Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.
Duuu ! Kwa uelewa huu , safari bado ndefuu! !
 
Watu wengi wanapenda kufanya mambo kihisia tu
hawataki kutazama reality....Lipumba hata kama kanunuliwa na CCM..
akiweza kuwa na wafuasi tu basi ni tatizo
siasa ni watu na sio sheria...
Watu gani aliokuwa nao huyu Lipumbaa !!
 
Nahisi umeya wa Ubungo na Kinondoni kuludi CCM. Mission complete chezea ccm wewe mahesabu ya mbali kabisa mkishtuka tayali zamaani wamemaliza michezo
Akili kumkichwa dadadeki
 
Prof, vipi unaamua kula matapishi yako, ulichotegemea kitatokea, hakijatokea?
Unda chama chako wafuasi unao.
Tayari kimetokea!! Sasa ni kumkabili tuu maana nyoka amekwishaingia ndani ya nyumba inahitajika Akili na ubabe wa hali ya juu maana hapo sioni hekma wala busara kuweza tena kutatua huu mgogoro ukizingatia kila mmoja anajiona NGANGARI.
 

Mkuu chabusalu.
Inawezekana kabisa kuwa huyu Lipumba wa kuanzia 2010 ni tofauti na Lipumba wa awali. Ni vyema tuichukue hiyo kama nadharia isiyo na uthibitisho kamili.
Hebu turudi nyuma kidogo na kutafakari uhusiano wa kiutendaji kati ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake kwenye vyama hivi (CUF/CHADEMA) kwa maana ya (Lipumba/Seif na Mbowe/Slaa). Ni dhahiri utakuta kuna matatizo makubwa yanayo pelekea kuwa na taswira inayo fanana.
Kwenye hivi vyama baadhi ya viongozi hujifanya miungu watu na kutoa maamuzi ambayo si shirikishi na hakuna uwajibikaji wa pamoja. Hebu tujaribu kufikiri kuanzia hapo.
 
Naanza kuhisi kuna mkono wachuma hapa....

Kwanini mtu ang'ang'anie madaraka na alishasusa huko nyuma?

Kipi ambacho kimebadilika?

Au lengo lilikua kuona CUF imesambaratika na halijafanikiwa hilo? Kwanini kutumia mabavu?
 
Mkuu Zinj, ukitaka tuanze kufikiri kuanzia kwenye huu "umungu watu ndani ya vyama" itabidi uwe tayari pia kuzungumzia ugumu wa kuendesha upinzani dhidi ya serikali katika mazingira ya Tanzania. Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya mambo haya mawili. Sijui kama uko tayari, kama jibu lako litakuwa "ndiyo", basi nikusihi tu uanze kwa kutonyesha hapa angalau mifano miwili ya "umungu watu ndani ya vyama" ambao ungependa tutumie kama "case study"!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…