rasmi 25/09/2016 kwa 9:15 mu · Jibu
Hivi ccm wanafikiri kufanya hivi ndio kutapunguza kasi ya mabadiliko Zanzibar!
Huyu mzee ameshajulikana atalolifanya ni kuitaambua serikali ya Dk Shein, baada ya hapo kuna wasaliti ambao wataingizwa kutoka CUF kwenye hiyo serikali ya Dk Shein kuonyesha kwamba ina uhalali na CUF wanaitambua.
CCM wanatengeneza tatizo jengine tu hapo hamna mafanikio watayoyapata, Lipumba na hicho kikundi chake hatokubalika Zanzibar abadan.
Kwa wakati huu wamechelewa mbinu hii ya wagawe uwatawale haifanyi kazi katika akili za Wazanzibari walio wengi…
Elbattawi 25/09/2016 kwa 11:14 mu · Jibu
rasmi
Kila mtu anayechukia ukoloni wa CCM, anafahamu fika kwamba Lipumba ana ‘issue’ kibindoni tayari alizopangiwa na CCM, anakujanazo ndani ya CUF kwa kuzitekeleza.
(l) Kutaka kuzima au kubabaisha mataifa katika madai yaliyopo juu ya meza ya wazanzibari kuhusiana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015.
(ll) Kama ulivyosema kwamba atataka kuitambua au niseme atajaribu kusema kwamba uchaguzi wa marudio wa Machi 20 ulistahili kisheria na kikatiba kufanywa, hivyo ulikuwa halali. Atasema, baada ya kutafakari vya kutosha CUF, imebadilisha uamuzi wake na sasa inaitambua serikali ya Dk Shein.
(lll) Pia, ana mkakati mzito aliyopangiwa na CCM, kufumfukuza Maalim Seif na viongozi wengine (kundi lake) ndani ya CUF (this is very serious issue), kwa sababu ya kutaka kuwachanganya kimawazo au kuwababaisha wazanzibari, wanachama na wafuwasi wa CUF, juu ya mwelekeo wa Zanzibar.
Itakumbukwa mkutano wa Kiembe Samaki wa CCM, Balozi Seif Ali Iddi (Nduli) alisema nini kuhusu CUF kuwa, mwaka huu ndiyo mwisho wake. Uchambuzi wa kitaalamu wa kauli ile ndiyo haya matokeo ya sasa.
Kuna mambo mengi ya ubaya dhidi ya wazanzibari waliyoikataa CCM, Lipumba anakuja nayo kapewa kuyatekeleza. Ndiyo sababu ‘speed’ au niseme kasi ya kumrejesha imekuwa kubwa.
CCM, wanahofu na hatua zinazochukuliwa na CUF chini ya Maalim Seif kuhusu Zanzibar na Tanzania, ambayo nayo inaathirika zaidi.
Ingawa kwa sasa tunaweza tukasema kwamba, kwa hatua iliyofikiwa kuhusu masuala ya Zanzibar, CCM wananafasi finyu na ndogo mno kunusurika na mkono wa dunia. Ndiyo maana wanajaripu kupapatua kwa njia za kijasusi, kupitia uhuni wa Lipumba na gengi lake.
Inafaa tujiulize, tena tujiulize sana tangu CUF kuasisiwa, sasa ni miaka 24 kwa hesabu, lini imetokea Mwenyekiti wake, kuanzia Mapalala kupelekwa ofisini kwa vikosi vya polisi, geti la ofisi kuvunjwa, walinzi kupigwa mabomu na uhalifu mwingine kama kweli kuna nia njema huko mbele.
Kwa Wazanzibari, haya si mageni labda kwa wenzetu upande wa bara ambao wao kwao yanaweza kuwa mageni, hawaifahamu CCM hulka yake kwa undani. Ingawa sasa kidogo kidogo wameanza kupata picha. Wazanzibari chini ya CUF, wamewazoea CCM wala hawawababaishi tena.
CCM, wanaamini kuwa dunia yote ni kama vile serikali yao ilivyo, viongozi kutembea kwa ving’ora na misururu ya gari za ulinzi kuelekea katika mikutano ya kinafiki ya hadhara na kurudi majumbani, wakisubiri siku inayofuta kwenda mashamba Unguja na Pemba, kudanganya watu. Dunia haiku hivyo tena sasa, imebadilika. Sindano ikianguka mto-pepo, dakika hiyo hiyo wanaisikia waliyoko Toronto.
Umoja wa ulaya (EU) imesema kuhusu uchaguzi wa Zanzibar, Jumuiya ya Madola (Commonwealth), Marekani na Uingereza na kadhalika wote wamesema na kutokuitambua Serikali ya Zanzibar, Lipumba anarejeshwa CUF kwa mabavu na ajenda ya kigaidi. Nani atamkubali kumpokea gaidi mkuu wa wazanzibari?.
Mwaka wa kwanza Julius Nyerere, kufanya ziara Pemba, ilikuwa mwaka 1965 hapa ilikuwa ni mwaka mmoja tangu kuunda Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Mzee mmoja mwenye asili ya Tanganyika, Ibrahim Mkumba alitunga na kughani utenzi kwa ajili ya Nyerere.
“Kila ajaye kwa shari – Aijuwa yake siri – Ivunde yake dhamiri – Asiweze kusimama.”
Maneno hayo ya ushairi yalikuwamo ndani ya utenzi uliyokuwa na zaidi ya beti 110 uliyoghaniwa na Mzee Ibrahim Mkumba aliyekuwa akiishi Chanjamjawiri, pale kwenye njia inayoelekea Skuli ya Kidongo (sasa Skuli ya Chanjamjawiri).
Kwa fumbo la kishairi la Mzee Mkumba, hatunashaka kwamba, dhamira aliyonayo ndani ya nafsi yake Ibrahim Lipumba, itamsuta na hataweza kusimama. Mwenyezi Mungu Jala Jalal, hatasimama naye, hatampa nguvu za kuweza kuwafanyia ugaidi wanzanzibari. – amin.
Wazanzibari, mjini na mashamba, Pemba na Unguja ni waelewa wa mambo yote kuhusu nchi yao. Miaka zaidi ya 50 ya Muungano ‘uchwara’ wamekumbana na mengi na sasa wamechoka kuishi katika hali ngumu ya umasikini na ufukara, hawatatetereka tena na mbinu ovu za CCM. Wazanzibari wako makni sana.