake imeshakubalika?
Kama una ile video yake ya Dhamira kumsuta itupie ili tujikumbushe.
 
Siasa za Tanzania zina mengi sana
Lipumba kabla hajajiuzulu aliwahi kutaka kujiuzulu zamani
sababu ni Seif kuwaburuza wana CUF wa bara
na wana CUF wa bara wanalijua hilo
alianza kupata 'die hard fans' kwa hilo..kitendo cha juzi Seif kumchagua
Mtatiro kimezidisha tatizo......wao hawataki 'mwenyekiti kibaraka'
na Seif kafanya exactly wasichotaka.....na sasa kila kitu kinaamuliwa Zanzibar...

Hili la kusema Lowassa ndo sababu nil la juu juu sana...
Hawa wafuasi wa Lipumba wana mengi sana...ndo maana huu mgogoro unazidi kuwa mkubwa....
Kwamba maamuzi yote yanatokea Zanzibar hilo lipo wazi na Mtatiro anatumika tu na CUF Zanzibar!

Kuhusu Lowassa, naamini sio tatizo lakini naamini Maalim Seif ana hofu kurejea kwa Lipumba kutahatarisha uhusiano wao na UKAWA kv tu Lipumba hakuwa kwenye good terms na EL! Siamini kwamba kinachomvuta Maalim Seif UKAWA ni uhusiano wa kisiasa kwa ujumla wake bali kuitumia UKAWA ktk agenda ya Zanzibar! Kisiasa, CHADEMA na CUF ni vitu viwili tofauti!!
 
Mbona Maandamano ya Hawa hayajaTawanywa na FFU , Wakati Maandamano yamekatazwa Nchi Nzima? Polisi Wamelazimika Kuyaruhusu haya Kwa Amri ya Nani?
Walikuwa na barua ya kisheria kutoka kwa msajili wa vyama, ruhusa ya kuingia ofisini kisheria
 
Hili swali ni la msingi sana, binafsi nashindwa kuelewa hii jeuri na nguvu Prof. Lipumba anaitoa wapi, kama hakubaliki au hana wafuasi ndani ya CUF anapata wapi ujasiri wa kutaka kurudi kwenye nafasi ya uenyekiti? akamuongoze nani? Nadhani kuna shida miongoni mwa viongozi ndani ya CUF, wanajaribu kujenga picha ya kwamba Lipumba hana wafuasi na hakubaliki ndani ya CUF lakini katika reality inaonekana ana backup ya watu.
Hata kama hana, atatafutiwa wafuasi. Wasípokuwa makini CUF is gone..,na hii ni hatari sana kwa mstakabali wa Zanzibar. Anatafutwa Maalím Seif kwa kumtumia Lípumba. This is so sad, siasa si muda mlefu zinatupeleka ťusikotaka
 
Sawa tulikubali lipumba ni kikwazo lakini safari hii ni kikwazo ZAIDI maana nyoka amepita huko na huko na sasa Yuko NDANI ya nyumba tena kwa mara nyingine tena
Kumtoa huko ni shughuli haswaa!
Kweli kabisa chief nyoka yupo ndani ya nyumba.....hata sijui kaibukia wapi huyu kumbe,labda kwa vile sijui sheria maana nisingeona shida kumburuza nje bila huruma.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom