Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.
CUF wanamtihani mgumu Sana kumuua nyoka ambaye yumo ndani ya kibuyu Chao,hapa Lipumba siyo kwamba ana kisuka Chama Bali ana suka uwenyekiti wake kwa kuwafukuza wanaompinga na kuwaingiza wanaomkubali Ili uchaguzi utakapo itishwa aweze kushinda kilaini naona huyu professor alipokuwa kimya alikuwa ana hudhiria mafunzo ya kuiua CUF.
 
Niliwahi kuuliza humu CUF Lipumba yuko peke yakeau ana wafuasi?

Hili swali ni la msingi sana, binafsi nashindwa kuelewa hii jeuri na nguvu Prof. Lipumba anaitoa wapi, kama hakubaliki au hana wafuasi ndani ya CUF anapata wapi ujasiri wa kutaka kurudi kwenye nafasi ya uenyekiti? akamuongoze nani? Nadhani kuna shida miongoni mwa viongozi ndani ya CUF, wanajaribu kujenga picha ya kwamba Lipumba hana wafuasi na hakubaliki ndani ya CUF lakini katika reality inaonekana ana backup ya watu.
 
Na walisema hatarudi Buguruni...
sasa yupo Buguruni guku wao wamekimbilia Zanzibar
 
duh, inabidi watafute njia ya kudeal na huyu jamaa kabla hajaleta further damage
Cause hali ikiendelea hivi, chama kinaonekana kiko on the edge ya kuparanganyika
Ila this prof should REALLY be ASHAMED of himself kwa huu ujinga anaofanya na kukubali kupelekeshwa kuharibu/dhoofisha chama ambacho amekuwa nacho na kukitumikia for years.
But, yawezekana napata shida kuunganisha dots. Hivi ni kweli CUF ndiyo great threat kwa CCM? I'm just curious, I guess there is something wrong within CUF itself, I'm not happy with what happens to CUF but I think the party members should open up the box and see what eats them inside
 
Hatua hii kaichukua kwa madai ya kwamba anakisuka chama upya. Professor Lipumba kachukua hatua hii mara baada ya jana kurudi katika kiti chake ikiwa ni maamuzi ya msajili wa vyama vya siasa, ambaye kisheria ndio mlezi wa vyama vyote vya siasa!...

Katika kauli yake, kasema hii ni hatua ya kawaida katika kusuka chama ili kiendane na wakati na kujipanga kwa uchaguzi wa meya Kinondoni na Ubungo, na uchaguzi mkuu wa 2020...

Pia, Prof. Lipumba kawaonya wabunge wa CUF kuacha kurukia mambo na kasema watii katiba, sheria, na kanuni za chama hicho vinginevyo watapoteza nafasi zao

Hayo yakiwa yanaendelea kwa upande mwingine viongozi wa mpito wakiongozwa na Mtatiro na Maalim Seif wameitisha baraza kuu itakayofanyika siku ya Jumanne Zanzibar ili kutoa kauli ya pamoja ya kupinga maamuzi ya Jaji Mtungi
Mtu aliyejiuzuru katikati ya mapambano Leo Ana sema kuwa ana kisuka Chama kwa ajili ya umeya wa Kinondoni,huyu sheni anayetumiwa na CCM Ili UKAWA wasishinde umeya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom