Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.
Hatua hii kaichukua kwa madai ya kwamba anakisuka chama upya. Professor Lipumba kachukua hatua hii mara baada ya jana kurudi katika kiti chake ikiwa ni maamuzi ya msajili wa vyama vya siasa, ambaye kisheria ndio mlezi wa vyama vyote vya siasa!...

Katika kauli yake, kasema hii ni hatua ya kawaida katika kusuka chama ili kiendane na wakati na kujipanga kwa uchaguzi wa meya Kinondoni na Ubungo, na uchaguzi mkuu wa 2020...

Pia, Prof. Lipumba kawaonya wabunge wa CUF kuacha kurukia mambo na kasema watii katiba, sheria, na kanuni za chama hicho vinginevyo watapoteza nafasi zao

Hayo yakiwa yanaendelea kwa upande mwingine viongozi wa mpito wakiongozwa na Mtatiro na Maalim Seif wameitisha baraza kuu itakayofanyika siku ya Jumanne Zanzibar ili kutoa kauli ya pamoja ya kupinga maamuzi ya Jaji Mtungi
Kazi ipo....
 
Ndugu umegonga kwenye uhalisia, mimi mara ya kwanza kushangaa ni kwenye mkutano wa baraza kuu la Taifa ambao uliisha kwa fujo. Niliangalia ule mkutano na nikastushwa na back up aliyokuwa nayo Prof, uhalisia wa kule ni tofauti na wa huku mtandaoni. CUF bara walikuwa bado wanamtaka Prof wakati CUF visiwani walikuwa watiifu kwa Maalim.
Kwani haiwezekani hao 'wafuasi' 'wakatengenezwa' na CCM? CCM will do ANYTHING to weaken its opponents!
 
But, yawezekana napata shida kuunganisha dots. Hivi ni kweli CUF ndiyo great threat kwa CCM? I'm just curious, I guess there is something wrong within CUF itself, I'm not happy with what happens to CUF but I think the party members should open up the box and see what eats them inside
Sio threat kwa ccm, ila the hypothesis so far, which is greatly turning into a fact, is that they are using this situation as a way ya kudhoofisha ukawa pia.Since CUF ni moja ya chama kikubwa kilichokuwa kinatengeneza ukawa, so wakifanikiwa kumback up Lipumba(through msajili wa vyama vya siasa na polisi as we have seen) akafanikisha agenda yake. Then cuf itakuwa imedhoofika vya kutosha which will inturn put huu muungano wa ukawa at risk.
 
1474800712241.jpg
 
Ama kweli wimbo wa kufundwa haukeshi ngoma!
Prof. Lipumba si mwanasiasa wala hana charisma ya kuongoza. Aliwahi kukiri wakati alipokuwa Bunge Maalum 2014 kuwa CUF si chama chake bali yeye aliitwa tu mwaka 1995 wakati wa kutafuta mgombea urais ili abebe bendera ya CUF. Alikiri kuwa alikubali dhamana hiyo kwa vile iliambatana na fungu kubwa alilokabidhiwa. Hivyo vitendo anavyofanya leo hii Mhe. Lipumba si bahati mbaya, bali yeye hana uchungu na chama hicho. Hata kikisambaratika ili mradi anapata fungu yuko tayari kukisaliti kama Yuda Iskariyote alivyomsaliti Yesu Kristo kwa kulipwa Shekeli 30.
Tunaomba sana viongozi wa dini wamuombee Lipumba ili Mwenyezi Mungu amfungue minyororo ya giza iliyomfunga. Kwa miaka 20 aliyoongoza chama hicho alifanya kazi ya kutukuka ambayo kama angestaafu kwa heshima na kurudi kufundisha Chama kingemuenzi daima. Hata Taifa lingethamini mchango wake kwa ustawi na maendeleo ya demokrasia nchini. Kwa bahati mbaya kama ambavyo nilianza kwa kusema kuwa "wimbo wa kufundwa haukeshi ngoma" ni dhahiri kuwa Lipumbe ana price tag. Watanzania wakae macho na Lipumba na Mhe. Rais asije akadanganyika akamteua Lipumba kumwakilisha popote kwani hatasita kusaliti Taifa akipatiwa fungu linalotuliza moyo wake. Hakika laana ya kukisaliti chama kilimchomkuza kisiasa kitatatfuna hadi ukoo wake wote. Lipumba amelaaniwa!!!!!!!!
 
Mtatiro hana kabisa influence kwa wana cuf wa Buguruni pale na bara kiujumla...
ilo ni tatizo lingine....
Kwa mwendo huu makao makuu yanaweza hamishiwa Zenji, sidhani kama CUF ya Maalim unaweza tena pata support au kuwarudisha wafuasi wengi watakao wapoteza baada ya hii dhoruba.

Lakini kitu kikubwa zaidi ni impact ya huu mgogoro kwa CDM 2020, kuna wabunge wengi wa UKAWA watadondoka kwa sababu ya huu mgogoro. Ni wazi majimbo ya Dar na Tanga yatarudi CCM kama hakutakuwa na UKAWA. CDM wanafikiria kuhusu umeya wa kesho kutwa ambao hata kama UKAWA ikivunjika bado wanaweza kuwa confront madiwani wachache tu wa CUF na kushinda badala yake inabidi waanze kufikiria 2020. Hiyo ni kete dume imerushwa na CCCM.
 
Ndugu umegonga kwenye uhalisia, mimi mara ya kwanza kushangaa ni kwenye mkutano wa baraza kuu la Taifa ambao uliisha kwa fujo. Niliangalia ule mkutano na nikastushwa na back up aliyokuwa nayo Prof, uhalisia wa kule ni tofauti na wa huku mtandaoni. CUF bara walikuwa bado wanamtaka Prof wakati CUF visiwani walikuwa watiifu kwa Maalim.
lipumba ana kundi lake la watu wachacbe wanaomsapoti.....Hata dr.slaa akirudi leo chadema wapo wengi tu ndani ya chama watamsapoti..
 
Civic United Front sasa inakwenda kuzikwa rasmi. Bwana Lipumba yupo anamalizia kupigilia misumari ya mwisho mwisho aliyoanza kuipiga 20 years ago.
 
Wanyamwezi ni wasaliti sana fuatilia mkoa wa tabora kama kuna upinzani labda kidogo kaliua halafu angalia maendeleo wengi ni waendesha baiskeli njaaa kali kwa hiyo sitishangaa huyo jamaaa kutumiwa kama kondom
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom